Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Vitambulisho vya Machinga sio lazima, acheni uongo

Ivi vitambulisho Kuna wafanyakazi za ofisi za umma walilazimishwa kuchukua na wengine kukatwa kwenye mishara yao , hapo mwaka jana lakini .
 
Leo anakana kila alichokiamuru
Kweli mwanakwetu kashikwa pasipozoeleka kushikwa!
Huyu mzee Hana haya, juzi juzi bi mkubwa kanipigia simu mtendaji wa Kijiji kaja na sungusungu kumkamata kwamba Hana kitambulisho cha magufuri. Nikamuuliza kwani unafanya bihashara gani? Akajibu jioni watu kijijin wanakusanyika kwangu kuangalia taarifa ya habari na mpira, kwa vile na yeye ni ccm nikamwambia mliyataka wenyewe. Bahati nzuri mtoto wake wa kike akamtumia iyo elfu 20, lakini Mimi nilitaka wamsumbue kwanza maana hawa wazazi wetu wanazingua sanaaaaaa!
Mkuu umenichekesha Sana na pia umenunikumbusha mbali Sana Bibi mkubwa wangu ni katibu mwenezi wa CCM kata ko ni mwana kada Sasa Kama unataka msielewane ongea vibaya Hawa nyoka wa kijani Sasa siku moja ikatokea skata moja hivi la mashamba wananyang'anya Bibi ambae pia ni mama yake sisi hatuishi huko tupo mikoa mingne na Bibi anaishi sehem nyingne na Mama sehem nyingne Sasa bi mkubwa akatupigia simu Mimi na bro akatuelezea sakata lilivyo Sasa bro yeye ni CDM ni sawa na Mimi tukamwambia Mama tatizo ni hao nyoka wenu wa kijani Mama akaanza kupanic tukasema ngoja Kwanza wamsumbue baadae atajua Sasa mzee yeye ni mtumish wa uuma inajikuta hachangii chochote ila na yeye ni mwana kada ila hajioneshi ko mzee akamsaidia
 
Mleta mada ndio anajua hilo leo,

Chadema wanachelewa sana kuelewa mambo,

Jambo linafanyika awamu ya nne wanakuja lielewa awamu wa tano,

Hata anayoyafanya sasa Magufuli watakuja muelewa awamu ya sita, mifano ipo mingi ni jambo la kuwavumilia tu hawa wapinzani tulionao kwani wanachelewa kuelewa mambo.
Ajabu wewe hapa peke yako ndo unamwelewa dikteta katika comments/replies 400, kwa hiyo tuseme katika watu 400, Magu ana kura yake 1, hujishangai?
 
Jana nimesikia mwanancji kuingiza fedha za kigeni nchini ruksa!
Bora tupunguze vipindi vya kufanya uchaguzi iwe kila baada ya miaka miwili ili mateso yasidumu kwa muda mrefu.
 
Nilienda ofisi za manispaa fulani, mkuu wa mkoa amekuja na wapambe wake wakiwemo mapolisi wanawatafuta maafisa biashara wamefunga ofisi wamekimbia, nikarudi mjini nikawakuta nikawambia mkuu anawatafuta wakasema hatuendi hadi aondoke, wakaenda kukopa
Pesa kwa mfanyabiashara fulani mwenye biashara kubwa ya Mpesa ili wakamkabidhi mkuu pesa halafu wakiendelea kuuza vutambulisho ndipo wakalipe deni kwa yule mfanyabiashara. Nikasema kweli kazi za serikali ni zaidi ya utumwa.
 
Ahaa! Lissu amekaba pabaya aisee! Kama vitambulisho hivyo sio lazima, kwanini wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi waliambiwa atakayeshindwa kuvimaliza ajuwe ameshindwa kazi? Tena ni amri hiyo ndio iliyopelekea baadhi wakuu wa mikoa kama yule wa Iringa kuanza kutaja kabisa makundi ya wafanyabiashara ambao lazima wawe navyo wakiwemo madereva wa bajaji ilihali wamiliki wao wameshalipia kodi TRA! Sehemu nyingine za vijijini watendaji walipita fremu moja ya duka hadi nyingine na kuamrisha hata mafundi viatu na washona ndala wanaolipwa TSHs 200 (miam bili) kwamba ni lazima walipe TSH 20,000 kuvinunuwa na kwamba ndio kibali cha shughuli yoyote kiuchumi! Sasa leo tunaambiwa tena haikuwa lazima!
 
Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli amesema, watu wanazusha kwamba Machinga wanalazimishwa kuwa na vitambulisho, sio kweli. Vitambulisho sio lazima.

''Vitambulisho havilazimishwi ni lazima itolewe elimu kwa wanaoshiriki kwenye vitambulisho ili wakafanye bishara mahali popote, tunataoa vitambulisho ili wanananchi hawa wenye biashara ndogondogo wasisumbuliwe''. Dkt John Magufuli, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Aidha amewataka wasaidizi wake wakiwamo wakuu wa wilaya kuendelea kuzingatia maelekezo yake ni wafanyabiashara wa aina gani wanaohitajika kuwa na vitambulisho vya machinga.

Vitambulisho hivyo humwezesha mjasiriamali kufanya baishara bila kutozwa kodi na halmashauri kwa kipindi cha mwaka mzima jambo ambalo hutajwa kuwa linalenga kuwainua wafanyabiashara wa mitaji midogo.

''Tulianzisha vitambulisho hivi kwaajili ya kuwalinda wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya kuona wanasumbuliwa na halmashauri, ukiwa na kitambulisho chako utafanya biashara mahali popote Tanzania, vitambulisho haviwezi vikatafutwa kwa bunduki, vitambulisho mtu anakata mwenyewe ni Sh 20000'' Dkt John Magufuli, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
Mh hivi vitambulisho vijijini ilifikia hatua hata mtu amebeba debe lake la mahindi kwenda kuuza anaulizwa kitambulisho.
 
Mkuu hayo maneno twaweza kuyapata katika clip ya video?
Hawa mbogamboga hawakawii kukanusha jambo hadi watwangwe rungu la kuwatoa damu kama kenge

Huu hapa Kaka mkubwa.

IMG-20200922-WA0006.jpg
h
 
Mh hivi vitambulisho vijijini ilifikia hatua hata mtu amebeba debe lake la mahindi kwenda kuuza anaulizwa kitambulisho.
Mimi walinifuata home wakaniambia una kuku zaidi ya 10 wewe ni mjasiriamali lazima uwe nacho. Nilikaza hadi mwisho
 
Vitambulisho ilikuwa ni shs 20,000/=.
Ma-RC na Ma -DC walipewa malengo ya kugawa kila mkoa na ndipo ikawa ni lazima wamachinga wote wawe navyo!
sasa hapo uongo uko wapi!
 
Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli amesema, watu wanazusha kwamba Machinga wanalazimishwa kuwa na vitambulisho, sio kweli. Vitambulisho sio lazima.

''Vitambulisho havilazimishwi ni lazima itolewe elimu kwa wanaoshiriki kwenye vitambulisho ili wakafanye bishara mahali popote, tunataoa vitambulisho ili wanananchi hawa wenye biashara ndogondogo wasisumbuliwe''. Dkt John Magufuli, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Aidha amewataka wasaidizi wake wakiwamo wakuu wa wilaya kuendelea kuzingatia maelekezo yake ni wafanyabiashara wa aina gani wanaohitajika kuwa na vitambulisho vya machinga.

Vitambulisho hivyo humwezesha mjasiriamali kufanya baishara bila kutozwa kodi na halmashauri kwa kipindi cha mwaka mzima jambo ambalo hutajwa kuwa linalenga kuwainua wafanyabiashara wa mitaji midogo.

''Tulianzisha vitambulisho hivi kwaajili ya kuwalinda wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya kuona wanasumbuliwa na halmashauri, ukiwa na kitambulisho chako utafanya biashara mahali popote Tanzania, vitambulisho haviwezi vikatafutwa kwa bunduki, vitambulisho mtu anakata mwenyewe ni Sh 20000'' Dkt John Magufuli, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
Wakuu wa wilaya na mikoa ufanisi wao unapimwa kwa mauzo ya hivyo vitambulisho pia.
Sijaona kipenger
le kuhusu hizo hela kwenye AG Report tangu vianzishwe au viko kwenye kasima ya Rais isiyokaguliwa????????
 
Back
Top Bottom