Dkt. Mpango azindua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Rombo

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,005
1,583
Alisema miaka ya nyuma baadhi ya maeneo nchini yalikuwa na 'mchwa' katika miradi ya umma, lakini serikali imejizatiti kudhibiti matukio hayo.

Dk. Mpango alisema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Rombo na kuagiza ianze kazi Oktoba mosi, mwaka huu.

"Ninaamini dawa zitakazoletwa hapa Hospitali ya Wilaya ya Rombo, zitahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa, zisipelekwe katika maduka binafsi," alisema.

Aliziomba nchi rafiki, sekta binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi kuisaidia serikali kuboresha sekta hiyo.

Katika hatua nyingine, Dk. Mpango amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Profesa Makame Mbarawa, kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya Holili/Rotima/Tarakea, yenye urefu wa kilomita 53 ambayo inapita hospitalini hapo.

"Nimeona hospitali hii ipo mbali na makazi ya watu, Profesa Mbarawa popote alipo atangaze zabuni ya barabara hii, kadhalika Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) muitazame barabara hii ipitike mwaka mzima," alisisitiza.

Wakati wa ukamilishaji wa hospitali hiyo ukiendelea, aliitaka Hospitali ya Huruma ambayo ina hadhi ya hospitali ya wilaya, iendelee na hadhi hiyo ili kuhudumia wananchi kikamilifu.

Kadhalika, alimwagiza Mkuu wa Mkoa huo, Stephen Kagaigai kuhakikisha hati ya kiwanja ilipojengwa hospitali hiyo inatunzwa kuepuka wajanja wanaotaka kumega ardhi hiyo.

Kuhusu suala la ukame unaokumba baadhi ya mikoa nchini, Makamu wa Rais, aliomba viongozi wa madhehebu ya dini kuliombea taifa liwe na hali nzuri ya hewa.

"Nitoe Rai kwa viongozi wa dini, kuliombea taifa kupata hali nzuri ya hewa na mvua za kutosha ili tupate mazao na kuondokana na janga la upungufu wa chakula.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa TAMISEMI, David Silinde alisema kuwa

kwa sasa wanaendelea na mpango wa kuboresha huduma za afya ikiwamo uboreshaji wa miundombinu.

Alisema, mpango huo pia unaenda sambamba kuhakikisha vituo vya afya vilivyoko vinakuwa na uwezo wa kutoa huduma za upasuaji, kukamilisha maboma ya zahanati na kuanza ujenzi wa hospitali za halmashauri ambazo hazina hospitali.

Akitoa taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, alisema mkoa huo unakabiliwa na upungufu wa watumishi katika sekta ya afya kwa asilimia 51.6, uhitaji 8,598 na waliopo ni 4162.

Aidha, alisema ujenzi wa hospitali hiyo utakuwa hatua kubwa katika kuboresha sekta ya afya wilayani Rombo.

Awali, akitoa taarifa ya mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga, alisema hospitali hiyo imejengwa katika Kijiji cha Kiwanda, Kata ya Kirongo Samanga, uliogharimu Sh. bilioni 7.9.

Alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutanufaisha wananchi zaidi 317,000 ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya.

Chanzo: Nipashe
 
Watakwambia hawaoni kitu 😁😬..

Soma hiyoo 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220719-063135.png
    Screenshot_20220719-063135.png
    193.5 KB · Views: 16
Huyo Waziri Makame Mbawala yupo wapi naona hata makamu wa raisi nae anamtafuta, Asije kuwa amezira hiyo kazi ya uwaziri has ukitukanwa na mwanamke inauma sana
 
Alisema miaka ya nyuma baadhi ya maeneo nchini yalikuwa na 'mchwa' katika miradi ya umma, lakini serikali imejizatiti kudhibiti matukio hayo.

Dk. Mpango alisema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Rombo na kuagiza ianze kazi Oktoba mosi, mwaka huu.

"Ninaamini dawa zitakazoletwa hapa Hospitali ya Wilaya ya Rombo, zitahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa, zisipelekwe katika maduka binafsi," alisema.

Aliziomba nchi rafiki, sekta binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi kuisaidia serikali kuboresha sekta hiyo.

Katika hatua nyingine, Dk. Mpango amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Profesa Makame Mbarawa, kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya Holili/Rotima/Tarakea, yenye urefu wa kilomita 53 ambayo inapita hospitalini hapo.

"Nimeona hospitali hii ipo mbali na makazi ya watu, Profesa Mbarawa popote alipo atangaze zabuni ya barabara hii, kadhalika Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) muitazame barabara hii ipitike mwaka mzima," alisisitiza.

Wakati wa ukamilishaji wa hospitali hiyo ukiendelea, aliitaka Hospitali ya Huruma ambayo ina hadhi ya hospitali ya wilaya, iendelee na hadhi hiyo ili kuhudumia wananchi kikamilifu.

Kadhalika, alimwagiza Mkuu wa Mkoa huo, Stephen Kagaigai kuhakikisha hati ya kiwanja ilipojengwa hospitali hiyo inatunzwa kuepuka wajanja wanaotaka kumega ardhi hiyo.

Kuhusu suala la ukame unaokumba baadhi ya mikoa nchini, Makamu wa Rais, aliomba viongozi wa madhehebu ya dini kuliombea taifa liwe na hali nzuri ya hewa.

"Nitoe Rai kwa viongozi wa dini, kuliombea taifa kupata hali nzuri ya hewa na mvua za kutosha ili tupate mazao na kuondokana na janga la upungufu wa chakula.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa TAMISEMI, David Silinde alisema kuwa

kwa sasa wanaendelea na mpango wa kuboresha huduma za afya ikiwamo uboreshaji wa miundombinu.

Alisema, mpango huo pia unaenda sambamba kuhakikisha vituo vya afya vilivyoko vinakuwa na uwezo wa kutoa huduma za upasuaji, kukamilisha maboma ya zahanati na kuanza ujenzi wa hospitali za halmashauri ambazo hazina hospitali.

Akitoa taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, alisema mkoa huo unakabiliwa na upungufu wa watumishi katika sekta ya afya kwa asilimia 51.6, uhitaji 8,598 na waliopo ni 4162.

Aidha, alisema ujenzi wa hospitali hiyo utakuwa hatua kubwa katika kuboresha sekta ya afya wilayani Rombo.

Awali, akitoa taarifa ya mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga, alisema hospitali hiyo imejengwa katika Kijiji cha Kiwanda, Kata ya Kirongo Samanga, uliogharimu Sh. bilioni 7.9.

Alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutanufaisha wananchi zaidi 317,000 ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya.

Chanzo: Nipashe
Yaani suluhisho la ukame ni kuwaomba viongozi wa dini kuomba mvua????
 
Hivi Hawa Mawaziri wanafanya Nini kwenye nafasi zao endapo kazi yake unafanyia na makamu wa Rais ama Raisi mwenyewe??!

Ndio sababu hawaelewani huko wizarani!?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom