Dkt.Magufuli aibukia Njombe aungana na Filipokunjombe ujenzi barabara za Liganga

Qualcomm

Senior Member
Nov 27, 2013
177
138
Leo Dkt.Magufuli kama ilivyokuwa kwa Filipokunjombe amesisitiza Makandarasi wanaojenga barabara za kwenda Liganga kwenye makaa ya mawe zikamilike ndani ya muda uliopangwa na kuheshimu matakwa ya Mkataba, alisema kusiwepo na kisingizio cha kuwa wao ni wakandarasi wazalendo. Alisisitiza barabara hizo zinatakiwa zikamilike mapema tayari kwa kupitisha mitambo yenye uzito wa tani 150 itayaosafirishwa kwenda Liganga.

Aidha, Dkt.Magufuli akiongea na Wafanyakazi wa TANROADS, TEMESA na TBA wote wa Mkoa wa Njombe alimhakikishia Kaimu RAS wa Mkoa wa Njombe kuwa serikali kupitia Wizara ya Ujenzi mwaka wa fedha 2014/2015 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 28 kutoka mfuko wa barabara ambapo shilingi bilioni 17 zitatumika kwenye barabara kuu na za mikoa na shilingi bilioni 11 ni kwa ajili ya kuhudumia barabara zilizo chini ya Halimashauri.

Katika hatua nyingine Dkt.Magufuli amewahakikishia wananchi wa Njombe ya kuwa mwaka huu wa fedha 2014/2015 serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuanza kuzijenga barabara za Njombe kwenda Makete yenye urefu wa kilomita 109.4 na ile ya Itoni kwenda Manda yenye urefu wa kilomita 211 kwa kuanzia kila barabara zitajengwa kwa kiwango cha lami kilomita 50.

Hivi ndo ilivyokuwa:
attachment.php
attachment.php
attachment.php

Dkt.Magufuli,Dkt.Wanyancha (M/Kiti Mfuko wa Barabara), Kaimu RAS Njombe,Wafanyakazi wa TANROADS,TEMESA na TBA wote kutoka Mkoa wa Njombe walipokutana kwenye kikao na Waziri wa Ujenzi.
 

Attachments

  • 3c42e284c21e8c97097c1db383303fe3.jpg
    3c42e284c21e8c97097c1db383303fe3.jpg
    71.5 KB · Views: 1,446
  • b25d1b9dcd61e96c798595a210cb5045.jpg
    b25d1b9dcd61e96c798595a210cb5045.jpg
    78.2 KB · Views: 1,133
Mh.Magufuli unapohimiza wakandarasi wamalize kazi ndani ya muda,himiza pia watendaji wako .Walipe kwa wakati certificate zinapofikishwa kwao,tunanyanyasika sana kwenye malipo!
 
Kamanda Magufuli piga kazi watanzania wanakuona ipo siku watakuajiri kwa kazi kubwa!
 
Hongera waziri Magufuli kwa kuibukia mikoa yz kusini.
Sasa bado mkoa wa Mbeya.
Wiki iliyopita niliweka sredi ya kuuliza Magufuli mbona ziara zake ni mikoa ya kanda ya ziwa, sasa anajibu kiu yangu
 
Njombe imesahaulika hasa wilaya ya makete .. wangingombe na ludewa..
Barabara zinazo takiwa kujengwa
1. Njombe makete
2.Njombe Ludewa
3. Njombe.. igwachanya hadi ilembula
 
Back
Top Bottom