Dkt. Mollel ataka wataalam wa Tehama kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji wa dawa

Wizara ya Afya Tanzania

Verified Member
Oct 1, 2020
33
125

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amewataka wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika hospitali kutengeneza mfumo wa ufutaliji wa dawa hospitalini ili kuwa na kanzidata ya matumizi sahihi ya dawa.

“Kila dawa inayokuja mtutengenezee mfumo ambao tunaona dawa kutoka taifa, unaiona inaingia mkoani, Hospitali ya Wilaya, vituo vya vyote na tuone ni aina gani ya dawa imeingia” Amesema Dkt. Mollel

Amesema mfumo huo utawasaidia kutambua mgawanyo wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kuwasaidia viongozi kuwa na taarifa sahihi wakati wanashughulikia malalamiko ya uhaba wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo kuwasaidia katika kufanya maamuzi.

“Mnafeli kwenye kufanya maamuzi na wakati mwingine tunaona hamjafanya maamuzi ya busara kumbe mmejifelisha kwa sababu mnashindwa kupata takwimu halisi za magonjwa, idadi ya wagonjwa na mahitaji ya dawa” Amefafanua Dkt. Mollel

Amesema kushindwa kwa wataalam hao kuwa na takwimu sahihi zinasababisha kuwa na mahitaji yasiyo na uhalisia upatikanaji wa dawa.
 

kunena

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
377
500
Nadhani mfumo wa GoTHIMIS ukiongezwa hiyo component unaweza kufanya vizuri, maana kwa sasa unafanya kwa level ya kituo husika tu.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,443
2,000
NAIBU waziri naomba awasiliane na waziri waziri wa Teknolojia Ndugulile kuna mwanachuo wa DIT katengeneza system ya uwajibikaji wa manesi wodi za watoto na taarifa anazo akipe kazi hicho chuo watengeneze hiyo system wauzie Wizara ya Afya.

DIT kazi kwenu

Pia kama wako waandika software binafsi ingineni kazini nadhani sio ngumu sana kuandika sababu ni kama tu stock control software ya bidhaa za godown tu sababu madawa ni stock tu ya kawaida.

Inginieni internet angalieni requirements kisha iandikeni kifupi inaitwa Drug Inventory Management Software FURSA HIYO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom