Dkt. Mpango: Maneno yanayosemwa mtaani, kwamba hali ya uchumi ni mbaya yanaenezwa na wapiga dili

comrade igwe

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Messages
7,329
Likes
3,819
Points
280
comrade igwe

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2015
7,329 3,819 280

WAKATI idadi kubwa ya wananchi wakilalamikia ugumu wa maisha unaowakabili, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Arusha na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini.

Pamoja na hayo, Dk. Mpango alisema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa.

“Tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

“Mbali na Repoa, zipo taasisi nyingine ambazo zinaendelea na uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi.
“Nilishasema bungeni na narudia tena, kwamba kwa vigezo vyote vya kimataifa, tutaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwani hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limetoka hapa nchini hata mwezi haujapita, nao wamechambua mwenendo wa uchumi wetu na kusema uchumi wa nchi yetu ni mzuri.

“Maneno yanayosemwa mitaani, kwamba hali ya uchumi ni mbaya na fedha zimepungua katika mzunguko yanaenezwa na wapiga dili.

“Katika hili, nawatoa hofu wananchi, kwamba hali ya uchumi iko imara na hayo maneno yanayosemwa si ya kweli bali tufanye kazi kwa bidii,” alisema Dk. Mpango.

Alisema pia kwamba deni la taifa na mauzo ya ndani na nje yanakwenda vizuri ingawa ukame unaonyemelea nchi, unaweza ukasababisha upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa.

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, alizishauri benki na taasisi nyingine za fedha kuhakikisha zinawafikia Watanzania wengi kwa kuwashirikisha kutoa mchango wa kifedha.

Chanzo: Mtanzania
 
W

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Messages
11,149
Likes
9,445
Points
280
W

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2016
11,149 9,445 280
WAKATI idadi kubwa ya wananchi wakilalamikia ugumu wa maisha unaowakabili, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri
Hili gazeti la Bashe lina vituko kweli....utafiti upi umefanya kugundua 'wananchi wengi'

“Tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

“Mbali na Repoa, zipo taasisi nyingine ambazo zinaendelea na uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi.
“Nilishasema bungeni na narudia tena, kwamba kwa vigezo vyote vya kimataifa, tutaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwani hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limetoka hapa nchini hata mwezi haujapita, nao wamechambua mwenendo wa uchumi wetu na kusema uchumi wa nchi yetu ni mzuri.
kwanini hujajikita na habari za utafiti wa Repoa, umekuja na ramli?
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
46,209
Likes
33,367
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
46,209 33,367 280
Jamaa yupo kwenye kiyoyozi ana shida gani?
Na hawa ndio washauri wa Rais.
Sasa mimacho itawatoka kwenye uchaguzi.
Wale jamaa wa ccm waliokuwa wanapita na mabilioni kununua ubunge sidhani kama watarudia kufanya huu mchezo(riz1)
Ni muda sasa wa watz kujaza wapinzani bungeni.
Rais kama JP akizingua anatinduliwa tu.
 
C

chige

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
8,375
Likes
16,068
Points
280
C

chige

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
8,375 16,068 280
Najua anafahamu sana kwamba hivyo vigezo vya kitaifa na kimataifa anavyozungumzia yeye ni ambavyo vinaangaliaji ukuaji wa uchumi, pato la taifa na pato la kila mmoja... it's all about GDP na per capita GDP! Mpango anafahamu vizuri sana kwamba hivyo vigezo haviakisi maisha ya wananchi bali vinaakisi ukuaji wa uchumi wa kwenye vitabu! Hata hivyo, kwavile mwenye shibe hamjui mwenye njaa; na labda anahisi hili ni taifa la maboya, basi haoni taabu wala aibu kuongea uongo usio na maana yoyote ile.

Shame on y'all.
 
mgoloko

mgoloko

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2016
Messages
4,609
Likes
3,790
Points
280
mgoloko

mgoloko

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2016
4,609 3,790 280

WAKATI idadi kubwa ya wananchi wakilalamikia ugumu wa maisha unaowakabili, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Arusha na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini.

Pamoja na hayo, Dk. Mpango alisema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa.

“Tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

“Mbali na Repoa, zipo taasisi nyingine ambazo zinaendelea na uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi.
“Nilishasema bungeni na narudia tena, kwamba kwa vigezo vyote vya kimataifa, tutaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwani hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limetoka hapa nchini hata mwezi haujapita, nao wamechambua mwenendo wa uchumi wetu na kusema uchumi wa nchi yetu ni mzuri.

“Maneno yanayosemwa mitaani, kwamba hali ya uchumi ni mbaya na fedha zimepungua katika mzunguko yanaenezwa na wapiga dili.

“Katika hili, nawatoa hofu wananchi, kwamba hali ya uchumi iko imara na hayo maneno yanayosemwa si ya kweli bali tufanye kazi kwa bidii,” alisema Dk. Mpango.

Alisema pia kwamba deni la taifa na mauzo ya ndani na nje yanakwenda vizuri ingawa ukame unaonyemelea nchi, unaweza ukasababisha upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa.

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, alizishauri benki na taasisi nyingine za fedha kuhakikisha zinawafikia Watanzania wengi kwa kuwashirikisha kutoa mchango wa kifedha.

Chanzo: Mtanzania
Ukimuona nyani na sizonje akasema yule sio nyani bali ni ngiri wote watasema "ngiriiiiiiiiiiii.........". Dr. Mpango hawezi kuongea kinyume na mkemiauchumi. Wahanga walinena "mtumikie kafiri upate ujira wako". Muda utaongea
 
Mfamaji

Mfamaji

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2007
Messages
6,612
Likes
685
Points
280
Mfamaji

Mfamaji

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2007
6,612 685 280
Huyu mpango sijui kasomea wapi. Mtu anaumwa njaa halafu mwingine anamwambia eti ameshiba. NI UPUUZI ULIOPITILIZA
 
Econometrician

Econometrician

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2013
Messages
9,571
Likes
10,001
Points
280
Econometrician

Econometrician

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2013
9,571 10,001 280
walisha jua Watanzania ni Ma.zu.zu hawaelewi chochote ndio maana wanajiongelea.kuanguka kwa soko la hisa kwenye nchi yyte ile duniani ni kielelezo kikubwa cha anguko la uchumi ktk Taifa! sasa sijui wanapingana na takwimu!
 
Kobello

Kobello

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Messages
6,553
Likes
1,606
Points
280
Kobello

Kobello

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2011
6,553 1,606 280
Najua anafahamu sana kwamba hivyo vigezo vya kitaifa na kimataifa anavyozungumzia yeye ni ambavyo vinaangaliaji ukuaji wa uchumi, pato la taifa na pato la kila mmoja... it's all about GDP na per capita GDP! Mpango anafahamu vizuri sana kwamba hivyo vigezo haviakisi maisha ya wananchi bali vinaakisi ukuaji wa uchumi wa kwenye vitabu! Hata hivyo, kwavile mwenye shibe hamjui mwenye njaa; na labda anahisi hili ni taifa la maboya, basi haoni taabu wala aibu kuongea uongo usio na maana yoyote ile.

Shame on y'all.
lol, thats so lame! ... gosh.
 
Himawari

Himawari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
2,312
Likes
850
Points
280
Himawari

Himawari

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
2,312 850 280
Hili somo la uchumi wa Tanzania kuimarika sijui kupanda, nahitaji malaika kunilewesha!

Hivi hawa wanaoitwa wapiga dili ni zao la uchumi pia au..?! Maana wanatajwa sana kuwa wao ndio wanaolalamikia ugumu wa maisha!!
 
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
3,500
Likes
2,232
Points
280
Age
38
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
3,500 2,232 280
Wao wanakusanya mapato wanagawana wana shida gani
 
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Messages
4,787
Likes
3,110
Points
280
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2011
4,787 3,110 280
Mi ni CCM Nyeupe iitwe nyeupe hali Ngumu kitaa hata frame zinapatikana kwa wingi mjini with less cost (rent).
Ngoja nikupe like leo maana taratibu utaanza kuelewa nini waungwana wanapigia kelele
 
M

m4cjb

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2012
Messages
6,903
Likes
359
Points
180
Age
34
M

m4cjb

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2012
6,903 359 180
hivi kumbe na mimi ni mpiga dili? lol muda utaongea
 
kivava

kivava

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Messages
5,797
Likes
4,573
Points
280
kivava

kivava

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2013
5,797 4,573 280
Sijawahi ona mtu muongo kama huyu
Yeye kwa sababu analipiwa kila kitu kuanzia mavazi,chakula,usafiri,matibabu,hadi bia anatuletea ujinga huu.
Kutusomea uchumi wa nadharia wa REPOA, kwamba mambo mazuri wakati hali ni mbaya ni uhayawani wa hali ya juu
 
M

Makusudically

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2014
Messages
2,098
Likes
1,067
Points
280
M

Makusudically

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2014
2,098 1,067 280
Mpango yuko sahihi kabisa, wapiga dili ndiyo wapiga propaganda za ugumu wa maisha. WATAISOMA NAMBA
 
Forum statistics

Threads 1,273,308
Members 490,351
Posts 30,477,653