Dkt. Magufuli na Tundu Lissu wawatakia maisha ya kheri wazee leo ikiwa Siku ya wazee duniani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,559
Mgombea Urais wa JMT kupitia CCM Dkt. Magufuli amewatakia kheri wazee wote katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.

Kadhalika mh Tundu Lisu mgombea urais wa JMT kupitia Chadema amewatakia kheri ya siku ya wazee duniani wazee wote.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nadhani hizo Heri zingekuwa na Baraka tele iwapo tu pension / retirement plans zingekuwa ni za ki-utu, sio mzee anazeeka badala yake anaonekana kama mzigo kwa jamii...., si matibabu, si pension wala hata kuomba watoto wake hawezi tena... (ukiniuliza kwanini) jibu ni kwamba hata watoto wake hawana ajira / kipato (tena ndio waliomfilisi mzee huyo kwa kuwekeza kwenye elimu yao)
 
Lissu wakomboe wazee wetu, pamekuwa na sera na maneno bila vitendo kuwaenzi wazee.CCM imekuwa ikiwajali wazee wastaafu waliokuwa na nyazifa pekee.
 
Mgombea Urais wa JMT kupitia CCM Dkt. Magufuli amewatakia kheri wazee wote katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.

Kadhalika mh Tundu Lisu mgombea urais wa JMT kupitia Chadema amewatakia kheri ya siku ya wazee duniani wazee wote.

Maendeleo hayana vyama!
Hivi miaka yote mitano ulishawahi sikia wanatakiwa heri hawa wazee wetu?
Halafu inabadi magufuli aseme wazee wenzake atawasaidiaje nasio kula pesa yao ya kiinua mgongo
 
JPM wakati anapambana na Lowassa alipiga push-ups nyingi mara kadhaa, ulifahamu maana yake? Dhihaka kwa Lowassa kuhusu afya yake. Rhetorical language.

Wakati huu anapambana na amepigishwa magoti mara mbili akiomba kura, unajua maana yake??

Mataga Tafuta thamani ya X......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom