#COVID19 Dkt. Mollel: Chanjo ya Corona ni salama, ndio maana Rais Samia baada ya kuchanja akaenda Lugalo kuendelea na majukumu yake

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Naibu Waziri wa afya Dkt. Mollel amesema chanjo ya Corona ni salama ndio maana Rais Samia mara tu baada ya kuchanjwa aliweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Mollel amesema Rais Samia alitoka Ikulu baada ya kuchanjwa na kwenda Lugalo Hospital ambako alifanya ukaguzi na kufungua mradi wa afya kisha akahutubia.

Chanzo: Channel Ten

1627636579200.png
 
Ili suala la chanjo mbona linawapa tabu sana viongozi wa juu , tumieni watu wa afya ambao wapo mpaka vijijini kuelimisha watu

Tz hakuna chanjo haijawai kuwekewa maneno, nakumbuka wakati inaanza chanjo ya pcv13, rota, maneno yalikua mengi , ila watoto wetu wanadungwa , na hazina shida,

Sasa KILA wakati mwapiga mapambio nyie mpaka mnashutua watu kwamba why viongozi wanashabikia chanjo hivi
 
Naibu Waziri wa afya Dr Mollel amesema chanjo ya Corona ni salama ndio maana Rais Samia mara tu baada ya kuchanjwa aliweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Mollel amesema Rais Samia alitoka Ikulu baada ya kuchanjwa na kwenda Lugalo hospital ambako alifanya ukaguzi na kufungua mradi wa afya kisha akahutubia.

Source: Channel ten
Dr mollel, hueleweki
 
Naibu Waziri wa afya Dr Mollel amesema chanjo ya Corona ni salama ndio maana Rais Samia mara tu baada ya kuchanjwa aliweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida...
Alie sign cheri chako cha udaktari anajuta, una uwezo mdogo sana wa kufikiri. Samia sio kipimo cha tiba, madhara ya tiba yoyote yanaweza tokea mapema au baadae.

Ungetoa takwimu za matokeo chanya kwa walio pata chanjo miezi kadhaa iliopita ungeeleweka. Leo hii wananchi wakihoji uhalali wa vyeti vyenu mnanuna.
 
...isijekuwa alijisogeza eneo hilo ambalo ni maalumu kwa viongozi kwa uchunguzi maalumuuu
 
Wakikaa kimya watawaacha wananchi wapate utulivu wa kuchambua na kufanya maamuzi sahihi kuhusu chanjo.

Hizi sarakasi zao zinazidi kuvuruga watu, hasa zikitolewa na watu tuliowaamini na kuwapa dhamana ya madaraka makubwa.

Inamaana hapo ndio kathibitisha usalama wa chanjo?

Chanjo sio lazima iwe na madhara lakini unavyoelezea nadharia yako ndio tatizo.

Ni sawa na mtu anasema kweli Mungu yupo, nimefaulu mtihani....nakubali Mungu yupo lakini kigezo kidogo na cha hovyo sana kinatumika kuthibitisha uwepo wake, hoja dhaifu.
 
Dr Mollel ameongea kama mimi ambae sio daktari

Chanjo inaweza kuwa salama au isiwe salama kweli. NA Rais kuendelea na kazi zake baada ya kupatiwa chanjo haithibitishi usalama wa Chanjo.

Kama anataka kuongelea Usalama wa Chanjo atueleze kwa muda mfupi baada ya chanjo Rais ameweza kufanya kazi zake na kwa muda mrefu .....aseme nini kinaweza kuwa kizuri pia
 
Ili swala la chanjo mbona linawapa tabu Sana viongozi wa juu , tumieni watu wa afya ambao wapo mpaka vijijini kuelimisha watu...
Na hao watu wa afya walioko vijijini hawajaongezewa mishaara mpaka leo. Wamenuna balaa. Alafu uje uwaambie mambo ya korona sijui kama wataelewa.
 
Mataga: Chanjo ya korona ni mbaya ndio Maana magufuli aliikataa.

Baada ya Mama Samia kuchanjwa...

Mataga: Chanjo ya korona haina shinda, ni safi kabisa haina madhara.

Mimi pamoja na wananchi wazalendo: Hao ni kasuku wa Lumumba wanacheza kulingana na biti ili wapate buku 7 zao.
 
Naibu Waziri wa afya Dr Mollel amesema chanjo ya Corona ni salama ndio maana Rais Samia mara tu baada ya kuchanjwa aliweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Mollel amesema Rais Samia alitoka Ikulu baada ya kuchanjwa na kwenda Lugalo hospital ambako alifanya ukaguzi na kufungua mradi wa afya kisha akahutubia.

Source: Channel ten
Kama na wewe ni Dr. basi alie saini cheti chako Cha udaktari akisoma hii post yako,hakianani anajuta Sana huko aliko.sijajua Dr. Molel aliemsainia cheti chake Kama yuko hai,Ila hata Kama Alisha R.i.p hakianani huko aliko ,marehemu anajuta kusain cheti Cha molel.
 
Alie sign cheri chako cha udaktari anajuta, una uwezo mdogo sana wa kufikiri. Samia sio kipimo cha tiba, madhara ya tiba yoyote yanaweza tokea mapema au baadae. Ungetoa takwimu za matokeo chanya kwa walio pata chanjo miezi kadhaa iliopita ungeeleweka. Leo hii wananchi wakihoji uhalali wa vyeti vyenu mnanuna.
Fact.
 
Serikali inabidi ijikite kuelimisha watu juu ya usalama wa chanjo baada ya mtu kuchanja na sio kuleta hoja ambazo hazina mashiko.

Watu wengi tayari wameshachanja mpaka sasa lakini bado sio hoja.
 
Dr Mollel ameongea kama mimi ambae sio daktari

Chanjo inaweza kuwa salama au isiwe salama kweli. NA Rais kuendelea na kazi zake baada ya kupatiwa chanjo haithibitishi usalama wa Chanjo.

Kama anataka kuongelea Usalama wa Chanjo atueleze kwa muda mfupi baada ya chanjo Rais ameweza kufanya kazi zake na kwa muda mrefu .....aseme nini kinaweza kuwa kizuri pia
Mimi Naona bora wangekaa kimya.
Wanavyotumia nguvu kubwa ndivyo wanavyozidi kuwapa watu wasiwasi.

Jana alikuwa channel ten anaongea yaani nadhani hadi koo lilimkauka, hadi niliokaa nao pembeni wakaanza kupata wasiwasi kwamba mbona anatumia nguvu kubwa mno kuaminisha watu na wakati walishasema chanjo ni hiari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mataga: Chanjo ya korona ni mbaya ndio Maana magufuli aliikataa.

Baada ya Mama Samia kuchanjwa...

Mataga: Chanjo ya korona haina shinda, ni safi kabisa haina madhara.

Mimi pamoja na wananchi wazalendo: Hao ni kasuku wa Lumumba wanacheza kulingana na biti ili wapate buku 7 zao.
Inaleta tafrani kwa wananchi.
Watu hawahawa walisimama na JPM,leo wamebadili gia angani.
Wanachanganya watu na inaonyesha jinsi gani wanawachezea wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom