Dkt. Mashinji: Huwezi ukawatofautisha Serikali, Mahakama na Bunge. Hata Mbinguni kuna Baba, Mwana na roho lakini maamuzi ni yaleyale

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na baadae kuhamia CCM, Dkt. Mashinji amesema Tanzania ni nchi changa na haiitaji kuwa na mabadiliko ya haraka ghafla kwa sababu kila mabadiliko yana athari.

Amesema yakifanyika mabadiliko na yakaja na athari, bado Tanzania halijawa Taifa linaloweza kujitanua kuhimili vishindo vya mabadiliko akitolea mfano mataifa yaliyofanikiwa kufanya mabadiliko kama Zambia na Malawi na kuyumba.

"Wameyumba sana, mpaka Zambia sasa hivi kuna watu wanaisema mtaani imekuwa kama imeuzwa kwa wachina, sasa sielewi kama ni kweli kwa sababu hivi karibuni sijaenda Zambia lakini ni kwa sababu ya haraka ya mabadiliko" Alisema Mashinji

UTAYARI VYAMA VYA SIASA
MASHINJI:
Chama cha mapinduzi kimekuwepo siku nyingi kikifanya kazi pamoja na dola, chama ndio kinaongoza serikali na sehemu yake ni dola. Huku nje tunaweza kukaa na kudanganyana wawe huru!

Hakuna kitu ambacho kinatofautisha hivi vitu, huwezi ukawatofautisha executive, mahakama na Bunge. Ni mawazo tu ya kufikirika hata kule Mbinguni kuna baba, mwana na roho lakini maamuzi ni yaleyale kwa sababu hawa wote lengo lao ni kufikia kitu kimoja

CHAMA KUMTEUA MGOMBEA URAIS AMBAE HAKUWEPO
MASHINJI:
Mfano uchaguzi ulioisha ambao umeisha na tunasonga mbele na maisha yetu, chama kinakuja na mgombea ambae hakuwepo kwa miaka mitatu. Hakujua shida za watu ni nini zaidi ya kujua kwenye mitandao, mimi naweza kuandika kwenye mtandao huo huo, naweza kusema tu nilikuwa Morogoro wakati niko hapa.

Amekuja hapa, chama makini kilitakiwa kwanza kijitafakari kwamba kweli umekuja, wewe ni maarufu, umefanya kazi nzuri lakini tunachokwenda kuangalia mbele ni kuweka mkuu wa nchi, mtu ambae ana mamlaka ya kusaini hati mtu akanyongwa, kutangaza vita. Juzijuzi hapa tulipigiwa kelele na Malawi kuhusiana na mpaka wa ziwa, tulikuwa na Rais Jakaya Kikwete, mliona utulivu wake, hakupika makelele, tumelimaliza salama.

Umeingia unatangaza upanga kwa upanga, nani atakupigia kura? Ni ngumu. Watanzania unajua ni wajanja, atakusikiliza vizuri wakishakuona unachokisema sio wanachokihitaji kwa wakati huo hawawezi

MASWALI NA MAJIBU
MWANDISHI:
Wewe umekuwepo kwenye ofisi kubwa, ulikuwa na nafasi ya kubadilisha mitazamo hii, ulifanya nini?

MASHINJI: Kulikua na hali ya tamaa kwa sababu ukishatengeneza mfumo, mfumo wa maamuzi ambao unatoka chini kuja juu maana yake unatengeneza Taasisi na mara nyingi taasisi hauamua kulingana na mahitaji ya wakati ule na ikija kufanya maamuzi huwa haiangalii umaarufu wa mtu.

Huwa inaangalia nani atatuvusha wakati huu, ukiangalia kwa mfano CCM ni taasisi. Wakati hayati Mkapa anapewa Urais sidhani kama kuna mtu alikuwa anazunguka mtaani anawaza Mkapa atakuwa Rais, kulikuwa na majina ambayo watu walikuwa wanayawaza lakini kwa kuwa ni Taasisi wakayachuja, wakasema anaetuvusha sasa ni huyu na kwa sababu ni kwenye taasisi watu wanaelewana.

Hivyohivyo Kikwete, vivyo hivyo huyu Rais tulienae sasa hivi, mheshimiwa Magufuli ameenda mle na watu maarufu tu, wanajulikana lakini kwa sababu ile ni taasisi na ina ajenda ilijua kabisa kwa ajenda na mfumo tulionao, mtu pekee ambae atatuvusha hapa ni John Magufuli.

