Dkt. Mengi atunukiwa tuzo maalumu na Askofu! Aahidi kutoa Tsh. Bilioni 1 kusaidia ujenzi wa Sekondari mkoani Kilimanjaro

We kweli mwehu Kilimanjaro tupo vizuri tunasomesha tangu enzi za mkoloni tunajenga Madarasa ndio maana Kilimanjaro Ni mkoa wa kwanza tz kuwa na secondary nyingi
ndio maana Hakuna ofisi yoyote tz utamkosa mtu wa Kilimanjaro
Soma hapo chini ripoti ya mikoa na hali za kiuchumi za watu wake uone jinsi Kilimanjaro ilivyo safi
Usirudie kuandika upuuzi wako utaumbukaView attachment 1030712View attachment 1030713

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kukariri!hujamuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alipigwa stop asijenge hospitali ya moyo na watu fulani. Hata yule Dr Massawe aliyeanzisha Heart Institute alifanyiwa njama na kuwa frustrated hadi akafa kwa msongo wa mawazo.

Ilionekana atawakosesha watu fulani ulaji yaani wale waliokuwa wanafaidika na wagonjwa wa moyo kupelekwa India.

Lakini sasa natumaini anaweza akajenga kama bado nia ipo. Ndivyo Tz yetu ilivyo.
Jibu mujarabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiwanda cha smartphone inayokaa na charge week hakijaisha na cha wakorea cha magari Hahahahah mwambie alipe kwanza wafanyakaz wake mishahara kwa tuzo hizo
 
View attachment 1030018

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi ametunukiwa tuzo maalum na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Mhashamu Isaac Amani kutambua mchango wake katika kusaidia jamii.

Pia Dk. Mengi ameahidi kutoa Tsh. Bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu ya Shule ya Sekondari Jumuishi ya Mtakatifu Pamakio iliyoko Kijiji cha Kimashuku, Hai mkoani Kilimanjaro.

Shule hiyo ilizinduliwa jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Wakati wa uzinduzi huo, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Isaac Amani, alisema Kanisa Katoliki limemtunuku tuzo maalum ya Msamaria Mwema (Good Samaritarian Special Needs Awards) kutokana na kutambua mchango wake katika kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu nchini kufikia ndoto zao.

Pia alisema kanisa hilo limemtunuku tuzo maalum ya ‘Innovative Leadership Award in Special Needs In Education’ Rais John Magufuli kwa kutambua mchango wa serikali katika kutoa huduma bora na shirikishi kwa Watanzania wote.

Katika hotuba yake, Dk. Mengi alisema Waziri Mkuu amekuwa akishiriki kwa kiwango kikubwa katika mipango yake ya kusaidia watu wenye ulemavu na hivi karibuni alishiriki ufunguzi wa Reginald Mengi Disability Foundation na amekuwa akimpa mawazo ya kusaidia watu wenye ulemavu.
Hii shule ingejengwa Mtwara au Lindi,katavi,au Kigoma ingekuwa poa zaidi,KLM,Kagera,Mbeya,zipo nyingi,jengeni zingine huku kwetu uswazi jamani hili na sisi tujisikie kama tupo Bongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii shule ingejengwa Mtwara au Lindi,katavi,au Kigoma ingekuwa poa zaidi,KLM,Kagera,Mbeya,zipo nyingi,jengeni zingine huku kwetu uswazi jamani hili na sisi tujisikie kama tupo Bongo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kanisa la kule Kilimanjaro ndio limejenga je huko kwenu hamna makanisa au misikiti ijenge shule kama hizo hadi utake kanisa la Kilimanjaro lije lijenge huko?
 
Back
Top Bottom