Dkt. Magufuli asema Serikali imejipanga kulifanya eneo la Kanda ya Ziwa kuwa eneo la utalii mkubwa na aeleza kuwa utalii utainua hiyo Kanda kiuchumi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,071
2,000
Dr Magufuli asema serikali imejipanga kulifanya eneo la Kanda ya Ziwa kuwa eneo la utalii mkubwa kama ilivyo Kilimanjaro na Arusha na aeleza kuwa utalii utainua hiyo kanda kiuchumi.

Wale mliokuwa mkibeza uanzishaji mbuga za wanyama Mwanza, Kagera na Geita na ujenzi wa kiwanja cha ndege Chato mjipange upya hayo ni maandalizi kuelekea kukuza utalii mkubwa huko ambao utaongeza mzunguko wa pesa za ndani na za kigeni na ajira.

Mwanza tu pale mbuga ya saa nane Island iliyoko mjini kabisa utalii umeshika kasi kubwa sana baada ya kuhamisha wanyama toka maeneo mengine na kuwapeleka pale.

1600249989753.png
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,071
2,000
Cheki alivyo na akili Dk Magufuli mapori yalikuwa yakifuga majambazi kaweka mbuga za wanyama ukiingia tu kwenye mbuga kama sio mtalii ni risasi unadungwa PIA hizo mbuga hizo kaona hazina hazina uwanja wa kimataifa karibu na mbuga kaujenga uwanja wa ndege Chato wakitua tu na ndege zao safari kwenye mbuga zilizo jirani na uwanja
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,071
2,000
Kwahiyo kaharibu makazi ya watu wengine wenye shughuri maalumu!!!!! Kazi ipo.
Kapiga ndege wanne kwa mpigo

1.Kakomesha ujambazi kwenye mapori
2.Kaanzisha mbuga za wanyama kwenye mbuga iliyokuwa ikitumiwa na majambazi ili itumiwe na watalii
3.Kajenga uwanja wa ndege Chato Jirani na mbuga zilizoanzishwa kwa ajili ya watalii kutua
4.Kajenga barabara za kuelekea kwenye hizo mbuga
 

issa yurry

JF-Expert Member
Apr 20, 2014
453
1,000
Cheki alivyo na akili Dk Magufuli mapori yalikuwa yakifuga majambazi kaweka mbuga za wanyama ukiingia tu kwenye mbuga kama sio mtalii ni risasi unadungwa PIA hizo mbuga hizo kaona hazina hazina uwanja wa kimataifa karibu na mbuga kaujenga uwanja wa ndege Chato wakitua tu na ndege zao safari kwenye mbuga zilizo jirani na uwanja
Kwahiyo kumbe mpaka pale bungeni nyumba za wabunge na mawaziri kuna mbuga za wanyama maana lisu alipigwa risasi maeneo yale

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,071
2,000
Sehemu ambazo zina asili ya utalii na ambazo hazihitaji nguvu kubwa kuinua utalii katika hayo maeneo zimetelekezwa badala yake wanaenda kutumia pesa nyingi sehemu nyingine...
Hayo maeneo yanapita ukubwa wa mbuga za Burigi na Ibanda na Rumanyika zilizoko kanda ya ziwa ?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,071
2,000
Safi sana tunataka kusikia mipango mgombea aliyonayo sio masimango tu kama anavyofanya mgombea mmoja.
Lisu hamna Kitu Dr magufuli akikohoa kwenye mkutano wa kampeni msubirie Lisu mkutano wake unaofuata utamsikia akihoji kwa nini Raisi Magufuli alikohoa kwenye mkutano wa kampeni badala ya kuhutubia?

KUKOHOA inakuwa sera ya yeye kuongelea hotuba ya mkutano!!!!
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,804
2,000
Hahaha ndio maana mnakaa UVCC hadi mnazeeka, yani kanda ya ziwa aifanye iwe kivutio cha watalii?!

Mkisikia hivyo akili zinawaruka, kivutio ni nini sasa, nyie WASUKUMA au nini, ziwa au nini kiwe kivutio kwa watalii saa?!

Serengeti ipo hiyo inajulikana, kawaambia nini kitavutia watalii uko kanda ya ziwa mkakimbia mbio kuja kanzisha uzi?!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom