Trubarg
JF-Expert Member
- Jan 8, 2020
- 4,256
- 6,893
Kwa waliokaribu na TV tune in TBC 1
======
Ndege ya kwanza ya watalii imewasili nchini ikiwa ni baada ya Rais John Magufuli kuruhusu kuendelea kwa shughuli za utalii nchini baada ya kupungua kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona Tanzania.
Tarehe 20, Mei 2020, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi aliahidi ya kuwa mwishoni mwa Mei ndege ya kwanza ingetua nchini.
Waziri Kigwangala
“Tuna matarajio makubwa kuwa sekta ya utalii na usafiri wa anga itafunguka vizuri kadiri tunavyoelekea”
“Hii ni ndege ya kwanza ya abiria ni ya Ethiopian Airlines, marafiki zetu.”
“Kwa kuanzia Ethiopian Airlines watatua Jumatatu, Alhamis na Jumamosi kwa ndege za abiria. Watatua hapa lakini pia Zanzibar. Kwa sasa wameshusha abiria na mizigo Zanzibar wanashusha na hapa Kilimanjaro, wanaenda Addis na nchi nyingine”
“Kwa siku tano za wiki tutakuwa na ndege zinazotua nchini, lakini zinazotuhusu zaidi watu wa utalii zitatua kwa siku tatu -- Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi -- ambazo purely ni ndege za abiria wote lakini kwa kiasi kikubwa tunatarajia itakuwa ni watalii”
“Dunia inajifunza namna ya kupambana na janga zito kama hili la mlipuko wa Covid 19 bila kufunga shughuli za kiuchumi na maisha ya watu”
Tumejipanga vizuri na tuna uhakika kutakuwa na usalama wa wageni na wahudumu. Tumefanya ziara ya kukagua mifumo na tumejiridhisha kwamba
Naibu Waziri wa Afya, Dr Godwin Mollel
“Ndani ya nchi maambukizi ya Corona kila siku yanapungu, hii ni kumaanisha kuwa kuna mabo yanafanyika”
“Tumehakikisha kuwa miongozo ya Shirika la Afya Duniani na Wizara ya Afya imefuatwa katika kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19”
Meneja Uwanja wa KIA
“Tupo tayari kuipokea kuutangazia dunia kuwa tupo tayari kupokea wageni.”
“Leo tumefurahi kuona tumepokea ndege ya kwanza”
“Kabla ya corona tulikuwa tunapokea abiria wengi sana. Mwaka jana tulikuwa na abiria 28,000 kwa mwezi na hadi kufikia kipindi cha Corona tulikuwa na wastani wa abiria 19,000”
“Tumejipanga vizuri kuwalinda wageni na wageni dhidi ya Covid 19”