Dkt. Mashinji kuchangiwa faini na chama (CCM)

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,397
Wakati kampeni ya kuchangisha pesa za kuwalipia faini Viongozi wa CHADEMA ikiendelea, upande wa CCM Humphrey Polepole ameandika yafuatayo kuhusu faini ya Vicent Mashinji ambae ni Mwanachama mpya wa CCM akihamia kutoka CHADEMA.

“Asante CCM Mkoa wa DSM, Mwenyekiti na Kamati ya Siasa kwa kujitoa kwenu kwa haraka ili kesho tukamnusuru Mwanachama wa CCM Vicent Mashinji.

Mtakumbuka kuongoka kwa Mashinji kumetupa picha nzuri ya wasiotutakia mema na mipango yao mingi yenye nia ovu #tunasimamanaMashinji”
FB_IMG_1583871521041.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu zamani tunaaminishwa kuwa Mbowe ni mtoto wa kishua aliyerithi utajiri wa kutisha. Tambo zake za kuzalisha wabunge wa viti maalum ni sababu ya kiburi cha pesa..! Lakini leo cha ajabu kwenye hukumu ya kumuuwa Akwilina, Freeman Mbowe amekosa million 70 ya kulipa faini hadi amepelekwa kulala Segerea, huku nyuma akiacha visebengo wa Sacco's yake wakihamasisha wananchi watoe hela zao kumchangia atoke!!!

Kweli Mbowe ni wa kuchangia ? Utajiri wake umeenda wapi?? Kweli wanachama hawako tayari kuchangia ujenzi wa makao makuu ya chama ila wako tayari kumchangia billionea Mbowe?

Huu utakuwa ni mwendelezo wa usanii wa DJ wa kubadili gia angani na kujifanya masikini ili apige hela za wasiojielewa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila ile M ngapi wanayochangishana wale wahuni wameunganisha na ya Masinji sijui wataifanyaje
 
Wamebaki kuwaiga cdm kila wafanyacho. Usishangae wanawake wa ccm nao wakakutana mlimani city ili kujibu shambulizi la wanawake wa cdm juzi. Kweli ukizeeka unabaki kuiga tu.
Asante dada

God save us
 
Tamko la Polepole kuhusu fine ya Dr Mashinji ni udhihirisho wa wazi kuwa kesi hii ya Viongozi wa Chadema, CCM ilikuwa na nia ovu na kwamba wapate maumivu wakiwa hawana Kosa. Kutoa fedha kumlipia MTU aliyekuwa amehukumiwa huku ukisema kwa wengine kuwa hukumu hiyo ni stahili yao hata mtoto atajua hukumu imebumbwa na mia yako imejulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Etwege,
Hukumu imetoka benki zishafungwa, hiyo cash 350M anapata wapi? Na by the way kuchangiwa ni hiyari sio lazima
 
Back
Top Bottom