Dkt. Mpango: Maneno yanayosemwa mtaani, kwamba hali ya uchumi ni mbaya yanaenezwa na wapiga dili

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939

WAKATI idadi kubwa ya wananchi wakilalamikia ugumu wa maisha unaowakabili, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Arusha na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini.

Pamoja na hayo, Dk. Mpango alisema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa.

“Tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

“Mbali na Repoa, zipo taasisi nyingine ambazo zinaendelea na uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi.
“Nilishasema bungeni na narudia tena, kwamba kwa vigezo vyote vya kimataifa, tutaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwani hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limetoka hapa nchini hata mwezi haujapita, nao wamechambua mwenendo wa uchumi wetu na kusema uchumi wa nchi yetu ni mzuri.

“Maneno yanayosemwa mitaani, kwamba hali ya uchumi ni mbaya na fedha zimepungua katika mzunguko yanaenezwa na wapiga dili.

“Katika hili, nawatoa hofu wananchi, kwamba hali ya uchumi iko imara na hayo maneno yanayosemwa si ya kweli bali tufanye kazi kwa bidii,” alisema Dk. Mpango.

Alisema pia kwamba deni la taifa na mauzo ya ndani na nje yanakwenda vizuri ingawa ukame unaonyemelea nchi, unaweza ukasababisha upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa.

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, alizishauri benki na taasisi nyingine za fedha kuhakikisha zinawafikia Watanzania wengi kwa kuwashirikisha kutoa mchango wa kifedha.

Chanzo: Mtanzania
 
WAKATI idadi kubwa ya wananchi wakilalamikia ugumu wa maisha unaowakabili, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri
Hili gazeti la Bashe lina vituko kweli....utafiti upi umefanya kugundua 'wananchi wengi'

“Tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

“Mbali na Repoa, zipo taasisi nyingine ambazo zinaendelea na uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi.
“Nilishasema bungeni na narudia tena, kwamba kwa vigezo vyote vya kimataifa, tutaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwani hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limetoka hapa nchini hata mwezi haujapita, nao wamechambua mwenendo wa uchumi wetu na kusema uchumi wa nchi yetu ni mzuri.
kwanini hujajikita na habari za utafiti wa Repoa, umekuja na ramli?
 
Jamaa yupo kwenye kiyoyozi ana shida gani?
Na hawa ndio washauri wa Rais.
Sasa mimacho itawatoka kwenye uchaguzi.
Wale jamaa wa ccm waliokuwa wanapita na mabilioni kununua ubunge sidhani kama watarudia kufanya huu mchezo(riz1)
Ni muda sasa wa watz kujaza wapinzani bungeni.
Rais kama JP akizingua anatinduliwa tu.
 
Najua anafahamu sana kwamba hivyo vigezo vya kitaifa na kimataifa anavyozungumzia yeye ni ambavyo vinaangaliaji ukuaji wa uchumi, pato la taifa na pato la kila mmoja... it's all about GDP na per capita GDP! Mpango anafahamu vizuri sana kwamba hivyo vigezo haviakisi maisha ya wananchi bali vinaakisi ukuaji wa uchumi wa kwenye vitabu! Hata hivyo, kwavile mwenye shibe hamjui mwenye njaa; na labda anahisi hili ni taifa la maboya, basi haoni taabu wala aibu kuongea uongo usio na maana yoyote ile.

Shame on y'all.
 
WAKATI idadi kubwa ya wananchi wakilalamikia ugumu wa maisha unaowakabili, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Arusha na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini.

Pamoja na hayo, Dk. Mpango alisema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa.

“Tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

“Mbali na Repoa, zipo taasisi nyingine ambazo zinaendelea na uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi.
“Nilishasema bungeni na narudia tena, kwamba kwa vigezo vyote vya kimataifa, tutaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwani hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limetoka hapa nchini hata mwezi haujapita, nao wamechambua mwenendo wa uchumi wetu na kusema uchumi wa nchi yetu ni mzuri.

“Maneno yanayosemwa mitaani, kwamba hali ya uchumi ni mbaya na fedha zimepungua katika mzunguko yanaenezwa na wapiga dili.

“Katika hili, nawatoa hofu wananchi, kwamba hali ya uchumi iko imara na hayo maneno yanayosemwa si ya kweli bali tufanye kazi kwa bidii,” alisema Dk. Mpango.

Alisema pia kwamba deni la taifa na mauzo ya ndani na nje yanakwenda vizuri ingawa ukame unaonyemelea nchi, unaweza ukasababisha upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa.

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, alizishauri benki na taasisi nyingine za fedha kuhakikisha zinawafikia Watanzania wengi kwa kuwashirikisha kutoa mchango wa kifedha.

Chanzo: Mtanzania
Ukimuona nyani na sizonje akasema yule sio nyani bali ni ngiri wote watasema "ngiriiiiiiiiiiii.........". Dr. Mpango hawezi kuongea kinyume na mkemiauchumi. Wahanga walinena "mtumikie kafiri upate ujira wako". Muda utaongea
 
Najua anafahamu sana kwamba hivyo vigezo vya kitaifa na kimataifa anavyozungumzia yeye ni ambavyo vinaangaliaji ukuaji wa uchumi, pato la taifa na pato la kila mmoja... it's all about GDP na per capita GDP! Mpango anafahamu vizuri sana kwamba hivyo vigezo haviakisi maisha ya wananchi bali vinaakisi ukuaji wa uchumi wa kwenye vitabu! Hata hivyo, kwavile mwenye shibe hamjui mwenye njaa; na labda anahisi hili ni taifa la maboya, basi haoni taabu wala aibu kuongea uongo usio na maana yoyote ile.

Shame on y'all.
lol, thats so lame! ... gosh.
 
Sijawahi ona mtu muongo kama huyu
Yeye kwa sababu analipiwa kila kitu kuanzia mavazi,chakula,usafiri,matibabu,hadi bia anatuletea ujinga huu.
Kutusomea uchumi wa nadharia wa REPOA, kwamba mambo mazuri wakati hali ni mbaya ni uhayawani wa hali ya juu
 
1480149018034.jpg
 
Back
Top Bottom