Dkt. Mpango: Marufuku kwa wakala wa Ajira kujigeuza kuwa waajiri

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
166
629
Akizungumza kwenye Sherehe za Mei Mosi Jijini Arusha, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema ni marufuku kwa wakala wa Ajira kujigeuza kuwa waajiri, jambo hili ni kinyume cha Sheria na halikubaliki.

"Jukumu la msingi la mawakala kwa mujibu wa Sheria ya kukuza huduma za ajira linabaki kuwa ni kuunganisha watafuta kazi na waajiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo, ni kosa kwa wakala kugeuka kuwa waajiri wa watafuta kazi" amesema Dkt. Mpango.

Amebainisha Serikali imepokea ushauri wa kuendelea kuwasimamia mawakala ili watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa Sheria na Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kudhibiti kitendo hiki.

Aidha, serikali itafanyia mabadiliko sheria ya kukuza huduma za ajira kwa lengo la kufuatilia usimamizi wa Mawakala hao.
 
Back
Top Bottom