Dkt. Louis Shika: Undercover informer aliyenusurika kifo ughaibuni?

Mimi nasubiri kitabu tu cha maisha ya Dr. Shika
Kwanza nimpe pole kamanda wa polisi aliyemu underrate Dr Shika kwamba hana thamani hata ya million... Hawa ndio makamanda wetu wenye dhamana kubwa ya kutulinda.... Tungesema sisi wa mitandaoni isingekuwa shida sana maana huku tuko mix grille, wajuzi na wajuvi wa kila jambo.. Kamanda hakujihangaisha kabisa kupata habari za huyu mtu kabla hajatoa taarifa yake mbele ya kamera.... Kumbe mtu aliyemdharau ni viwango vingine kabisa.. Mazoea yale yale ya kuwaamini wasaidizi na bila kujiridhisha na taarifa zao

Dr Shika ni mtu zaidi ya tunavyomfahamu, kaeleza machache kabaki na mengi, lakini machache aliyoasema yametosha kumchora picha yake halisi katika uhalisia wake..... Twende na dondoo zifuatazo

1. Masomoni Urusi na kuanzisha biashara kubwa
Achana na scholarship za siku hizi za kupeana... Wakati ule ukienda kusoma/kusomeshwa nje... Wewe ni cream... Historia inaonesha Dr Shika alikuwa vizuri sana kichwani tangu sekondari.... Na kwa vyovyote huko Urusi alifanya vizuri pia kitu kilichowavutia wengi...
Ni baada ya kumaliza masomo yake hakurudi nchini bali alibaki Urusi na kuanzisha biashara kubwa, yeye pamoja na washirika wengine ambao asili ya kukutana kwao haiwekwi wazi... Dr. Shika yeye ndio akawa rais wa kampuni kubwa yenye mtandao wa makampuni mengi.. Mafanikio ya haraka ya kampuni hii yaliwagutua warusi na kuanza kumdukua

2. Mafanikio ya kampuni na kumiliki mali nyingi
Kampuni yao hiyo bila kujulikana kwa hakika shughuli zao hasa ikawa ni kampuni inayokuwa kwa haraka mpaka kuwa na uwezo wa kumiliki ndege binafsi... Hapa warusi wakashtukia mchezo kuwa pengine hawa watu ni undercover informers wa wamarekani, na hii kampuni ni zuga tuu... Janja hii hutumiwa na mataifa mengi... Dr. Shika inapofikia hapa huwa na kigugumizi kidogo na bahati mbaya hatuna waandishi wanaojua kuhoji

3. Kuwindwa kutekwa na mateso
Dr. Hapa kuna kitu kikubwa sana anakificha.. Aliliwa timing ya muda mrefu mpaka alipokamatwa nyumbani kwake.. Inawezekana kabisa nyumba ilishakaguliwa yote.... Lakini pia style ya kuondoka naye wakiwa wamemfungia kwenye kabati maana yake huyu hakuwa mtu wa kawaida.

Kwa maelezo yake alipelekwa mpaka nje ya mji Kwenye nyumba yenye chumba cha siri chini ya ardhi na kuanza kuteswa, kwa madai kwamba watekaji walitaka pesa kiasi cha USD million moja... Dr hapa pia kasema uongo kuna kitu anaficha pia... Kwa utekaje huo watekaji wangetaka awapigie simu jamaa zake wakate mpunga (ransom).. Lakini Dr Shika anakiri kwamba alitekwa na kuteswa na the professionals toka KGB- shirika la kijasusi la Urusi... Kwa mateso yale hawa walikuwa wanamlainisha aseme yeye ni nani hasa.. Amekuwa mlemavu wa vidole vitano vya mikono.. Mkono mmoja viwili, mmoja vitatu, amevunjwa mbavu tano, na sikio moja limepindishwa kwasasa ya makofi... Majambazi wanaotaka hela hawana mateso ya namna hii.. Haya ni mateso ili ufunguke.. Roma anajua vema..

4. Ujasiri, uvumilivu na utulivu
Dr ana viashiria vyote vya majasusi, pamoja na mateso yote hayo na kujeruhiwa vibaya kabisa lakini hakupaniki wala kukata tamaa alikuwa mtulivu jasiri akisuburi one mistake one goal... Na akajenga nao urafiki yani hakuwa kiburi, unateswa unatukanwa unadhalilishwa unaumizwa lakini baada ya hapo unaenda nao sawa... Hii kitu ina mafunzo maalum.. Dr. Alikuwa mtulivu na mvumilivu mpaka akaweza kutoroka akiwa hoi kabisa...

5. Kutoroka kwake kunaacha maswali mengi, kwanini alibebwa na ndege maalum ya malkia wa uholanzi? Je ilikuwaje? Ni nani walifanikisha hii mipango? Kwanini mmarekani alitoa msaada mkubwa kwake mpaka akaweza kufika nchini salama? Je KGB walikuwa sahihi? Je alifanikiwa kuficha siri kuu ndio maana wamarekani hawakumtupa hata sasa?

6. Vifo vya washirika wake kwenye kampuni
Wenzake karibia wote walikufa kwa kuuwawa.. Yeye kaponea shimo la tewa (kuna maswali mengi sana kwenye hili..... Kampuni lao bado lipo lakini limesimamisha shughuli zake.. Wamarekani wanamsaidia Dr Shika kupata pesa zake! Kaamua kuishi nyuma ya wakati.... Osama alitumia hii mbinu kwa mafanikio makubwa.. Dr kaamua ku act low profile na kujitenga kabisa na harakati za dunia.....


ITAENDELEA........

7.Dr. Hakuwakimbia vibaka wa Moscow, kawakimbia watu ambao ni the professional killers.... Wahuni majambazi wa kupora wasingeweza kuwa na nguvu kuzidi serikali eti wamfuatilie mpaka airport ambako kwa hadhi yake na ulinzi ulivyo angeweza kulindwa mpaka anapanda jet lake na kuondoka. Na pia angepata hata wasa wa kuchukua kiasi na fedha nk.... Dr aliondoshwa in rush hour tena kwa ndege maalum ya malkia... Huyu alikuwa ni zaidi ya mtu aliyetaka kuporwa pesa...alikuwa ni kiungo mchezaji katika siasa na vita ya kimataifa... Na alikuwa anagombewa na pande mbili ama zaidi na kwa vyovyote ilikuwa ni mambo ya kijasusi na ushushushu.... Na katika kuondoka huko hakuwa na muda hata wa kufungasha na kuweka mambo yake sawa... Ilibidi aondoke hapo hapo alipokuwa saa hiyo hiyo ili aokoe roho yake, ama abaki na akutane na kilichomtoa kanga manyoya

8. Kurejea nyumbani Tanzania, kujificha na kujitenga kabisa na jamii
Kwakuwa anafahamu vema undani wa kisa kizima katika uhalisia wake, hata safari ya kurudi nyumbanj haikuwa ya moja kwa moja, alirudi zigzag kuwapoteza maboya watesi wake..
Dr. Alikuwa anajua kwa hakika bado anatafutwa. Hivyo akawa ni mtu asiyetulia sehemu moja huku akiishi kwa kujificha na maisha ya chini hasa... Alikata mawasiliano karibia na watu wote, akatumia simu ya hali ya chini kabisa... Akakata mawasiliano na mwenza wake aliyemwacha Urusi... Alijua akimtafuta tu.. Wamemdaka... Mtu aliyetaka kuporwa pesa hawezi kuishi kwa kujihami kiasi hiki... Si mtembezi hana mizunguko ya mbali.. Zaidi ya kwenda kwenye meza ya magazeti kujua nini kinajiri, si mtembezi wa usiku na muda mwingi hujifungia chumbani kwake...hana rafiki na hana mazoea ya karibu sana na watu wengi
9. Kwanini ajitokeze sasa tena kwenye mnada mkubwa?
Kila jambo lina wakati wake na ukitimia jambo husika hujifunua... Dr alifahamu fika ule mnada ungemuweka kwenye macho ya dunia.. Je haogopi tena kufa? Je watesi wake wamekufa wote? Nini kimemfanya ajitokeze sasa? Imethibitishwa polisi kuwa ni kweli ana pesa zake na mmarekani ndio anazishughulikia.. Kwanini mmarekani? Huyu mmarekani huwa hafanyi kazi ya hasara hata mara moja ukiona anakushika mkono jua unamfaa na mengi...hii ishu inaweza kuwa mwanzo wa tamati yenye break through kubwa sana.. Tuwe wapole tuwe na saburi...... .

Mwisho.........
Tumjifunza mengi kwenye ishu ya Dr. Shika, hasa tabia ya kufanya vitu kwa mazoea, kuwadharau wasomi wetu eti tu kwakuwa hawana mwonekano na kuwatukuza wanasiasa wezi...
Funzo lingine ni je tunao wasomi wangapi kama Dr Shika ambao serikali haiwapi heshima na kipaumbele halafu wanatumika na mataifa mengine kiasi cha kuhatarisha maisha yao?
Je tunao wangapi kama Dr Shika ambao tunadhani ni machizi fresh na kuwadharau huko kwenye mishe zetu kumbe wako kazini? Jiulize Dr Shika alivyokuwa ana act low profile kumbe ana mawasiliano na mmarekani na anafuatilia mabilioni yake? Alikuwa anawasiliana nao saa ngapi? Kwa njia gani?

Nimefarijika kuona kuwa kumbe Dr anathamini bado elimu yetu ya kienyeji.. Kubana kende unapopita kwenye mbwa wakali....
Umesikia na hiyo ya mtu aliyelala ukimuangalia usoni anaamka? Kuna siri gani hapo? Hili tutalijadili kwa leo niishie hapa ya haya machache ya Dr Shika...!!!!

NB. Nimeandika kwa muktadha wa mtazamo wangu kulingana na simulizi za mlengwa mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr shika ni mtu ambaye alisoma vizuri na kuwa na maisha yake.badaye akapata matatizo ya akili. Na kuanza ku hallucinate. Watu wa namna hii huwa wanaweza kukusimulia tukio several times ukaamini lilivyo kama vile ni wahusika but not. HAJAWAHI KUWA UNDERCOVER AGENT NA HAITATOKEA AKAWA.SABABU KISAIKOLOJIA HAYUPO SAWA.

NA ANGEKUWA undercover USA wasingemwacha rogue undercover awe anabwabwaja tu huku dar.isingetokea.jamaa alitumia udhaifu wake kutengeneza pesa. Na sasa amerudi majalala. Kuna wanaijeria walimtapeli pesa kwenye mitandao wakamwambia watamtumia mabilion ya pesa ndo hizo pesa alikuwa anadai zinakuja...mpaka leo yupo majalala hamna tena anayemjali.

Mzee mshana jr. Ulitirirka kweli kwenye huu uzi. Lakini bado simuamini dr shika na hizi drama zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Undercover gani huyu
Mlimpaa sifa tu.... Za Bure

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina hakika
tapatalk_1581494550554.jpeg


Jr
 
Kweli siku hazigandi... Tuko season ya Pierre sasa.... Dr.. Kapotea kusikojulikana na mamilioni hatujawahi kuyaona... Kwa simulizi zake na mambo aliyopitia.... Kweli duniani kuna viumbe wa aina yake, na huyu ni mmojawapo

Jr
Hiki kitendo pekee kilikuwa kinatosha kabisa kuwafanya watu wenye upeo waache kuendelea kuhoji uhalali wa maudhui ya uzi huu. Yaani mtu mwingine anataka mpaka asikie Dr. Shika mwenyewe anataja kuwa ni agent, wakati hata kwao huko Masaki wanaishi nao ma-agent kibao na hawajawahi kuwatamkia hayo, sasa ije iwe kwa Dr. Shika? Yaani mtu anakuwa hawezi kabisa ku-connect dots tu kutoka kwenye maongezi ya mtu husika?
 
Nimeshangazwa sana na pierre kuingia bungeni .
What was the reason ya bunge kuruhusu kijana mwenye kauli tatanishi kuingia bungeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi huwa nahisi labda ni kwa sababu kuna mtu A aliwahi kupishana kauli kidogo na baadhi ya Wabunge, halafu baadaye tena huyo mtu A akawa ameingia kwenye kimgogoro kidogo cha maneno na Peter Maji. Nadhani sasa wale aliopishana nao kauli kwa mara ya kwanza, wakatengeneza joint forces na Peter Maji, kama kitendo cha kuonyesha kuwa wanamsuta mtu A. Sipingi hoja ya Peter Maji kukaribishwa Bungeni kwa sababu ni haki/ upendeleo wake unaotokana na uraia, ambao mtu yeyote ambaye ni raia wa JMT anao, hata mimi na wewe tunao. Hata hivyo naomba kutoa angalizo kuwa watu wakaribishwe Bungeni kwa hoja zenye mashiko ambazo hata ikitokea tuseme wa-Tanzania wakahoji ukaribisho huo, kusiwe na kigugumizi katika kuzitaja sababu za ukaribisho wao Bungeni!
 
Kaka mshana Jr. samahani kama hutopenda maswali yangu.I hope you will take it positively.

Unahisi thread yako inamuweka katika mazingira gani uyo unayemzungumzia?

Hauoni kama unahatarisha maisha yake endapo uvumi huu ukienea kiasi cha kiwafikia maadui zake ,au washirika wake wakigundua amekua exposed endapo uyasemayo yakiwa ni ya kweli?
Kwenye uzi huu Mshana Jr hajasema chochote kipya ambacho mhusika hakutamani kijulikane na watu. Aliyoyaongea mhusika, ndiyo yale yale mleta uzi huu ameamua kuyanyumbulisha ili yaweze kueleweka kirahisi na watu wengi zaidi na wenye upeo tofauti tofauti. Kwa hiyo anachoongea hapa mleta uzi, ndiyo alichosema Dr. Shika ambaye wewe anakuweka kweye wasiwasi wa kumuona yuko hatarini. Wewe unamhurumia zaidi kuliko anavyoweza kujihurmia mwenyewe? Dr. Shika alikuwa na kitu alikuwa anataka kijulikane kwa umma, akawa anatafuta nafasi ambayo alijua kuwa kitajulikana na watu kwa kasi ya kipekee sana aliyoitamani, na ndiyo maana akaamua kwenda kufanya manunuzi hewa kwenye mnada wa Serikali. Hiyo akili peke yake tu pamoja na courage aliyotumia katika swala zima la mnada wa Lugumi, vinatosha kabisa hata kwa mtu layman kama mimi, kuni-convince kwa 100% kuwa huyu mtu ni agent, tena wa kimataifa!Na ndiyo maana hata baada ya hapo, hakupata matatizo yoyote yale. Jaribu wewe kufanya hivyo, kama si mmoja wao, bhalafu uone moto utakavyokuwakia!
 
mzee baba unaweza ku encrypt file then ukatuma tu. so mtu anaona umetuma email ila hawez jua umetuma nn ndani yake, ila kuna private internet ways zinatumika, yan natumia internet ya cafe ila nachange gateways napata private internet(VPN) then nafanya yangu.
Huwezi ukabadilisha Default Gateway au ku-assign IP Address kwenye workstation ya mtandao ambao hauna Administrative Rights nao. Much far, huwezi ukatengeneza VPN kwenye foreign network. Kama unasema unaweza, nipe technical details. Tusitake kudanganyana hapa
 
Na conclusion yangu ilikuwa very clear
Hiki kitendo pekee kilikuwa kinatosha kabisa kuwafanya watu wenye upeo waache kuendelea kuhoji uhalali wa maudhui ya uzi huu. Yaani mtu mwingine anataka mpaka asikie Dr. Shika mwenyewe anataja kuwa ni agent, wakati hata kwao huko Masaki wanaishi nao ma-agent kibao na hawajawahi kuwatamkia hayo, sasa ije iwe kwa Dr. Shika? Yaani mtu anakuwa hawezi kabisa ku-connect dots tu kutoka kwenye maongezi ya mtu husika?
NB: Nimeandika kwa muktadha wa mtazamo wangu kulingana na simulizi za mlengwa mwenyewe

Jr
 
Na conclusion yangu ilikuwa very clearNB: Nimeandika kwa muktadha wa mtazamo wangu kulingana na simulizi za mlengwa mwenyewe

Jr
Kwa umri wangu mdogo na kusoma Visa vingi sana katika vitabu mbali mbali na kuongeza na za Mbweni kidogo unaunganisha na za kaka mshana nachanganya na za mshikaji wangu muuza kahawa karibu na bustan moja pale hivi, ongeza na ujinga wangu kidogo, Tangu hii makala iandikwe hapa bado nina imani nayo na wala hakuna atakaenitolea kuiamini.

Wengi wetu humu tunakurupuka tu na akili za kula chips hatujui nini maana kukanwa na kukana na kufunga agano na kula kiapo,
Nakumbuka machozi yananitoka.

All in all kati ya watu elfu mia sita biblia imewataja kutoka Misri kwenda Kaanani walifika watu wawili tu wale walioianza safari toka Misri to Kaanani nae ni JOSHUA na KALEBU, namna gani waliamua kuwa waaminifu na kuzingatia kiapo chao hawakuogopa mateso wala dhiki ila wakatoboa ( Mungu nisaidie kuvuka)

Mshana God bless you brother nimekusoma na nilikusoma vema endelea kuamini unachokiamini
 
Kwa umri wangu mdogo na kusoma Visa vingi sana katika vitabu mbali mbali na kuongeza na za Mbweni kidogo unaunganisha na za kaka mshana nachanganya na za mshikaji wangu muuza kahawa karibu na bustan moja pale hivi, ongeza na ujinga wangu kidogo, Tangu hii makala iandikwe hapa bado nina imani nayo na wala hakuna atakaenitolea kuiamini.

Wengi wetu humu tunakurupuka tu na akili za kula chips hatujui nini maana kukanwa na kukana na kufunga agano na kula kiapo,
Nakumbuka machozi yananitoka.

All in all kati ya watu elfu mia sita biblia imewataja kutoka Misri kwenda Kaanani walifika watu wawili tu wale walioianza safari toka Misri to Kaanani nae ni JOSHUA na KALEBU, namna gani waliamua kuwa waaminifu na kuzingatia kiapo chao hawakuogopa mateso wala dhiki ila wakatoboa ( Mungu nisaidie kuvuka)

Mshana God bless you brother nimekusoma na nilikusoma vema endelea kuamini unachokiamini

Jr
 
Back
Top Bottom