Dkt. Mengi atunukiwa tuzo maalumu na Askofu! Aahidi kutoa Tsh. Bilioni 1 kusaidia ujenzi wa Sekondari mkoani Kilimanjaro

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
500
1550913806843.png


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi ametunukiwa tuzo maalum na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Mhashamu Isaac Amani kutambua mchango wake katika kusaidia jamii.

Pia Dk. Mengi ameahidi kutoa Tsh. Bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu ya Shule ya Sekondari Jumuishi ya Mtakatifu Pamakio iliyoko Kijiji cha Kimashuku, Hai mkoani Kilimanjaro.

Shule hiyo ilizinduliwa jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Wakati wa uzinduzi huo, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Isaac Amani, alisema Kanisa Katoliki limemtunuku tuzo maalum ya Msamaria Mwema (Good Samaritarian Special Needs Awards) kutokana na kutambua mchango wake katika kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu nchini kufikia ndoto zao.

Pia alisema kanisa hilo limemtunuku tuzo maalum ya ‘Innovative Leadership Award in Special Needs In Education’ Rais John Magufuli kwa kutambua mchango wa serikali katika kutoa huduma bora na shirikishi kwa Watanzania wote.

Katika hotuba yake, Dk. Mengi alisema Waziri Mkuu amekuwa akishiriki kwa kiwango kikubwa katika mipango yake ya kusaidia watu wenye ulemavu na hivi karibuni alishiriki ufunguzi wa Reginald Mengi Disability Foundation na amekuwa akimpa mawazo ya kusaidia watu wenye ulemavu.
 

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,770
2,000
Acha wewe ungejua shule nyingi za Kilimanjaro za bweni wamejaa watoto wa mikoa mingine kwa asilimia kubwa sio wa Kilimanjaro usingeandika hiki.Mimi shahidi.
Na kweli kama hapa mtaani kwetu wamekuja watoto toka Morogoro kuja kusomea Moshi. Kurudi kwao hawataki kubeba maji na kutafuta kuni porini

Kilimanjaro I love you much

Sent using Jamii Forums mobile app
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
24,872
2,000
Na kweli kama hapa mtaani kwetu wamekuja watoto toka Morogoro kuja kusomea Moshi. Kurudi kwao hawataki kubeba maji na kutafuta kuni porini

Kilimanjaro I love you much

Sent using Jamii Forums mobile app
Mazingira ya kusoma Kilimanjaro shule za Bweni yako vizuri mno kuanzia mazingira,hali ya hewa , discipline kwa wote kuanzia wanafunzi, walimu na wamiliki wa shule ziko vizuri na zimebalance.Huwezi ona mapungufu.
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
17,439
2,000
Mtu kwao kwanza,kila mtu ajenge kwao bana.

Hongera mzee wa bao la dakika za majeruhi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom