Dkt. Louis Shika: Mgeni mualikwa mahafali ya chuo cha afya Kahama Shinyanga, atangaza neema

Avriel

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
4,947
5,342
WanaJamiiForums habari za mchana,

Yule Daktari bilionea maarufu nchini kwa sasa ameonekana wilayani Kahama akiwa ni mgeni maalumu katika uzinduzi wa chuo hicho ambao unafanyika leo..
Picha zaidi nitatupia .

img-20171123-wa0043-jpg.636240


img-20171123-wa0049-jpg.636241


img-20171123-wa0041-jpg.636243

shi1.jpg
shi2.jpg




Bilionea Dkt. Louis Shika ambaye amejizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania baada ya kuibuka katika mnada wa kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi ametua leo alhamisi Novemba 23, 2017 mjini Kahama kwenda kuhudhuria katika mahafali katika chuo cha Afya cha (Kahama College of Health Science).
dr. ss.jpg

Dkt. Louis Shika akiwa katika matukio ya upigaji picha na wahitimu chuoni hapo.

Dkt. Shika akitoa hotuba kwenye sherehe za mahafali mbele ya wahitimu amesema anatambua kuwa masomo ya sayansi hususani ya Afya karo yake ni ghali hivyo ameahidi kuwalipia karo wanafunzi wote watakaofanya vizuri kwenye masomo yao chuoni hapo.

“Natambua umuhimu wa masomo ya afya na ughari wa malipo yake kwa Watanzania wenye kipato cha chini, nitawalipia wanafunzi wote wenye uwezo darasani ambao wazazi au walezi wao hawana uwezo wa kugharamia masomo yao.“ amesema Dkt. Shika wakati akitoa hotuba yake kwenye mahafali chuoni hapo.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Chuo hicho, Yona Bakungile ameeleza sababu za kumualika Dkt. Shika katika Chuo chake kuwa ni kutokana na utaalamu wake wa masuala ya tiba ya binadamu na umaarufu wake unaoendelea kuvuma nchini.

“Chuo changu kinatoa mafunzo ya afya ya binadamu; licha ya umaarufu wake nchini kwa sasa, Dk Shika ni miongoni mwa wataalamu katika fani ya utabibu ndiyo maana nimemwalika. Naamini atawashauri na kuwapa hamasa wahitimu na wanafunzi wanaoendelea,” amesema Bakungile kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwananchi.

====

Kahama. Dk Louis Shika, ‘bilionea’ aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi, bado anaendeleza vituko; safari hii amesema hataki kufuatiliwa.

Dk Shika alijizolea umaarufu baada ya kuibuka kwenye mnada huo na kutaja viwango vya juu vya fedha kuwapiku watu wengine waliojaribu kununua nyumba hizo.

Lakini akashangaza baada ya kushindwa kulipia hata asilimia 25 ya takriban Sh3 bilioni ya nyumba tatu alizoshinda mnada licha ya kuahidi kuwa angefanya hivyo ndani ya muda mfupi kwa sababu fedha zake ziko nchini Urusi.

Kauli zake katika mnada huo, hasa ya "900 itapendeza", ndizo zilizompa umaarufu kiasi cha kupata udhamini wa kampuni tofauti, lakini bado hajaisha vituko.

Akiwa mjini Kahama mkoani Shinyanga jana Alhamisi (Novemba 23,2017) kuhudhuria mahafali ya Chuo cha Afya, msomi huyo wa Urusi aliahidi kukifadhili chuo hicho Sh2.2 bilioni kila mwaka.

Hata hivyo, mtaalamu huyo wa utabibu wa binadamu ameutahadharisha uongozi wa chuo hicho, akiutaka kutomfuatilia kudai kutimiza ahadi yake kwa kuwa anataka kuepuke mambo ya mnada wa nyumba kujirudia.

“Inapendeza tu mkiamini kwamba mtakuwa mnapokea kiasi hicho cha fedha (dola milioni moja), kila mwaka,” alisema Dk Shika.

Dk Shika pia aliwatahadharisha waandishi wa habari kutomuuliza kuhusu kutimiza ahadi hiyo ya dola milioni moja kwa chuo ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa kwa sababu hana fedha taslimu hadi mchakato aliosema wa kuhamisha fedha kutoka Urusi utakapokamilika.

Akizungumza na jumuiya ya chuo na wageni waalikwa, Dk Shika ametaja sababu ya kuahidi msaada huo kuwa ni kukiwezesha kutoa elimu bora ya utabibu na masuala ya afya ambayo ni muhimu kwa jamii na maendeleo ya Taifa.

Dk Shika aliwasili Kahama kwa ndege iliyotua uwanja wa ndege wa Buzwagi na kupokewa na mkuu wa chuo hicho, Yona Bakungile, huku msafara wake ukiwa na magari zaidi ya 50 yaliyopita mitaa mbalimbali kabla ya kufika chuoni.

Chuo hicho kipo Kata ya Mwendakulima umbali wa takriban kilomita tatu kutoka mji wa Kahama.

Dk Shika, mbele ya mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ya kwanza, alitoa ahadi hiyo baada ya Bakungile kuzungumzia changamoto ya baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo kutokana na wazazi na walezi kushindwa kuwalipia ada.

“Baadhi ya wanafunzi pia wamekatisha masomo kwa kukosa ada baada ya wazazi au walezi wao kufariki dunia,” alisema Bakungile.

Akizungumzia ahadi ya Sh2.2 bilioni kwa chuo chake kila mwaka, Bakungile alisema anaamini na "itapendeza akizipokea" kwa sababu zitasaidia kuinua kiwango cha taaluma na ubora wa miundombinu chuoni.


Chanzo: Mwananchi
 
Wanajamii forum habari za mchana,
Yule Daktari bilionea maarufu nchini kwa sasa ameonekana wilayani Kahama akiwa ni mgeni maalumu katika uzinduzi wa chuo hicho ambao unafanyika leo..
Picha zaidi nitatupia .
Mkuu...
Nilipitia hapo chuoni kwaajili ya kumsabahi kijana wangu, nikamuona pia Minard Ayo anapita huku na kule...
Nikikaa poa nitatupia picha zaidi....

SASISHA.....

Dr Shika ameanza kwa kukisifia chuo pamoja na majengo ikiwapo na madhari yenye kuvuti.....

Kwambaaaali namuona mkuu wa wilaya Kahama ameshika tama na mdomo wake umebaki wazi kabisaaaaaaaa.....

Dr Shika anashukuru kwa kupewa nafasi ya mualiko wa kuwa mgeni rasmi.
Kisha anaendelea kwa kuahidi kukiunganisha chuo na wafadhili ambao ni rafiki zake.

Dr Shika ameitosa rasmi LUGUMI kwa kusema hataki tena habari za lugumi. Na anaahidi kutumia fedha atakazo tumiwa kwa kusomesha watoto yatima na wasio jiweza.

Itaendelea......

IMG-20171123-WA0043.jpg
IMG-20171123-WA0049.jpg
IMG-20171123-WA0041.jpg
 
Back
Top Bottom