Dkt. Magufuli tafadhali vumilia, mwaka huu ni zamu yako. Lowassa alivumilia ingawa aliumia

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mwaka 2015, aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CHADEMA Edward Lowassa aliteseka sana. Alisemwa vibaya, alikejeliwa, alidhihakiwa, 'alitukanwa' alidhalilishwa na kutwezwa vya kutosha na kutisha. Lowassa alikosa ushawishi katika jukwaa la kampeni. Alikosa maneno ya kuongea. Aliishia kupata kigugumizi na kutoa salamu ya CHADEMA tu. Watu walijaa kwenye mikutano yake lakini hakuwa na cha kuwaambia kilichowavutia. Ulikuwa mwaka wake!

Mwaka huu, CHADEMA wana mgombea (Tundu Lissu) anayejua kusema, kusimanga, kunanga, kujenga hoja, kukera, kutangaza sera, kushawishi na kutupa vijembe. Mwaka huu makombora yanaelekezwa kwa Dkt. Magufuli, mgombea wa CCM. Yanaelekezwa kwake kwakuwa kwa miaka yote mitano ya awamu yake, ni yeye tu ndiye aliyekuwa akitajwa kwenye kila jambo linalohusu Serikali. Sifa zote alipewa yeye. Sasa apokee na kukosolewa yeye mwenyewe.

Mwaka huu, kwa nilivyomfuatilia, Dkt. Magufuli ameishiwa cha kuzungumza. Ameishiwa hoja. Hana jipya kwenye kampeni zake. Sasa imebaki 'kukopi' na 'kupesti' kutoka kwa Lissu. Mfano, jana tu ameahidi Bima ya Afya kwa kila mtanzania. Ni ahadi na sera ya Lissu tangu mwanzo. Nani kampa Dkt. Magufuli sera hii ya kuiga? Nasema, Dkt. Magufuli aseme mambo mapya; si abaki na yale yale na kuyasema vilevile.

Aseme alichoahidi mwaka 2015; alichofanikiwa na alichoshindwa. Halafu, aseme atawezaje kutimiza kile alichoshindwa. Wakati huohuo, avumilie 'madongo' ya mpnzani wake uchaguzini Lissu na kujibu kwa kutulia. Ajibu kwa kueleweka. Ajibu kwa hoja za haja. Mwaka huu ni mwaka wake, ni zamu yake katika kukosa cha kushawishi ingawa umati wa wananchi 'hukusanywa' na 'kuandaliwa' kutoa tafsiri ya kukubalika kwake.

Abadili santuri. Hakuna kipindi redioni au runingani kinachopiga wimbo mmoja tu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Shinyanga Mjini)
 
Waliomshauri aongee peke yake kwa miaka mitano hawakufikiri vizuri, haya ndio madhara sasa...alishaongea akamaliza, hoja zingine angeishazijibu kitambo.

Wenzie ndio kwanza wanaanza, hana kipya anaishia kujibu mashambulizi tu!
Mkuu si unakumbuka alisema yeye ni Jiwe hashauriki? Na mkijaribu tu ndiyo mnaharibu. Wazee wastaafu walipojaribu waliishia kuambiwa Mnawashwawashwa.
 
Mzee kazi anayo mwaka huu, spana anazopigwa zinamtoa mchezoni kabisa
Hzo spana za kawaida Sana na haziwez athiri kishindo cha ushindi cha mweshimiwa , anamsaidia Tu kufanya marekebisho fulan fulan Kwa miaka mingine mitano lakini to knock him out , sio kazi ya kukamilishwa na sku 44 za kampeni zilizobaki
 
Mwaka huu, CHADEMA wana mgombea (Tundu Lissu) anayejua kusema, kusimanga, kunanga, kujenga hoja, kukera, kutangaza sera, kushawishi na kutupa vijembe. Mwaka huu makombora yanaelekezwa kwa Dkt. Magufuli, mgombea wa CCM. Yanaelekezwa kwake kwakuwa kwa miaka yote mitano ya awamu yake, ni yeye tu ndiye aliyekuwa akitajwa kwenye kila jambo linalohusu Serikali. Sifa zote alipewa yeye. Sasa apokee na kukosolewa yeye mwenyewe.
Nyuzi kama hii unasoma huku unakunywa supu matata hapa Diamond Hotel mjini Kati Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom