Dkt. Magufuli asema Serikali imejipanga kulifanya eneo la Kanda ya Ziwa kuwa eneo la utalii mkubwa na aeleza kuwa utalii utainua hiyo Kanda kiuchumi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,071
2,000
Hahaha ndio maana mnakaa UVCC hadi mnazeeka, yani kanda ya ziwa aifanye iwe kivutio cha watalii?!

Mkisikia hivyo akili zinawaruka, kivutio ni nini sasa, nyie WASUKUMA au nini, ziwa au nini kiwe kivutio kwa watalii saa?!

Serengeti ipo hiyo inajulikana, kawaambia nini kitavutia watalii uko kanda ya ziwa mkakimbia mbio kuja kanzisha uzi?!
Kwa sasa kazi ni kujenga miundo mbinu ya utalii kama vile kuanzisha mbuga,kujenga barabara,kiwanja cha ndege karibu na mbuga ambacho tayari kipo Chato ,kuvutia wawejezaji wajenga mahoteli ambayo tayari mengine yameshakamiliki yenye hadhi za kitalii ,wawekezaji makampuni ya tours nk

Hatua hii ya kwanza ikikamilika shughuli ya utangazaji mkubwa ndani na nje utaanza pamoja na kuwa hata sasa kuna utalii tayari lakini mkubwa uko njiani baada ya main logistics kukamilika
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,804
2,000
Kwa sasa kazi ni kujenga miundo mbinu ya utalii kama vile kuanzisha mbuga,kujenga barabara,kiwanja cha ndege karibu na mbuga ambacho tayari kipo Chato ,kuvutia wawejezaji wajenga mahoteli ambayo tayari mengine yameshakamiliki yenye hadhi za kitalii ,wawekezaji makampuni ya tours nk

Hatua hii ya kwanza ikikamilika shughuli ya utangazji mkubwa ndani na nje utaanza pamoja na kuwa hata sasa kuna utalii tayari lakini mkubwa uko njiani baada ya main logistics kukamilika
Hahaha hivyo target yenu sio wananchi wa maeneo hayo, bali watalii!?

Kila kitu mafanya kwa ajili ya watalii sio wananchi?! Hao watalii sisi wanatusaidia nini?!

Ndio maana hamuongelei kutoa haki kwa raia, kwasababu nyie focus yenu ni watalii?!

Ndege za watali, barabara za watalii, mbuga za watalii, viwanja vya ndege vya watalii, sisi wananchi chetu kipi?!
 
INRI

JF-Expert Member
Oct 5, 2017
1,199
2,000
Cheki alivyo na akili Dk Magufuli mapori yalikuwa yakifuga majambazi kaweka mbuga za wanyama ukiingia tu kwenye mbuga kama sio mtalii ni risasi unadungwa PIA hizo mbuga hizo kaona hazina hazina uwanja wa kimataifa karibu na mbuga kaujenga uwanja wa ndege Chato wakitua tu na ndege zao safari kwenye mbuga zilizo jirani na uwanja
Ni yeye
tapatalk_1600270550830.jpeg
 
INRI

JF-Expert Member
Oct 5, 2017
1,199
2,000
Kapiga ndege wanne kwa mpigo

1.Kakomesha ujambazi kwenye mapori
2.Kaanzisha mbuga za wanyama kwenye mbuga iliyokuwa ikitumiwa na majambazi ili itumiwe na watalii
3.Kajenga uwanja wa ndege Chato Jirani na mbuga zilizoanzishwa kwa ajili ya watalii kutua
4.Kajenga barabara za kuelekea kwenye hizo mbuga
Upupu ndio maana huna likes.

Kafanya mambo mengi miaka mitano alisikika nyumbu.

Sasa KWANINI MNATUMIA NGUVU KUBWA?

INRI

JF-Expert Member
Oct 5, 2017
1,199
2,000
Wanaoweza kumpigia Kura Magufuli wanywa gongo na waliokata tamaa ya maisha TU!! Ila vijana wenye malengo ya kimaisha hawawezi kufanya huo upuuzi.
MTU mwenye akili hawezi kumpigia jiwe.

Ni yeye, wananchi wanamkubali bila mafuso, wanafunzi , buku saba.
tapatalk_1600270550830.jpeg
 
INRI

JF-Expert Member
Oct 5, 2017
1,199
2,000
Lisu hamna Kitu Dr magufuli akikohoa kwenye mkutano wa kampeni msubirie Lisu mkutano wake unaofuata utamsikia akihoji kwa nini Raisi Magufuli alikohoa kwenye mkutano wa kampeni badala ya kuhutubia?

KUKOHOA inakuwa sera ya yeye kuongelea hotuba ya mkutano!!!!
Yeye mbona anamjibu kila akipigwa spana na lissu?

Kumbe anatenga muda kupata darasa la lissu.

Ni yeye
IMG_20200916_081205.jpeg
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,083
2,000
Hahaha ndio maana mnakaa UVCC hadi mnazeeka, yani kanda ya ziwa aifanye iwe kivutio cha watalii?!

Mkisikia hivyo akili zinawaruka, kivutio ni nini sasa, nyie WASUKUMA au nini, ziwa au nini kiwe kivutio kwa watalii saa?!

Serengeti ipo hiyo inajulikana, kawaambia nini kitavutia watalii uko kanda ya ziwa mkakimbia mbio kuja kanzisha uzi?!
Usiwafokee kaka mkubwa
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
146,083
2,000
Magufuli asema serikali imejipanga kulifanya eneo la Kanda ya Ziwa kuwa eneo la utalii mkubwa kama ilivyo Kilimanjaro na Arusha na aeleza kuwa utalii utainua hiyo kanda kiuchumi.

Wale mliokuwa mkibeza uanzishaji mbuga za wanyama Mwanza, Kagera na Geita na ujenzi wa kiwanja cha ndege Chato mjipange upya hayo ni maandalizi kuelekea kukuza utalii mkubwa huko ambao utaongeza mzunguko wa pesa za ndani na za kigeni na ajira.

Mwanza tu pale mbuga ya saa nane Island iliyoko mjini kabisa utalii umeshika kasi kubwa sana baada ya kuhamisha wanyama toka maeneo mengine na kuwapeleka pale.

View attachment 1571327
Hizi habari za kufokewa na wapiga kura kule Kashozi ni za kweli au uzushi?
 
ighaghe

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
1,849
2,000
Hahaha hivyo target yenu sio wananchi wa maeneo hayo, bali watalii!?

Kila kitu mafanya kwa ajili ya watalii sio wananchi?! Hao watalii sisi wanatusaidia nini?!

Ndio maana hamuongelei kutoa haki kwa raia, kwasababu nyie focus yenu ni watalii?!

Ndege za watali, barabara za watalii, mbuga za watalii, viwanja vya ndege vya watalii, sisi wananchi chetu kipi?!
Nina wasiwasi na I'd yako mkuu. Sio kwamba unajiuliza maswali mepesi na ya kitoto ili ujijibu?
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,083
2,000
Sehemu ambazo zina asili ya utalii na ambazo hazihitaji nguvu kubwa kuinua utalii katika hayo maeneo zimetelekezwa badala yake wanaenda kutumia pesa nyingi sehemu nyingine...
What a joke before independence kulikuwa na shughuli za kitalii maeneo hayo.
Wewe unafikiri utalii ni kupanda tu mlima wa Kilimanjaro ?Tourism is a combination of many things.
Singapore kaeneo kadogo kama wilaya ya Temeke inapata watalii milioni 20 kwa mwaka.
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
9,443
2,000
Magufuli asema serikali imejipanga kulifanya eneo la Kanda ya Ziwa kuwa eneo la utalii mkubwa kama ilivyo Kilimanjaro na Arusha na aeleza kuwa utalii utainua hiyo kanda kiuchumi.

Wale mliokuwa mkibeza uanzishaji mbuga za wanyama Mwanza, Kagera na Geita na ujenzi wa kiwanja cha ndege Chato mjipange upya hayo ni maandalizi kuelekea kukuza utalii mkubwa huko ambao utaongeza mzunguko wa pesa za ndani na za kigeni na ajira.

Mwanza tu pale mbuga ya saa nane Island iliyoko mjini kabisa utalii umeshika kasi kubwa sana baada ya kuhamisha wanyama toka maeneo mengine na kuwapeleka pale.

View attachment 1571327
Madini yangeweza kabisa kubadilisha maisha ya watu wa hiyo kanda ya ziwa lakini serikali za ccm miaka yote zimeshindwa kutumia hiyo fursa ya madini wenyeji wamebaki kuwa waangaliaji tu. Hata utalii ukija mtakuwa watazamaji tu. Kuna mabadiliko lazima yafanyike kuwasaidia watu wa kanda ya ziwa na yanawezekana tu ccm iking'olewa
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,804
2,000
Usiwafokee kaka mkubwa
Hahaha kuna mtu haelewi utalii ni nini, vivutio ni nini, na mtalii ni nani, wao wakiamshwa na Bashiru wanakuja bila hata kufikiria.

Ndio maana nikawauliza nini kitavutia hao watalii huko kanda ya ziwa?!

Ila samahani kwa kuwafokea, hawa wazee hawajitambui ndio maana wanaitwa uvcc hadi wanazeeka.

Juzi kati walipewa title mpya eti JESHI LA AKIBA, Lisu akawaharibia ulaji.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,071
2,000
Hahaha hivyo target yenu sio wananchi wa maeneo hayo, bali watalii!?

Kila kitu mafanya kwa ajili ya watalii sio wananchi?! Hao watalii sisi wanatusaidia nini?!
Maskini hujui faida za watalii ? wakifika hujui kuwa mahoteli yanaingiza pesa kwa watalii wanaolala? Hujui kuwa watalii wakifika soko la vyakula linaongezeka kwa vyakula kuuziwa watalii hivyo kumsaidia mkulima na mfanya biashara wa vyakula kuinua kipato?

Hujui kuwa utalii ukiwepo mahali huongeza ajira kuanzia za waongoza watalii,ajira mahotelini,madereva ,usafiri wa magari sababu hawatembei kwa miguu hivyo mauzo ya vituo vya mafuta kuongeza mauzo nk

Hujui kuwa watalii pia hununua vitu vinavyouzwa na wenyeji kama vile bidhaa za sanaa nk

HUJUI KUWA MAPATO YA KODI ZITOKANAZO NA UTALII ndizo hutumika kutoa mikopo kwa akina mama na vijana wanaotaka kujiajiri kwenye halmashauri na pia hutumika kuboresha huduma za jamii eneo husika?
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,804
2,000
Nina wasiwasi na I'd yako mkuu. Sio kwamba unajiuliza maswali mepesi na ya kitoto ili ujijibu?
Hahaha kwa taarifa yako hii ID hadi Magufuli mwenyeketi wako anaifahamu,
Hebu tueleweshe mtalii ni nani na kivutio kitakuwa nini huko kanda ya ziwa?!
 
ighaghe

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
1,849
2,000
Hahaha kwa taarifa yako hii ID hadi Magufuli mwenyeketi wako anaifahamu,
Hebu tueleweshe mtalii ni nani na kivutio kitakuwa nini huko kanda ya ziwa?!
Kuna namna nyingi za kubana hoja zake za utalii akakosa majibu ila si kwa maswali uliyouliza.
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,804
2,000
Maskini hujui faida za watalii ? wakifika hujui kuwa mahoteli yanaingiza pesa kwa watalii wanaolala? Hujui kuwa watalii wakifika soko la vyakula linaongezeka kwa vyakula kuuziwa watalii hivyo kumsaidia mkulima na mfanya biashara wa vyakula kuinua kipato?

Hujui kuwa utalii ukiwepo mahali huongeza ajira kuanzia za waongoza watalii,ajira mahotelini,madereva ,usafiri wa magari sababu hawatembei kwa miguu hivyo mauzo ya vituo vya mafuta kuongeza mauzo nk

Hujui kuwa watalii pia hununua vitu vinavyouzwa na wenyeji kama vile bidhaa za sanaa nk

HUJUI KUWA MAPATO YA KODI ZITOKANAZO NA UTALII ndizo hutumika kutoa mikopo kwa akina mama na vijana wanaotaka kujiajiri kwenye halmashauri na pia hutumika kuboresha huduma za jamii eneo husika?
Sasa Magufuli kawaambia nini kitakuwa kivutio na nani atakuwa mtalii?!

Watalii wanakuja serengeti kila siku Magufuli ndiye huwaleta?!

Kabla ya Magufuli watalii walikuwa hawaji serengeti?!

Hamna hoja mnabwabwaja tu.
 
ighaghe

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
1,849
2,000
Mbona hujayajibu sasa?!
Sijayajibu kwa sababu naamini yupo kwenye kampeni na anajua anachofanya na atakachokipata kwa kutetea analolitetea liwe lina maana au halina maana.

Ww uliyeamua umjibu ulitakiwa utlist umtendee haki.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom