Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Huwezi ukaacha kujenga reli, ukasema hii hela naenda kupandisha mishahara

Mkuu huyo anajiita KICHAA na ukweli anacho na huko kujichanganya kuhusu mishahara ni ushahidi tosha kabisa wa kichaa chake.

Kwahiyo hajapandisha mishahara!Sasa mbona hapo anasema amepandisha mishahara???
Kama sielewi vile!
 
Kwahiyo hajapandisha mishahara!Sasa mbona hapo anasema amepandisha mishahara???
Kama sielewi vile!
Huyo ndiyo Magu mara nimetembea ulimwengu mzima mara sijasafiri nje ya nchi isipokuwa nilipokwenda masomoni haeleweki
 
Haki ni pamoja na usawa, huwezi zungumzia haki wakati usawa hakuna, yani wafanyakazi wawe na mishahara mikubwa wakati wanafunzi wanakaa chini, wawe na laptop wakati hatuna maabara, mishahara yenyewe ikiwa mikubwa watashindwa kujenga na kununua magari kwasababu miundombinu ya kuendesha magari itakuwa mibovu, watashindwa kusafirisha vifaa vya ujenzi kwani gharama itakuwa kubwa sana kutokana na usafirishaji ndio maana tunajenga reli, mabwawa ya umeme n.k

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Katika yote uliyo yaorodhesha hakuna hata moja linalo husiana na usawa. Mfano wa wafanyakazi kutoongezwa mishahara/kutopandishwa madaraja havihusiani na wanafunzi kukaa chini.

Usawa ni labda ungetolea mfano wa mwalimu kutokulipwa kwa wakati achilia mbali mshahara husiokidhi majukumu ya mwalimu, na wakati huo huo kwa mbunge ukiondoa mshahara posho yakuhudhuria kikao pia analipwa kwa wakati, yaani akisaini kuhudhuria kikao tu 340,000 inamuhusu. Hapa ndio tutazungumzia kukosekana kwa usawa.

Mengine yote yanabaki kuwa haki.
Mwanafunzi kukaa chini ama kwenye dawati bado mwalimu analo jukumu lakumfundisha, hivyo ni haki ya mwalimu kuongezewa mshahara/kupandishwa daraja.
Walimu hawajapandishwa mishahara/madaraja, je wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati?
Mishahara/madaraja havijapandishwa je kunatumika laptop?
Mishahara/madaraja havija pandishwa je tuna maabara ngapi za uhakika?
Kama kutoongezwa mishahara/kupandishwa madaraja ni kwa ajili ya maabara kwa nini vipimo bado vinatuambia papai na mbuzi vina corona?

Watu hawatoshindwa kujenga kwa sababu yakuongezwa mishahara, badala yake wameshindwa kujenga kutokana na kutoongezewa mishahara na kodi hisiyo rafiki kwenye vifaa vya ujenzi.

Watu hawatoshindwa kununua magari ndani/nje ya nchi kwa sababu yakuongezewa mishahara ama miundombinu, badala yake watashindwa/wameshindwa kwa kutoongezewa mishahara na mfumo wa kodi/ushuhuru husio rafiki.

Maendeleo ya watu ndiyo yanayo zalisha maendeleo ya vitu. Kwa mfano reli ya Tanga - Korogwe - Moshi adi Arusha ni maendeleo ya vitu, lakini kwa kuwa watu walikosa maendeleo reli ile ilisimama kwa miaka takriban 26 bila kutumika. Leo hii tumetumia fedha nyingi kuikarabati lakini mishahara ya watumishi haija panda (watu hawana maendeleo). Je miundombinu hii itakuwa na faida gani kwa mwananchi?

Haki yakupanda misharaha kwa wafanyakazi ndio chachu ya maendeleo ya watu na vitu.
 
Washaurini basi wafute hiyo sheria maana waliiweka wao, mbona unawalalamikia watumishi as if walijitungia hiyo sheria? Rais wako anavunja sheria wewe uko busy kumshangilia, Je unafahamu kuvunja sheria ni kosa?
Kwani na wewe ni mtumishi wa Umma?? Rais wangu ni yupi?? Unashindwa kulink mawazo ya ubongo wako na mdomo wako?? by the way siwezi kuwalalamikia kwa sababu hawajui ni wapi wadai haki zao na kwa wakati gani.
 
Ila unaweza ukaaacha kulipa wahanga wa tetemeko fedha ukajenga airport Chato hehheh

Lissu ni YEYE!
 
Wananchi hawataki wagombea ambao hawajui shida zao; wagombea ambao wanaonekana kipindi cha kampeni tu. JPM analazimisha wananchi kuchagua ccm kwa nguvu, haiwezekani.
Mwananchi jua wewe ndio mwenye nguvu kipindi hiki, zitumie nguvu zako vizuri kuleta mabadiliko.
Unajiita kipanga Lakini ni kiazi! Huelewi tu! Ngoja 2025 utakuwa unamlilia JPM. Maendeleo ya nchi yanaanzia katika infrastructures siyo kugawa pesa kama njugu. Huoni sasa kenya na wazungu wana mpiga vita kwa vile anaimarisha miundombinu?
 
Mgombea urais wa ccm amesema, hawezi kuongeza wafanyakazi mshahara na huku anajenga reli,elimu bure,miradi mikubwa kwa sababu na wafanyakazi watatumia hivyo vitu

Poleni wafanyakazi ,twende na Lissu

=====
View attachment 1559428
DKT MAGUFULI: MARA

> Huwezi ukaacha kujenga reli, ukasema hii hela naenda kupandisha mishahara

> Huwezi ukaacha kujenga vituo vya afya, ukatumia hiyo hela kupandisha mishahara

#Uchaguzi2020
Huyu mtu si mzima, fisiemu kazi mnayo
 
..UBINAFSI ni kuacha kuwapa motisha watumishi wa umma, na kwenda kujenga airport ya kimataifa CHATO kijijini kwa Raisi.
Viwanja vya ndege vinajengwa na kukarabatiwa nchi nzima na watumiaji wake ni mamilioni ya watanzania na wageni.

Ni wengi kuliko hao laki tano na nusu walioajiriwa serikalini.

Uchumi endelevu unatazama mahitaji ya kila sekta.
 
Na ndiyo maana hayupo mfanyakazi wa nchi hii mwenye akili zake timamu kichwani, anaweza kumfagilia huyo magufuli kwa chochote.

Kiufupi tu hana faida kwa wafanyakazi wa nchi hii. Amejawa tu na dharau, kiburi, roho mbaya na ya kikatili, ubinafsi, unafiki, ubaguzi, nk. Nachelea tu kumuombea mabaya kwa sababu na yeye ni binadamu kama mimi! ila kiukweli anatuzingua sana wafanyakazi.

Huu ndiyo ukweli. Kazi kwenu watumishi
Kama anaona wafanya kazi wanammalizia hela zake si awafukuze wote ili awe ameokoa matrilioni mengi akamalizie miradi yake
 
Viwanja vya ndege vinajengwa na kukarabatiwa nchi nzima na watumiaji wake ni mamilioni ya watanzania na wageni.

Ni wengi kuliko hao laki tano na nusu walioajiriwa serikalini.

Uchumi endelevu unatazama mahitaji ya kila sekta.
Mkiona wafanyakazi wanawamalizia hela zenu muwafukuze tuu wote ili muokoe matrilion mengi ili mkamalizie miradi yenu
 
Bila shaka wewe utakua na PhD ya kubangua karanga! Wote ni wale wale tu. Mnakua na mavyeti mengi halafu mnakua na uelewa mdogo kwenye mambo ya kawaida kabisa.

Je, unafahamu kitendo cha Rais wako kusitisha mchakato wa wafanyakazi kupanda madaraja yao kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi, amesababisha mishahara kwa wafanyakazi kuto kutofautiana?

Yaani aliyeajiriwa mwaka 2014 na yule atakaye ajiriwa mwaka huu wa 2020, mshahara wao utafanana? Uonevu wa kijinga kabisa! Muwe mnamuelimisha huyo mtu wenu. Anazingua.
Achana nae, siku nyingine unapojibu comment check kwa "upana" humu ndni utakuta phd holder anabishana na muuza maaandazi vijiweni. au mtu aliyefeli hata darasa la saba.
 
Bila shaka wewe utakua na PhD ya kubangua karanga! Wote ni wale wale tu. Mnakua na mavyeti mengi halafu mnakua na uelewa mdogo kwenye mambo ya kawaida kabisa.

Je, unafahamu kitendo cha Rais wako kusitisha mchakato wa wafanyakazi kupanda madaraja yao kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi, amesababisha mishahara kwa wafanyakazi kuto kutofautiana?

Yaani aliyeajiriwa mwaka 2014 na yule atakaye ajiriwa mwaka huu wa 2020, mshahara wao utafanana? Uonevu wa kijinga kabisa! Muwe mnamuelimisha huyo mtu wenu. Anazingua.
Tatizo la Magufuri ni kutotii sheria, kupandisha mfanyakazi daraja na mshahara ni takwa la kisheria. Sheria za kazi zinamtaka muajiri kutekeleza hill. Tukisema anaendeshi nchi kwa akili na mawazo yake bila kufuata sheria, maana yake ndiyo hiyo. Na rais aliye chaguliwa kisheria na na aka APA kuilinda katiba, anatakiwe kuiendesha nchi kwa kufuata sheria

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kifupi huyu mtu ni mshamba na limbukeni. Kupewa madaraka anajiona yeye ndo Mungu. Ndo maana hata sheria zilizopo haziheshim idiot.
 
Mkiona wafanyakazi wanawamalizia hela zenu muwafukuze tuu wote ili muokoe matrilion mengi ili mkamalizie miradi yenu
Wafanyakazi watakumbukwa tu kwani umuhimu wao sio wa kuuliza, kinachoendelea kufanyika katika miundo mbinu Kina kwenda kuyagusa mpaka maisha ya wajukuu wa hao wafanyakazi.
 
Viwanja vya ndege vinajengwa na kukarabatiwa nchi nzima na watumiaji wake ni mamilioni ya watanzania na wageni.

Ni wengi kuliko hao laki tano na nusu walioajiriwa serikalini.

Uchumi endelevu unatazama mahitaji ya kila sekta.

..chato airport na mbuga ya wanyama iliyoanzishwa ni kwa ajili ya hoteli ya bwana mkubwa aliyojenga huko.

..lakini kwa sasa hivi hakuna ndege inatua Chato airport.
 
..chato airport na mbuga ya wanyama iliyoanzishwa ni kwa ajili ya hoteli ya bwana mkubwa aliyojenga huko.

..lakini kwa sasa hivi hakuna ndege inatua Chato airport.
Kuna dhambi gani mbuga ya wanyama na hoteli kuwa ni za bwana mkubwa?.

Kuna waliokatazwa kuwa na mbuga zao na hoteli
zao?.

Hizo mbuga zinawapa ajira wakenya na waganda na sio watanzania?.
 
Kuna dhambi gani mbuga ya wanyama na hoteli kuwa ni za bwana mkubwa?.

Kuna waliokatazwa kuwa na mbuga zao na hoteli
zao?.

Hizo mbuga zinawapa ajira wakenya na waganda na sio watanzania?.

..uwanja wa ndege, mbuga ya wanyama, na hoteli, ni kwa faidayake yeye sio, kwa faida ya waTz.
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom