Corona ipo haijaondoka ila nakubaliana na wewe imetumika kisiasa zaidi na wamekuza mambo na kutisha watu ila corona ipo, uzuri sisi population kubwa ni vijana, na kuna watu mpaka leo wakipima ndio utasikia labda anaambiwa positive, hata yeye anashangaa niko fresh ana jitenga hapati dalili zozote baada ya muda anapima negative. Sasa wa namna hiyo ni wengi sana, tumepata au tunapata na inaisha bila hata kujijuwa. Magufuli alichosaidia kuondoa ile hofu kama kiongozi lakini ndio dunia ilitakiwa hivyo, ila media zimekalia masaa 24 corona alfu moja wanakufa kila siku maambukizi alfu 10 muhimu kuwatisha watu tu. Wazee hatari kwako maskini wazee hofu ikawaingia wakafariki wengi tu. sidharau corona kama sidharau malaria ila asilimia kubwa wameuliza na hizi media za dunia. huko USA kwa kuwa media hazimpendi huyu mzee basi wanatumia karata ya corona kuonesha watu wasingekufa kama Trump angefanya hivi... zote ni siasa baada ya uchaguzi hutasikia tena. mimi nikiona habari wanaongelea corona tu nabadili.