Dkt. Louis Shika: Undercover informer aliyenusurika kifo ughaibuni?

Hihihiiii..jamaa anafunga mwaka huyu.mpaka nimemkumbuka babu wa samunge alivyotikisa enzi zake,mwaka huu ni wa Dr
Kuna kitu cha kumakinika hapo , hivi online transfer ya USD million moja bima yake ni dola mia?
 
Pia suala la kusafirisha pesa kwa Cheque kwa njia ya currior kidogo lina ukakasi,siku hizi kila kitu ni online transfer(Swift).
Kama kweli Shika ni jasusi basi ina make sense kutumia Courier..Transfer ni rahisi kufuatiliwa tofauti na paperwork
 
Inaendelea...
7.Dr. Hakuwakimbia vibaka wa Moscow, kawakimbia watu ambao ni the professional killers.... Wahuni majambazi wa kupora wasingeweza kuwa na nguvu kuzidi serikali eti wamfuatilie mpaka airport ambako kwa hadhi yake na ulinzi ulivyo angeweza kulindwa mpaka anapanda jet lake na kuondoka. Na pia angepata hata wasa wa kuchukua kiasi na fedha nk.... Dr aliondoshwa in rush hour tena kwa ndege maalum ya malkia... Huyu alikuwa ni zaidi ya mtu aliyetaka kuporwa pesa...alikuwa ni kiungo mchezaji katika siasa na vita ya kimataifa... Na alikuwa anagombewa na pande mbili ama zaidi na kwa vyovyote ilikuwa ni mambo ya kijasusi na ushushushu.... Na katika kuondoka huko hakuwa na muda hata wa kufungasha na kuweka mambo yake sawa... Ilibidi aondoke hapo hapo alipokuwa saa hiyo hiyo ili aokoe roho yake, ama abaki na akutane na kilichomtoa kanga manyoya

8. Kurejea nyumbani Tanzania, kujificha na kujitenga kabisa na jamii
Kwakuwa anafahamu vema undani wa kisa kizima katika uhalisia wake, hata safari ya kurudi nyumbanj haikuwa ya moja kwa moja, alirudi zigzag kuwapoteza maboya watesi wake..
Dr. Alikuwa anajua kwa hakika bado anatafutwa. Hivyo akawa ni mtu asiyetulia sehemu moja huku akiishi kwa kujificha na maisha ya chini hasa... Alikata mawasiliano karibia na watu wote, akatumia simu ya hali ya chini kabisa... Akakata mawasiliano na mwenza wake aliyemwacha Urusi... Alijua akimtafuta tu.. Wamemdaka... Mtu aliyetaka kuporwa pesa hawezi kuishi kwa kujihami kiasi hiki... Si mtembezi hana mizunguko ya mbali.. Zaidi ya kwenda kwenye meza ya magazeti kujua nini kinajiri, si mtembezi wa usiku na muda mwingi hujifungia chumbani kwake...hana rafiki na hana mazoea ya karibu sana na watu wengi
9. Kwanini ajitokeze sasa tena kwenye mnada mkubwa?
Kila jambo lina wakati wake na ukitimia jambo husika hujifunua... Dr alifahamu fika ule mnada ungemuweka kwenye macho ya dunia.. Je haogopi tena kufa? Je watesi wake wamekufa wote? Nini kimemfanya ajitokeze sasa? Imethibitishwa polisi kuwa ni kweli ana pesa zake na mmarekani ndio anazishughulikia.. Kwanini mmarekani? Huyu mmarekani huwa hafanyi kazi ya hasara hata mara moja ukiona anakushika mkono jua unamfaa na mengi...hii ishu inaweza kuwa mwanzo wa tamati yenye break through kubwa sana.. Tuwe wapole tuwe na saburi...... .

Mwisho.........
Tumjifunza mengi kwenye ishu ya Dr. Shika, hasa tabia ya kufanya vitu kwa mazoea, kuwadharau wasomi wetu eti tu kwakuwa hawana mwonekano na kuwatukuza wanasiasa wezi...
Funzo lingine ni je tunao wasomi wangapi kama Dr Shika ambao serikali haiwapi heshima na kipaumbele halafu wanatumika na mataifa mengine kiasi cha kuhatarisha maisha yao?
Je tunao wangapi kama Dr Shika ambao tunadhani ni machizi fresh na kuwadharau huko kwenye mishe zetu kumbe wako kazini? Jiulize Dr Shika alivyokuwa ana act low profile kumbe ana mawasiliano na mmarekani na anafuatilia mabilioni yake? Alikuwa anawasiliana nao saa ngapi? Kwa njia gani?

Nimefarijika kuona kuwa kumbe Dr anathamini bado elimu yetu ya kienyeji.. Kubana kende unapopita kwenye mbwa wakali....
Umesikia na hiyo ya mtu aliyelala ukimuangalia usoni anaamka? Kuna siri gani hapo? Hili tutalijadili kwa leo niishie hapa ya haya machache ya Dr Shika...!!!!


NB. Nimeandika kwa muktadha wa mtazamo wangu kulingana na simulizi za mlengwa mwenyewe

Jr
Mshana frankly speaking nami nilipo ona video na baadhi ya mambo niliwaza kama ulivyoeleza.Nakubaliana na wewe ila hizo red highlihted jamaa alipozisema nilijua ana elimu extra na mtu wa kawaida.Sitaki kucomment sana kwa huyu Dr.
 
mshana jr si umeona jipya leo la pesa zimeenda wapi zile usd 100 na kupokelewa kama cash pickup.. haya shuka kutoka kwenye ungo wako uje uendeleze basi. Eeeeeh

Unajua from Day 1 mie napenda kujua kinachojiri juu ya Mzee wetu huyu.. ni level ingine.. najifurahia nilimnoti kuwa atakuwa na mengi siku hiyo alipotokeza.. na bado najua kuna mengi.. ila na yeye amezidi ujanja wa kuminyia yake shaaaaa.. simlaumu.
 
Ila yule polisi alimshusha thamani sana na kumweka kwenye kundi la wachovu kabisa.
Swali langu naimba lijibiwe, kwanini kaamua kujianika sasa na wakati amekaa miaka mingi akijificha na kukwepakwepa?
 
mshana jr si umeona jipya leo la pesa zimeenda wapi zile usd 100 na kupokelewa kama cash pickup.. haya shuka kutoka kwenye ungo wako uje uendeleze basi. Eeeeeh

Unajua from Day 1 mie napenda kujua kinachojiri juu ya Mzee wetu huyu.. ni level ingine.. najifurahia nilimnoti kuwa atakuwa na mengi siku hiyo alipotokeza.. na bado najua kuna mengi.. ila na yeye amezidi ujanja wa kuminyia yake shaaaaa.. simlaumu.
nilikuwa busy leo Coco nipe hint nifanyie kazi
 
Ila yule polisi alimshusha thamani sana na kumweka kwenye kundi la wachovu kabisa.
Swali langu naimba lijibiwe, kwanini kaamua kujianika sasa na wakati amekaa miaka mingi akijificha na kukwepakwepa?
Matumizi ya nyakati kila kitu huwa na mwisho wa matumizi
 
Je umejiiza maswali machache..
-kumaliza kusoma,akaanza kufundisha na ghafla akapata MTAJI wa kuanzisha kampuni kubwa hivyo?
-Rais wa kampuni anaondolewa kimya kimya,hata bodi ZA kampuni hawaelewi?
-mbona anaonyesha kama ni mission town fulani wa kipindi hicho( huko Russia),alifanya dili chafu ndio akaminywa hivyo.
-kweli pesa zinasafirishwa kwa staili aliyosema?
By the way,
Yote yanawezekana ,hatuna haja ya kumu under rate daktari huyo.
Serikali ilipaswa kumuwekea mazingira mazuri ili nae awe msukuma gurudumu la maendeleo badala ya kumchukulia poa tu.
 
Back
Top Bottom