Dkt. Magufuli: Mwanasayansi anayevumilia hasara ya "Type II Error" dhidi ya "Type I Error". Je, ni Utu?

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
Haya yote ni kwa ajili ya nini? Hili ni swali moja ambalo mtu yeyote makini anaweza kujiuliza kufuatia kitendo cha Rais Magufuli kutoa tuhuma wazi wazi dhidi ya watalaamu wa Maabara Kuu ya Afya kwa kuonesha kuwa na mashaka juu ya ukweli wa matokeo ya vipimo vya ugonjwa wa korona yanayotolewa na maabara hii. Jibu la swali hili kwa mujibu wa rais mwenyewe ni kwamba “hii ni vita”.

Kusema tu “hii ni vita” bila kufafanua ni nani hasa muanzilishi, nani mlengwa (adui) na huyo muanzilishi amekusudia kupata manufaa gani kutokana na matokeo ya vita hii, kunafanya jibu la Dkt. Magufuli liwe jepesi na kwa maana hiyo halikidhi swali ipasavyo. Hii ni kwasababu kama mlengwa (adui) wa vita hii ni taifa la Tanzania au serikali yake bado haiingii akilini kwa maana karibu nchi zote duniani zimepigika na vita hii ya korona bali kuna nchi nyingi zimeathirika zaidi ukilinganisha na Tanzania.

Lakini ingawa Rais Magufuli ni mwanasayansi (mkemia) na hupenda kuonesha “mamlaka” ya kisayansi aliyonayo katika changamoto/ukosoaji dhidi ya kazi za wanasayansi wenzake, bado ameshindwa kutoa ufafanuzi kwa kutumia hoja za kitaalamu juu ya “athari mbaya” zitokanazo na “majibu ya uongo” ya ugojwa (korona). Matokeo ya kushindwa huko kunawafanya watu watatizike (confused) kutokana na shutuma anazozitoa.

Ukweli ni kwamba, katika kufanya kipimo (diagnosis) kuna matokeo manne tu; mawili ya kweli na mawili ya uongo na kati ya hayo ni jibu moja tu ndo linaweza kuibuka (mutually exclusive events) kama ifuatavyo.

  • “Chanya kweli” (True Positive): Jibu hili hutokea pale ambapo matokeo ya kipimo yanaonesha uwepo wa ugonjwa wakati ni kweli kwamba ugonjwa upo.
  • Hasi kweli” (True Negative): Maana yake ni kwamba matokeo ya kipimo yanaonesha hakuna ugonjwa wakati ni kweli hakuna ugojwa.
  • Chanya uongo” (False Positive/Type I Error): Haya ni matokeo ya kipimo ambapo yanayoonesha kwamba ugonjwa upo wakati si kweli. Hili ni kosa (error) ambalo halitakiwi kwenye vipimo na kitaalamu huitwa” type I error”
  • Hasi uongo” (False Negative/Type II Error): Jibu hili hutokea pale ambapo kipimo kinaonesha hakuna ugonjwa wakati kiuhalisia ugonjwa upo. Hili nalo ni kosa na kitaalamu huitwa “type II error”.
Majibu yenye makosa (type I and type II errors) hayakubaliki kwenye vipimo kwavile yanapotosha maamuzi dhidi ya tatizo (mislead in decision making). Hasara inayoweza kusababishwa na majibu ya kipimo yenye type I error (FP) ni upotevu wa rasilimali (pesa, dawa, vifaa na muda) katika kupambana na tatizo au ugonjwa (intervention) ambapo kiuhalisia haupo. Huu ndio msingi wa malalamiko/tuhuma za Dkt. Magufuli kwa wataalamu wa maabara; yaani majibu ya vipimo vya korona yanayotolewa ni False Positive (kama ni kweli) ambayo yanabeba type I error na kwahiyo yanapelekea hasara kiuchumi na hofu ambazo hazina haja.

Kwa upande mwingine, majibu yenye type II error (False Negative) hasara yake ni kwamba hatua (interventional measures) zitaachwa kuchukuliwa dhidi ya tatizo kwa kuamini hakuna tatizo wakati ni kweli lipo. Mgonjwa ndiye anayeathirika moja kwa moja na majibu yenye type II error kwa kuwa anaweza kuendelea kuugua na hata kufa kwa kukosa matibabu akidhani ni mzima wakati kiuhalisia ni mgonjwa.

Kwakuwa Dkt. Magufuli halalamikii majibu ya False Negative (type II error) kwa ugonjwa huu wa korona maana yake yuko tayari ugonjwa uzidi kusambaa au watu wafe kwa kutochukuliwa hatua za kitabibu dhidi ya ugonjwa. Kiufupi ni kwamba Dkt. Magufuli yupo tayari kupoteza wananchi kwa korona kutokana na majibu yenye Type II error (FP) kuliko kupoteza rasilimali kutokana na majibu yenye Type I error (FN). Maana yake anajali zaidi vitu (uchumi) kuliko uzima wa watu.
 
Mkuu umenisaidia kukiweka vizuri kile nilichokuwa nijifikiriacho tangia nilipomsikiliza. Kiufupi sasa hivi wananchi wameachwa dillema na watajifia tu hovyo na hakuna hatua stahiki zitakazochukuliwa.

Kwa hatuna ile serikali imekimbia majukumu yake. Kama mashine ndizo hizo hizo zinazolalamikiwa basi tusitegemee kupokea report tena juu ya huu ugonjwa nchini mpaka tutakapopata zingine.

Pia hata wale watakaojihisi kuwa wako infected hawataona umuhimu wa kwenda hospitali kwasababu mashine za kupimia haziaminiki, so wengi wataendelwa kutumia mbinu za kijadi/kujifukiza hata wale walio serious mwishowe kujifia majumbani
 
X-bar,

Kama kuna mtu hatakuelewa, basi huyo labda atasaidiwa na maombi tu. Umeelezea vizuri sana.

Rais hakufanya jitihada zozote za kuangalia labda kuna watu wanapata majibu ya negative kumbe ni positive. Maana kama kuna makosa ya kipimo kama alivyoelezea, basi kuna uwezekano wote - kusema positive kumbe ni negative, na kusema negative kumbe ni positive.

Rais hasumbuliwi na jibu likiwa negative wakati ni positive ila anasumbuliwa sana na jibu likiwa positive kumbe ni negative. He is too biased.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom