Dkt. Migiro ateuliwa na UN kama Mjumbe wa Bodi ya Ngazi ya Juu ya Ushauri kuhusu Usuluhishi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameteua jopo la wataalamu 18 watakaokuwa na kazi ya kuhakikisha wanatumia uzoefu wao kukabiliana na migogoro duniani kwa njia ya kidiplomasia, huku mwanadiplomasia wa Tanzania, Dk Asha- Rose Migiro akiwa miongoni mwa wateule hao.

Hatua ya kuteuliwa Dk Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UN kwenye jopo hilo imeelezwa na wataalamu wa masuala ya diplomasia kuwa ni uthibitisho mwingine wa namna Tanzania ilivyo mshiriki muhimu katika kusaka amani ya dunia.

Jopo hilo ambalo linafahamika kama ‘Bodi ya Ngazi ya Juu ya Ushauri kuhusu Usuluhishi’ limeundwa kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na uwakilishi wa kikanda, pia likizingatia historia ya wahusika katika masuala ya diplomasia na utatuaji wa migogoro.

Pamoja na Dk Migiro ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, wengine walioteuliwa ni aliyekuwa mke wa rais wa Msumbiji na baadaye akaolewa na Rais Nelson Mandela wa Afrika Kusini, Graca Machel, Rais mstaafu wa Nigeria, Olesegun Obasanjo, Rais wa zamani wa Chile, Michelle Bachallete na Rais mstaafu wa Finland, Tarja Halonen.

Pia, wamo wanadiplomasia, mawaziri wa zamani, watu waliowahi kuongoza taasisi za kimataifa na watu wengine mashuhuri. Jopo hilo pamoja na kazi nyingine litakuwa na jukumu la kumshauri Katibu Mkuu wa UN kuhusu njia zinazopaswa kuzuia migogoro na kushiriki kutatua mizozo katika maeneo yanayokumbwa na hali hiyo.

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya diplomasia wamesema kuteuliwa kwa watu kama Dk Migiro na Graca Machel kwenye jopo hilo kunaonyesha jinsi walivyoiva kidiplomasia na watatoa mchango mkubwa katika kuhakikisha amani inapatikana duniani.

“Mtu kama Dk Migiro ana uzoefu mkubwa wa mambo haya na kuteuliwa kwake kunadhihirisha namna Tanzania ilivyo mstari wa mbele katika kusaidia kupatikana kwa amani duniani,” amesema Innocent Shoo, Mhadhiri wa Chuo cha Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia (CFR).

Amesema Tanzania imekuwa ikishiriki katika utatuzi wa migogoro katika maeneo mbalimbali duniani, hivyo kuteuliwa kwake hakushangazi kwa vile kunaendelea kudhihirisha diplomasia ya Tanzania kwenye eneo hilo.

“Hivi sasa tunaweza kuona jinsi Rais wetu mstaafu Benjamin Mkapa anavyoendelea na upatanishi katika mzozo wa Burundi, wakati Rais Jakaya Kikwete akipatanisha nchini Libya na hata Dk Migiro amewahi kushiriki kikamilifu katika kusaka amani katika eneo la Nchi za Maziwa Makuu wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na hata alipokua UN kama Naibu Katibu Mkuu,” amesema.

Kuhusu Graca Machel amesema amekuwa mstari wa mbele katika kupigania usawa ambao mara nyingi unapokosekana huwa chanzo cha kuzuka kwa migogoro mingi duniani.

“Lakini pia alishiriki katika kusaka amani nchini Kenya wakati wa machafuko baada ya uchaguzi wa mwaka 2007,” amesema.

Mwananchi
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
11,896
2,000
Hongera zake Mama.....mwana diplomasia!! Wengine wakistaafu sijui wata fit wapi hata kujieleza mistari 2 hawawezi...."i wish I kudube.....diplomat"
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,268
2,000
Vipi JK hayumo au kutakuwa na uteuzi mwingine!
Akafanye nini?Dunia ya Leo hata huyo Gutierrez na wenzie hawajitambui. Akian Trump hawana muda tena wa mazungumzo na michakato ya kupoteza muda miaka nenda rudi hadi tatizo linapitwa na wakati.Kisha wanasema wamesolve tatizo.Muda huo watu wanakula hela za wavuja jasho duniani. Gutierrez ,blatter, na wengine ktk hizi taasisi zieny ekutegemea kura wanajua kuna watu ukiwaweka utapata wajinga wa africa na na wengine wa dunia ya 3 kwa ajili ya kura za uchaguzi ujao.
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,385

Sidhani kama sababu ni kwa UTANZANIA wake bali kwa uwezo wake.
 
UCD

JF-Expert Member
Aug 17, 2012
7,669
2,000
Akafanye nini?Dunia ya Leo hata huyo Gutierrez na wenzie hawajitambui. Akian Trump hawana muda tena wa mazungumzo na michakato ya kupoteza muda miaka nenda rudi hadi tatizo linapitwa na wakati.Kisha wanasema wamesolve tatizo.Muda huo watu wanakula hela za wavuja jasho duniani. Gutierrez ,blatter, na wengine ktk hizi taasisi zieny ekutegemea kura wanajua kuna watu ukiwaweka utapata wajinga wa africa na na wengine wa dunia ya 3 kwa ajili ya kura za uchaguzi ujao.
Ni haki yako na wewe kutoa maoni hata yakiwa pumba tupu!!
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,268
2,000
Ni haki yako na wewe kutoa maoni hata yakiwa pumba tupu!!
Km ilivyo haki yako kutafsiri utakavyo ili upate majibu utakayo. Africa hata uwaweke darasa moja na wazungu,bado siku ya mwisho matokeo yatakuwa tofauti tuu na wao watakuwa ktk njia potofu.
 
Android

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
964
1,000
Huyu mama ana zali tu au kismati, lakin uwezo wake ni mdogo sana.pasco mshana jr watu wenye ngekewa kwenye jicho la tatu huwa wana kitu gani? Kuna dawa ya ngekewa?
 
shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,899
2,000
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameteua jopo la wataalamu 18 watakaokuwa na kazi ya kuhakikisha wanatumia uzoefu wao kukabiliana na migogoro duniani kwa njia ya kidiplomasia, huku mwanadiplomasia wa Tanzania, Dk Asha- Rose Migiro akiwa miongoni mwa wateule hao.

Hatua ya kuteuliwa Dk Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UN kwenye jopo hilo imeelezwa na wataalamu wa masuala ya diplomasia kuwa ni uthibitisho mwingine wa namna Tanzania ilivyo mshiriki muhimu katika kusaka amani ya dunia.

Jopo hilo ambalo linafahamika kama ‘Bodi ya Ngazi ya Juu ya Ushauri kuhusu Usuluhishi’ limeundwa kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na uwakilishi wa kikanda, pia likizingatia historia ya wahusika katika masuala ya diplomasia na utatuaji wa migogoro.

Pamoja na Dk Migiro ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, wengine walioteuliwa ni aliyekuwa mke wa rais wa Msumbiji na baadaye akaolewa na Rais Nelson Mandela wa Afrika Kusini, Graca Machel, Rais mstaafu wa Nigeria, Olesegun Obasanjo, Rais wa zamani wa Chile, Michelle Bachallete na Rais mstaafu wa Finland, Tarja Halonen.

Pia, wamo wanadiplomasia, mawaziri wa zamani, watu waliowahi kuongoza taasisi za kimataifa na watu wengine mashuhuri. Jopo hilo pamoja na kazi nyingine litakuwa na jukumu la kumshauri Katibu Mkuu wa UN kuhusu njia zinazopaswa kuzuia migogoro na kushiriki kutatua mizozo katika maeneo yanayokumbwa na hali hiyo.

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya diplomasia wamesema kuteuliwa kwa watu kama Dk Migiro na Graca Machel kwenye jopo hilo kunaonyesha jinsi walivyoiva kidiplomasia na watatoa mchango mkubwa katika kuhakikisha amani inapatikana duniani.

“Mtu kama Dk Migiro ana uzoefu mkubwa wa mambo haya na kuteuliwa kwake kunadhihirisha namna Tanzania ilivyo mstari wa mbele katika kusaidia kupatikana kwa amani duniani,” amesema Innocent Shoo, Mhadhiri wa Chuo cha Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia (CFR).

Amesema Tanzania imekuwa ikishiriki katika utatuzi wa migogoro katika maeneo mbalimbali duniani, hivyo kuteuliwa kwake hakushangazi kwa vile kunaendelea kudhihirisha diplomasia ya Tanzania kwenye eneo hilo.

“Hivi sasa tunaweza kuona jinsi Rais wetu mstaafu Benjamin Mkapa anavyoendelea na upatanishi katika mzozo wa Burundi, wakati Rais Jakaya Kikwete akipatanisha nchini Libya na hata Dk Migiro amewahi kushiriki kikamilifu katika kusaka amani katika eneo la Nchi za Maziwa Makuu wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na hata alipokua UN kama Naibu Katibu Mkuu,” amesema.

Kuhusu Graca Machel amesema amekuwa mstari wa mbele katika kupigania usawa ambao mara nyingi unapokosekana huwa chanzo cha kuzuka kwa migogoro mingi duniani.

“Lakini pia alishiriki katika kusaka amani nchini Kenya wakati wa machafuko baada ya uchaguzi wa mwaka 2007,” amesema.

Mwananchi
Hii ni habari nzuri.
Na itaifanya Tanzania ionekane KICHANYA machoni pa Jumuia ya Mataifa.
Badala ya HABARI MBAYA MBAYA ambazo wengine wamekuwa wakijaribu sana nchi ionekane NEGATIVELY/ KIHASI machoni mwa jumuia ya kimataifa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom