Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli wa CCM, kuzuia mikutano ya siasa miaka 5 itamgharimu sana

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Viona mbali tulisema kwamba mzee baba kuwabana wapinzani wasifanye mikutano ni kuzuia waseme ya moyoni ili upate kujirekebisha. Ilikua ni wakati sahihi kuwaacha wazunguke kisha utathmini siasa zao majukwaani kisha uone madhaifu yao. Sasa umewaambia hakuna mikutano ya hadhara wajifungie kwenye kumbi wafanye mikutano ya ndani ambayo nayo ilikua ikipigwa marufuku.Hapa ungejua inakubalika kwa kiasi gani.

Sasa Baba yangu wapinzani wako umewawekea imewazuia kufanya mikutano, wewe unafanya ziara unazunguka nchi nzima huku wasaidizi wako wakuu wa wilaya na mikoa wakiwatia ndani masaa 48 wapinzani wako, kikweli hukupata muda wa kujipima na wa kujifunza baba, walibakia wale wanaokusudia tu kwa vile uliwapa vyeo.

Sasa CCM mmeingia kwenye kampeni mkidhani mmeshafanya kazi kubwa ya kukijenga chama na nchi kumbe watu wako kimya wanawaangalia tu. Matokeo yake sasa mnafanya siasa huku mnatekeleza ahadi ambazo mlitakuwa msifanye kipindi chote za miaka 5, huku siyo kuwadanganyia wapiga kura ni nini?
Kura hatuwapi kwa sababu ni waongo hamsemi ukweli mnatudanganya.
 
Sasa hivi wanatafutana Polepole anaingilia mlango wa nyuma Bashiru anatokea wa mbele...haha.
 
ccm walifikiri kuwanyanyasa viongozi wa upinzani hasa CDM, kuwanunua wale 'makaka poa' a.k.a. machangu basi ndio imetosha kuua wapinzani! Tuliwaambia wazi kuwa upinzani unazidi kukua na kustawi na huo ndio ukweli!
 
ccm walifikiri kuwanyanyasa viongozi wa upinzani hasa CDM, kuwanunua wale 'makaka poa' a.k.a. machangu basi ndio imetosha kuua wapinzani! Tuliwaambia wazi kuwa upinzani unazidi kukua na kustawi na huo ndio ukweli!
Hata kwa maombi,magufuli hatoboi.,nakwa bahati mbaya ccm wote ni wanafiki kwake.
 
Angewaruhusu wapinzani kufanya siasa kama kawaida angepata muda wa miaka 5 kujibu au kushughulikia hoja zao kwa wakati. Sasa hivi zinaibuka hoja ambazo zilikuwepo miaka yote mitano lakini alijinyima mwenyewe fursa ya kuzisikia.
 
Back
Top Bottom