Dkt. Mpango amuagiza IGP kuwachukulia hatua Askari wanaoharibu taswira ya jeshi hilo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,097
Makamu wa Rais Dkt. Phili Mpango amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Camillus Wambura, kuangazia malalamiko yanayotolewa na #Wananchi kwa Jeshi la Polisi na kuwachukulia hatua askari wachache wanaoharibu taswira yake.

Dkt. Mpango amelitaka Jeshi hilo kutenda haki pasipo kuonea mtu yeyote na kwa yeyote anayekwenda kinyume na taratibu za nchi achukuliwe hatua kwa mujibu wa Sheria na sio vinginevyo.

IGP Wambura alimtembelea Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.
 
Haiitaji agizo IGP kuwa chukuliwa hatua askari yeyote asiye tii amri na taratibu za kijeshi. IGP una kazi sana jeshi lako kuanzia maafsa mpaka askari wamepinda sana. Kijeshi tunasema ni ' Co- cup'
 
"IGP Wambura alimtembelea Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania"

Hayo maandishi hapo juu ndipo ninaposhangaa.

Kujitambulisha maana yake nini!!??
Kwamba huyo anayetambulishwa hamjui!!??
Kwamba huyo anayetambulishwa hajui majukumu ya huyo anayejitambulisha!!??
Kwamba hakuna "job description" ya huyo anayejitambulisha!!???
Nina maswali zaidi ya mia moja ambayo yananiacha "akili wazi" kwa kujitambulisha kwa wateule.
 
Makamu wa Rais Dkt. Phili Mpango amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Camillus Wambura, kuangazia malalamiko yanayotolewa na #Wananchi kwa Jeshi la Polisi na kuwachukulia hatua askari wachache wanaoharibu taswira yake.

Dkt. Mpango amelitaka Jeshi hilo kutenda haki pasipo kuonea mtu yeyote na kwa yeyote anayekwenda kinyume na taratibu za nchi achukuliwe hatua kwa mujibu wa Sheria na sio vinginevyo.

IGP Wambura alimtembelea Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Hizi siasa tu hamna lolote hakuna wa kusafisha Polisi iliyojaa rushwa unyama na uonevu hata huyo Wambura ndio wale wale tusitegemee maajabu yoyote
 
Back
Top Bottom