Dkt. Magufuli. Mwanafunzi atakayepata mimba shuleni, asirudishwe shuleni

Mkuu umasikini ni chanzo cha matatizo mengi.
Nadhani unaona hata watoto wa kike wanashindwa kwenda shule kipindi wakiingia kwenye mzunguko wao wa hedhi kwa kukosa 1200 ya kununulia taulo za usafi. Matatizo kama hayo huwezi kuyaona shuke binafsi za bweni maana hivyo vitu wanapewa.

Unasikini unachangia mahuzurio mabaya shuleni, watoto wa kike wanakua exposed kwenye hatari ya wanaume ili wapate hela ya kuwasaidia kuishi.

Watoto wengi wanaopata mimba ni wa shule za kata, kwa kua muda mwingine wanajikuta katika mazingira ya kushawishika kitu ambacho sio rahisi kukuta kwenye shule binafsi .
Kwa hiyo ndio tuwaruhusu wazae na kurudi shule, je wakirudi shule ndo umaskini wao utaisha?
 
Ni sawa unachokisena ila huoni kuruhusu hilo litahalalisha hizo unazoziita changamoto ama kurubuniwa kuwa kitu cha kawaida?
Heri ipi, wazae waendelee na shule au wasizae wapoteze haki yao ya kusoma?

Mtu kubeba mimba kunamuondoleaje haki yake ya ya msingi ya kupata elimu?au unaona watoe mimba kisha waendelee na shule, maana kwa mtino huo tutasababisha watoto kutoa mimba na pia kupoteza uhai wao.

Ni haki ya kila mwanamke kupata mimba na wala haki yao ya kuoata mimba haiwaondolei haki zao nyingine kama elimu nk.

Tuache unafiki, tukubali kukabiliana na ukweli.
 
Ni haki ya kila mwanamke kupata mimba ila pia ni utovu wa nidhamu mwanafunzi kujihusisha na mapenzi akiwa shuleni, ikiwa umeruhusu mimba utawezaje kuzuia suala la mapenzi mashuleni?
 
Kwa hiyo ndio tuwaruhusu wazae na kurudi shule, je wakirudi shule ndo umaskini wao utaisha?
Shule au elimu ni haki yao ya msingi kabisa. Pia kupata mimba ni haki ya kila mwanamke maana anazaliwa hivyo kwamba atabeba mimba.

Sasa iweje mtu apate mimba ambayo ni haki yake imuondolee haki yake ya kupata elimu?

Shule haiondoi umasikini ila inamsaidia mtu kukabikiana na changamoto za maisha, shule ina faida kubwa na nyingi kuliko mtu kutokua na shule, hata kama haiondoi umasikini basi haina maana watu wasiipate.
 
Ila hajasema haruhusiwi kusoma, atasoma ila aidha kwa kuanza tena mwanzo katika shule nyingine ila si kuendeleza pale pale alipoishia, hivyo ndivyo nimeelewa au nyie mmwelewaje?
 
"SPEED & POWER WITHOUT BRAIN IS ZERO"
VIGEZO GANI VIMETUMIKA MTOTO WA SHULE AKIPATA MIMBA ASIRUDI SHULENI AU ARUDISHWE SHULENI BAADA YA KUPATA MIMBA.
LAZIMA TUANGALIE SOURCE NA FACTORS KUTATUA TATIZO HILI.
 
Ila hajasema haruhusiwi kusoma, atasoma ila aidha kwa kuanza tena mwanzo katika shule nyingine ila si kuendeleza pale pale alipoishia, hivyo ndivyo nimeelewa au nyie mmwelewaje?
Na wewe ndo wale wale. Kamuulize tena akufafanulie
 
"SPEED & POWER WITHOUT BRAIN IS ZERO"
VIGEZO GANI VIMETUMIKA MTOTO WA SHULE AKIPATA MIMBA ASIRUDI SHULENI AU ARUDISHWE SHULENI BAADA YA KUPATA MIMBA.
LAZIMA TUANGALIE SOURCE NA FACTORS KUTATUA TATIZO HILI.
Well said mkuu bridalmask. Tatizo letu, especially this time-ni kuwa na mwendo wa kasi mnooo. Mwaka 2013 kama sikosei wizara ya elimu walitishwa na ongezeko la wanafunzi kupewa ujauzito licha ya kuwepo kwa amri/sheria aliyoisisitiza Rais leo. Kutokana na kasi hiyo wizara iliazimia kuanzisha mchakato wa kuangalia uwezekano wa kuwarudisha shuleni mabinti wanaojifungua ili waendelee na masomo.

Ni kweli kama ulivyosema, ni muhimu sana kutumia ubongo katika suala hili. Kwangu mimi naona ni hasara zaidi kumzuia kuendelea na masomo binti anayepewa ujauzito baada ya kujifungua, kuliko ukimruhusu.
 
Back
Top Bottom