Dkt. Magufuli. Mwanafunzi atakayepata mimba shuleni, asirudishwe shuleni

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,037
2,000
Mheshimiwa Rais amesema katika kipindi chake cha utawala, mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari atakayepata mimba, hataruhusiwa kurudi shuleni.

"Awe kaipata kwa raha zake, awe kaipata kwa bahati mbaya, akishapata mimba, elimu ya serikali basi"

Amezitaka NGOs zinazowatetea ziwafungulie shule za wazazi.

"Serikali haiwezi kusomesha wazazi", amesisitiza.
 
kiduni

JF-Expert Member
Jun 26, 2015
239
250
Ni kweli maana kuna vitu vikiruhusiwa itakua vurugu kwenye shule za serikali hasa ikizingatiwa siku hizi wanafunzi wanaanza mapenzi mapema, kama nia ya kusoma na wazazi wao wana nia ya kusomesha binti zao ipo njia nyingine ya kusoma kwa kufanya mitihani kama watahiniwa binafsi[private candidate]
 
Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,042
2,000
Vizuri kama kaweka hiyo exclusion kua akipata mimba asirudi shule za serikali.

Ila hii sioni kama ni nzuri, watoto wengi wanaopata mimba wakiwa shuleni ni watoto wa maskini wanaosoma shule za kata ambapo wanakua katika changamoto kubwa hivyo kushawishika kuvuliwa chupi.

Akisema hakuna kurudi shuleni, sioni kama ni sawa.
 
mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,396

Kwani sisi hatukuziona hizo changamoto? mbona tulivumilia
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,384
2,000
Ukiwa unaongea pekeyako unaweza kusema lolote na isiwe shida!!
 
Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,544
2,000
Ni lazima , tuwe na vigezo na vizingatiwe.

Safi, rais Dr. Magufuli, kwa kauli madhubuti.
 
kuuuu

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
391
250
Hii ni nzur zana hata dada zetu watsoma maana watajua umuhim w kusoma au kupigwa mimba, ww ni mwanafunz kwa nn upigwe mimba hii ni raha ya ote iweje apate mmoja mimba mwingne apate adhabu inakujaje?hapa safi kabisa
 
Zesh

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
14,624
2,000
Vizuri kama kaweka hiyo exclusion kua akipata mimba asirudi shule za serikali.

Ila hii sioni kama ni nzuri, watoto wengi wanaopata mimba wakiwa shuleni ni watoto wa maskini wanaosoma shule za kata ambapo wanakua katika changamoto kubwa hivyo kushawishika kuvuliwa chupi.

Akisema hakuna kurudi shuleni, sioni kama ni sawa.
Nimesoma shule ya kata miaka minne.....sijawahi kujazwa .......namuunga mkono rais litoto likipata mimba likae hukohuko....mitoto ya siku hizi ina tamaa balaa
 
prospilla

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
784
1,000
Vizuri kama kaweka hiyo exclusion kua akipata mimba asirudi shule za serikali.

Ila hii sioni kama ni nzuri, watoto wengi wanaopata mimba wakiwa shuleni ni watoto wa maskini wanaosoma shule za kata ambapo wanakua katika changamoto kubwa hivyo kushawishika kuvuliwa chupi.

Akisema hakuna kurudi shuleni, sioni kama ni sawa.
Mkuu mbona unausingizia sana umaskini? Hata kupata kupata mimba una husisha na umaskini pamoja na shule za kata?
 
Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,042
2,000
Mkuu mbona unausingizia sana umaskini? Hata kupata kupata mimba una husisha na umaskini pamoja na shule za kata?
Mkuu umasikini ni chanzo cha matatizo mengi.
Nadhani unaona hata watoto wa kike wanashindwa kwenda shule kipindi wakiingia kwenye mzunguko wao wa hedhi kwa kukosa 1200 ya kununulia taulo za usafi. Matatizo kama hayo huwezi kuyaona shuke binafsi za bweni maana hivyo vitu wanapewa.

Unasikini unachangia mahuzurio mabaya shuleni, watoto wa kike wanakua exposed kwenye hatari ya wanaume ili wapate hela ya kuwasaidia kuishi.

Watoto wengi wanaopata mimba ni wa shule za kata, kwa kua muda mwingine wanajikuta katika mazingira ya kushawishika kitu ambacho sio rahisi kukuta kwenye shule binafsi .
 
Ni sawa unachokisena ila huoni kuruhusu hilo litahalalisha hizo unazoziita changamoto ama kurubuniwa kuwa kitu cha kawaida?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom