DKT. Mollel: Rais Samia ametoa bilioni 148 kwa ajili ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

Lugha nyingine ngumu mno kuelezeka!
Mfuko wa bima unakusanya fedha nyingi mno mno, je hizi walizopewa zinatoka wapi? Ni hazina? Ni mfuko wa raisi?
 
Hii tabia ya kusema Rais fulani ametoa shs fulani ni mbaya sana. Inatengeneza kutukuza mtu kuona ndio mwenye hela. Kwanini msiseme serikali imetoa kiasi fulani? Tengenezeni taasisi imara na sio utukufu kwa watu.
Wanasema Rais ni taasisi.
 
"Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ametoa Shilingi Bilioni 148 kwa ajili ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenda kuwasaidia wananchi wasiokuwa na uwezo kuwa na uhakika wa bima. Tusiposimamia vizuri mifumo yeti na kuondoa ubadhirifu, mfuko huu utakufa" Dkt. Godwin Mollel

Rais ametoa au Serikali ndio imetoa..??

Ukiona kauli kama hizo ujue hzo hela zinakuwa zimetolewa kwa maamuzi binafsi ya Raisi,,, tofauti na hvo angesema Serikali imetoa.........

Hii nchi katiba inatakiwa ije haraka sana kuliko maji na umeme...

🚕Akawasha gari akatelezaa
 
Sema Serikali imetoa sh.....

Mbona mnampamba sana? Ana mfuko wa Rais nje ya kodi?

Mkijipendekeza sana mtafeli nyie wateule.R#

Sema Serikali imetoa sh.....

Mbona mnampamba sana? Ana mfuko wa Rais nje ya kodi?

Mkijipendekeza sana mtafeli nyie wateule.
Rais ana mamlaka na utashi wake angeweza kuamua kujenga terminal two Chato International Airdrome badala ya kulipia bima ya afya
 
Hii tabia ya kusema rais wetu mpendwa sijui shujaa etc amefanya nini inatia kinyaa sana. Na iliasisiwa majuzi tu wakati wa magufuli. Mollel ajue kwamba sio Samia ametoa hiyo pesa. Ni bajeti ya serikali inatekelezwa full stop.
Pia ajue matumizi ya serikali hayaidhinishwi na rais bali bunge.
 
Back
Top Bottom