Akitoa maoni yake Dr. Azavel Lwaitama mdau mkubwa katika harakati za kutafuta nchi yenye demokrasia iliyo stawi yenye maridhiano, umoja, uhuru na maendeleo amesikika huko Clubhouse kwenye mjadala wa moto unaohudhuriwa na watu wengi kuliko jukwa lingine lolote la kijamii.
Dr Lwaitama amewataka watawala na wadau woote wa siasa za tanzania kuwa wapole na wavumilivu ili kila raia achague upande wake anaopendezwa nao.
Kuhusu swala la katiba mpya Dr Lwaitama amesema kuwa Maridhiano ni serikali kuruhusu vyama na wadau mbali mbali kila upande utangaze sera na itikadi zake bila kufukuzana.
Lwaitama ambaye alikamatwa Mwaka jana akiwa katika kongamano la kutoa elimu ya Katiba mpya kwa vijana huko Mwanza amesema kuwa kuwindana na kufukuzana ni jambo la ajabu na linatia aibu.
Ameshauri vijana, wazee, matajiri kwa maskini kila mtu aachwe atafakari. Wanaotaka katiba mpya wahamasishane na wasio taka pia waachwe wahamasishane na mwisho wa siku Wananchi wataamuwa wenyewe badala ya kile kinachofanykka sasa.
Amewataka vijana wa chadema waache kupoteza muda kujibizana na vijana wa ACT kuhusu matakwa yao ya Tume huru ya uchaguzi kwanza na kwamba hiyo ndio demokrasia ya vyama vingi kuwa na mawazo huru.
Wito kwa serikali na vyombo vyake pia umetolewa kwa kuruhusu wananchi wafanye na kutekeleza wajibu wao wa kikatiba bila kusumbuliwa na mwisho wa siku Wananchi wenyewe wataamuwa kama wanataka katiba mpya au la! badala ya kutumia malungu.
Msikilize Mwanazuoni Huyu hapa.