Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli kuagiza na kupiga simu Wizara fulani walete huduma sehemu mara moja, NEC hii rushwa

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,395
512
NEC mbona mgombea CCM anavunja sana maadili na hawampi adhabu? Akivaa kijani yupo kama mgombea na mbona anazungumuza tumetenga hela, nitawaletea hiki hela ipo, anapiga simu kwa Mfugale kuhusu daraja like au kile. Anapiga simu kwa makatibu wakuu wa wizara mpaka kwa mawaziri. Hii sio rushwa kweli?

Maana kutamka mkiletea wa chama kingine sileti maendeleo kwenu, sio rushwa hiyo NEC? Inamaana anataka wote wawe CCM? Wananchi kubagulia kwenyehuduma sababu ya vyama.

Yeye anasema maendeleo hayana chama, lakini yeye ndo nambari moja kuhubiri uchama kwenye maendeleo. Hili tume wanafanya kusudi sana na ni upendeleo wa waziwazi kwa CCM.
 
huwezi tena kutofautisha nec na ccm, usiumize kichwa mkuu, hapo ni mwanachama kutetea maslahi ya mwenyekiti wake.

tulihitaji katiba mpya kabla ya uchaguzi
 
ma, lakini yeye ndo nambali moja kuhubiri uchama kwenye maendeleo. Hili tume wanafanya kusudi sana na ni upendeleo wa waziwazi kwa CCM.
Katiba mpya inahitajika. Wakati kama huu nafasi ya urais ikaimishwe kwa na Jaji mkuu.
 
NEC, Magufuli, CCM na upinzani wote wanajua anachofanya Magufuli ni kosa. Tatizo ni kwamba, Magufuli hapangiwi, na Watanzania wengi hawajali Magufuli akivunja sheria na katiba, bado anabaki mpendwa wao. Huo ndio ukweli.

Tanzania ni nchi ambayo Magufuli anaweza kumnunulia Bombardie my wife wake kwa hela ya serikali na hakuna atakachofanywa, na watu bado watamshangilia kwa kumnunulia my wife wake Bombardier kwa hela ya serikali. Nadhani umeelewa hali ilivyo.

Jiulize kama tatizo ni Magufuli au Watanzania.
 
Back
Top Bottom