Medecin
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 7,895
- 21,301
Kwa hiyo ndio tuwaruhusu wazae na kurudi shule, je wakirudi shule ndo umaskini wao utaisha?Mkuu umasikini ni chanzo cha matatizo mengi.
Nadhani unaona hata watoto wa kike wanashindwa kwenda shule kipindi wakiingia kwenye mzunguko wao wa hedhi kwa kukosa 1200 ya kununulia taulo za usafi. Matatizo kama hayo huwezi kuyaona shuke binafsi za bweni maana hivyo vitu wanapewa.
Unasikini unachangia mahuzurio mabaya shuleni, watoto wa kike wanakua exposed kwenye hatari ya wanaume ili wapate hela ya kuwasaidia kuishi.
Watoto wengi wanaopata mimba ni wa shule za kata, kwa kua muda mwingine wanajikuta katika mazingira ya kushawishika kitu ambacho sio rahisi kukuta kwenye shule binafsi .