Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango ameiagiza wizara ya Viwanda na Biashara kufanya tathmini ya kweli kwenye Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido), limefanikiwaau kushindwa kwa kiasi gani katika kuleta tija katika kutekeleza wa malengo ya kuanzishwa kwake kwa miaka 48 iliyopita.
Akizungumza leo, Septemba 22, 2021 baada ya kufungua maonesho ya tatu ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido), kitaifa yaliyofanyika katika kiwanja cha Umoja, wilayani Kasulu mkoani Kigoma, amesema anasikitika kuona hadi panga na vifungashio wanaagiza kutoka nje ya nchi Shirika la SIDO wanakwama wapi.
Amesema katika tathmini hiyo watakwenda na mapendekezo ya mikakati mipya itakayopelekea Tanzania kuweza kukidhi mahitaji ya uchumi wa kati ya mashine ndogo,za kati,vipuri,bidhaa na huduma katika karne ya 21.
"Wiziri wa Viwanda na Biashara uhakikishe na isimamie utekelezaji wa zoezi hilo na unipatie mrejesho kupitia kwa Waziri Mkuu," amesema Makamu wa Rais Mpango.
Awali akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC), Samweli Gamakwa amesema baadhi ya shughuli za uwekezaji zimekuwa zikifanywa na wajasiriamali bila kuangalia athari za shughuli zao katika mazingira.
Amesema hivyo kuwataka wajasiriamali kufika kupata Elimu katika ofisi zao ili uwekezaji wanaoufanya usilete athari za kimazingira.