Hakuna biashara yeyote utaifanya bila kujua wateja wako ni kina nani, kwa mfani biashara kubwa ya chama cha siasa ni kushinda uchaguzi na uchaguzi utaushindaje? Uchaguzi unaushinda kwenye kituo cha kupigia kura, huushindi uchaguzi kwa kuandamana barabarani wala kwenda kwenye mitandao ya kijamii, kule hamna uchaguzi sanasana utaenda kukera watu na kujinesha wewe ni mtu wa namna gani.

Kushinda uchaguzi unahitaji mambo manne, wagombea, ajenda na tulifanikiwa kupewa ajenda na wapinzani wetu kwamba ni kupinga kila kitu na tulishindwa kuiondoa na mpaka leo wananchi wanajua ajenda yetu ni kupinga kila kitu.
 
Huyu nae ni bora akae kimya tu. Katika watu waliofeli mapema ni huyu blaza.

Sijui udokta wake ni wa nini huyu jamaa?

Anaibuka sasa kipindi cha uteuzi anawaza anaweza bahatisha hata mkaguzi wa waganga wa kienyeji wilaya.
 
Pamoja na Kwamba alikuwa liability wakati akiwa CHADEMA na alipoenda SieSiem aliendelea kuwa liability kama kawa, Kwa Maneno mengine He did not add value kwa chama Pendwa. Msomi huyu wa Phd. ameona apige mayowe ili Kipindi hiki cha wapakwa mafuta ( wateule/wateuliwa) asije kusaulika.

Wasomi Wa Bongo Ma Phd plus Maprof, Wameamua Kuziacha taaluma zao na kwenda kwenye politics, Kwa lugha rahisi Matumbo yao yamekuwa na ushawishi mkubwa kuliko bongo zao. Bro, PhD Zingine zimespecialize Nyuki so wanazilazimishia Kwenye Political science...
 
Kwa hiyo huyu jamaa anataka atuaminishe kwamba huu mfumo wa sasa wa kutekana nyara, kukimbizana kunyanganyana form za uteuzi njiani, kupeana kesi za kukomoana kama visasi kisiasa, kuuana, kupotea, kupigwa kupeana vilema vya maisha, kujipendekeza kwa wenye mamlaka, Taasisi za umma nazo kujipendekeza kwa serikali - huu ndiyo unatufaa na tuendelee nao kwa sasa kwa tafsiri ya Mashinji.
 
Mimi nafikia kutoamini mtu yeyote hata namba moja simuamini . Huyu Dr Mashinji alivyokuwa CHADEMA alinyanyaswa kupigwa na kubambikiwa vyesi . Yaani anabariki upuuzi wa wana siasa kuwaamuru mahakimu kwenda kinyume na sheria ?!.
 
miaka 50 ya Uhuru hata kuchaguana wenyewe kwa wenyewe kwa ustarabu hamuwezi !! hadi wengine wawe vilema, wengine wafe, wengine wafungwe... yaani huu ni ustaarabu wa karne ya 13, aibu.

Huyu DR. hana lolote la maana.
Sasa miaka50 ya uhuru unataka tulingane na wale wa miaka 250 ya uhuru...? Tena wale waliotuibia na wanalazimisha kuendelea kutuibia?
Tutafika walipo safari ni hatua
 
Pamoja na Kwamba alikuwa liability wakati akiwa CHADEMA na alipoenda SieSiem aliendelea kuwa liability, Kwa Maneno mengine He did not add value kwa wale TAL anawaita MaCCM. Msomi huyu wa Phd. ameona apige mayowe ili Kipindi hiki cha Mavuno wasije kusaulika. Wasomi Wa Bongo Ma Phd plus Maprof, Wameamua Kuziacha taaluma zao na kwenda kwenye politics, Kwa lugha rahisi Matumbo yao yamekuwa na ushawishi mkubwa kuliko bongo zao. bro. PhD zimespecialize Nyuki so wanazilazimishia Kwenye Political science...
Serikali ya awamu ya tano imejenga Zahanati na Vituo vya afya vingi sana; wataamu kama huyo arudishwe kwenye eneo lake la utabibu
 
Back
Top Bottom