Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Miaka mitano ijayo tutawakatia bima ya Afya Wananchi wote wa Tanzania

..kwa hiyo ccm wanamuunga mkono Tundu Lissu?

..tulikuwa mwezi mzima tunabishana kuhusu suala hili.

..na makada watiifu wa ccm wakisema haiwezekani Tz na bima ya afya kwa wananchi wote.

..ushabiki wa vyama wakati mwingine ni mbaya sana.

cc Kilatha

Mkuu Magufuli katamka hivyo ili apate kura, lakini hana uwezo wa kutekeleza hilo akipita tena. Fahamu kuwa ana miradi miwili mikubwa ya 15t+ achia mambo mengine, na kwenye miradi hiyo hajafika hata 5t. Ni wapi atapata 10t, kisha atekeleze na hilo la bima ya afya?
 
Hakika.
Screenshot_2020-09-24-19-55-15-1.jpg
 
Pana tofauti kubwa Kati ya huyo chambo wa Mabeberu na JPM katika ahadi hii

Mmoja Anasema, maendeleo ya vitu hayafai, maana yake, hospital na vituo Vyote vya Afya vilivyojengwa na miundo Mbinu mingine si kitu kwake na huwenda ikabomolewabomolewa pindi atakspoingia mjengoni

Na kama miundombinu hiyo si looote, Je atawaketia bima wananchi Ili ziwasaidie nini wakati hakuna miundombinu ya Majengo ya vituo vya afya?

Lakini huyu mtu Bora;"" anahalali SASA ya kusema hivyo Kwa kuwa kila kitu kipo kuhusu sector hiyo!

JPM Twende kazi,

Hata kwenye ufisadi uliahidi kushughurikia, uzembe pia na matumizi mabovu ya fedha za serikali na umeweza!!

Halafu Mitandao mnayoizungumza hiyo ya Twitter, sjui JF haina watu weengi kama Fecbook Instagram huko ndo tundu hajawahi kufahamika huko
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema kwa miaka mitano ijayo wakipata ridhaa kutoka kwa wananchi watakata bima ya afya kwa kila mwananchi

Amesema kwanza walikuwa wanaboresha miundombinu na kwa miaka mitano anayoimaliza tayari wameshajenga hospitali na vituo vya afya vya kutosha zoezi linalofuata ni kuwakatia bima watu wote milino 60 waliopo Tanzania

Amesema jambo la kumpa bima kila mwananchi linawezekana kwa kuwa wanafahamu hela za kutimiza hilo watakapozitoa

Amesema hadi sasa wameshaajiri madaktari zaidi ya 1,000 na watumishi wa afya zaidi ya 14,000. Anasema wamepanga kwa kuwa wanajua watakavyotekeleza
Kiongozi thabiti ni yule mwenye uwezo wa kupanga vitu kwa sasa ili kuchagiza maendeleo ya baadae. Chagua Magufuli
 
Mkuu Magufuli katamka hivyo ili apate kura, lakini hana uwezo wa kutekeleza hilo akipita tena. Fahamu kuwa ana miradi miwili mikubwa ya 15t+ achia mambo mengine, na kwenye miradi hiyo hajafika hata 5t. Ni wapi atapata 10t, kisha atekeleze na hilo la bima ya afya?
Mzee wa copy and paste haibu
 
Huu ni uongo. Kama ana nia japo kidogo, yeye labda aseme kila Mtanzania atapimwa bure malaria, mkojo na stool then dawa akajinunulie.

Otherwise ni uongo mtupu kumpatia Bima bure bwerere kila Mtanzania
 
Ni aibu kubwa ,uzalilisjaji na fedheha hospitali za umma, wengi wanapoteza maisha mbele ya matabibu kwa kukosa madawa na vifaa tiba.
Vitu vya umuhimu vilikuwa sio vifaa tiba na huduma bora za kiafya, ila majengo ndio yalikuwa na umuhimu zaidi ya afya za watanzania.
 
Ata yeye Lisu anajua anakwenda kuangukia pua katika uchaguzi huu, tatizo anakwenda kushindwa vibaya na illo ndilo wanalo liogopa, kwasasa vinatafutwa visingizio.
 
Back
Top Bottom