Dkt. Louis Shika aeleza Magumu aliyopitia hadi akatoroka Urusi. Alitekwa na kukatwa Vidole, Tanzania ilimtelekeza...

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,634
29,997
Kwanza tuanze na kukanyana kwa unafiki,
Inaonekana mzee Shika siyo mwendawazimu kama watu walivyosambaza ujumbe kwamba ni mbovu wa akili,

Wengine wakasema hana nyumba anadaiwa kodi, kumbe watanzania unafiki tutauacha lini?

MAELEZO YAKE NIMEYAWEKA KWA KIFUPI

Katika mahojiano na kituo kimoja ameeleza yafuatayo
1. Anadai ana nia bado ya kununua nyumba za Lugumi

2. Alitekwa nchini Russia na kuteswa na warusi kwa kutaka awape hela na kumkata vidole kama anavyoonesha kwenye video

3. Aliwekwa ndani ya andaki kwa siku 28 na vijana wahuni wa urusi bila majirani zake kujua alipo na kujua atapatikana wapi, baadae akatumia mbinu mbadala kuwatoroka baada ya wao kulewa sana,

4. Alipopelekwa hospitali alitembelewa na ubalozi wa marekani, lakini ubalozi wa Tanzania ulimtelekeza.

Hapa nakubaliana na Shika, huku Urusi kuishi kwa wasiwasi sana kwa kifupi SISI HUKU NI NYANI, NAITWA NYANI na incidence kama hii imenikuta nilipotembelea SARATOV mwaka 2016 nilihisi mazingira ya sintofahamu, Mpaka nilipo rudi kazini kwangu ST PETERSBERG.

Hebu pitia video yake, weka bando la kutosha upitie,


Dar es Salaam. Dk Louis Shika ‘bilionea’ aliyejitokeza kununua majumba ya kifahari ya mfanyabiashara maarufu Said Lugumi ameelezea siku 28 za mateso aliyodai kuyapata baada ya kutekwa nyara nchini Urusi miaka 13 iliyopita.

Dk Shika, ambaye jana aliachiwa kwa dhamana na polisi amesema haikuwa rahisi kujinasua kwa sababu alipata mateso makali na alijua ndiyo mwisho wa maisha yake, lakini kwa uhodari na nguvu za Mungu alifanikiwa kutoroka kutoka mikononi mwa watekaji hao.

Hata hivyo aliendelea kusisitiza kuwa mpango wake wa kununua nyumba za Lugumi haujabadilika na kwamba ataishangaza dunia.

Alisema hayo jana jioni katika mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake Tabata Mawenzi baada ya kurejea kutoka mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi alikoshikiliwa kwa siku sita akituhumiwa kuvuruga mnada huku leo akitakiwa kuripoti kituoni hapo saa tatu asubuhi.

Dk Shika, ambaye alidai kuwa alikwenda Urusi kwa masomo na baadaye kufanya kazi nchini humo alisimulia kuwa alitekwa na watu wasiojulikana Juni mwaka 2004 huku ‘watekaji’ wakimtaka awape Dola1.5 milioni za Marekani (Sh3 bilioni kwa sasa) ambazo hakuwa tayari kuzitoa licha ya kuwa na uwezo wa kuwapa.

“Nilipokamatwa walinipeleka sehemu huku nikipigwa, nikiteswa kwa siku 28 na nilijua ndio itakuwa kifo changu. Nilipigwa ngumi, niliteswa vikali, walitumia nyaya za umeme kunitesa, walinikata vidole kimoja kwa nyundo na viwili kwa panga, yote wakitaka niwape dola milioni moja na nusu,” alisema Dk Shika, ambaye mwandishi wa habari hizi alishuhudia kuona mkono wake wa kushoto ukiwa umekatwa vidole viwili na kidole kimoja mkono wa kulia.

“Sikuwa tayari kutoa, uwezo huo nilikuwa nao, siku 28 zilikuwa ngumu kwani chakula nilikula kile ambacho walibakiza wao, mwili wangu ulijaa damu, wale Warusi walinitesa sana kwani hata sikio langu (la kushoto, anamuonyesha mwandishi) limebondwabondwa, ni tofauti na hili la kulia hadi nafika Tanzania ni Mungu pekee anajua.”

Dk Shika alisema mateso hayo yalimsababishia maumivu makali ikiwamo kuvunjika mbavu tatu upande wa kulia na mbili kushoto ambazo bado hazijaunga vizuri.

Aliuhusisha mkakati wa kumteka na mmoja wa wafanyakazi katika kampuni yake aliyodai inaitwa Ralcefort ili kujipatia kiasi hicho cha fedha, lakini hawakufanikiwa baada ya kuwazidi ujanja na kutoroka.

Mwananchi lilipotaka kujua alitumia mbinu gani kutoroka ikiwa alikuwa hana nguvu na ndani ya jumba asiloweza kujua mlango ulipo, Dk Shika alidai, “ilikuwa siku moja wale watu walitoka na kumwacha mwenzao, akaanza kunywa pombe aina ya vodka na kujidunga unga, mimi nilipoona hivyo wakati huo nimefungiwa katika pipa la maji nilianza kufikiria mbinu za kumtoka.”

“Nilimhesabia tu muda, kuna muda ulifika nikamwona amelala na kwa kawaida mtu akilala ukimwangalia usoni anaweza kuamka, kwa hiyo mimi nikalibinua lile pipa na nikatoka, kule nje nilipotoka nilikutana na binti ambaye hakunisaidia.”

Dk Shika, ambaye huongea kwa kujiamini alisema baada ya kutoroka alipata msaada kutoka kwa wasamaria wema ambao walimchukua na kumpatia huduma ya kwanza wakati huo mwili wake ukiwa umeloa damu.

Alisema watu waliomsaidia walitaka awapeleke eneo alipotekwa, lakini siku ya kwanza hawakufanikiwa kwa sababu alikuwa hapajui vizuri ila siku ya pili walifanikiwa kupaona.

“Tulipofika mle ndani tulikuta damu imetapakaa chumba chote, kumbe wale watu walimuua yule mwenzao niliyemtoroka baada ya kudhani nilimpa fedha ili aniachie, wakadhani amewasaliti.

Kuhusu familia yake kumtenga kama alivyosema kaka yake anayeitwa Pelanya Lunyalula (84), katika mahojiano na Mwananchi, Dk Shika alisema, “mawasiliano mabaya, kama hatuwasiliani ni ukosefu wa mawasiliano, yawezekana mwenzangu akawa hana simu, sasa tutawasilianaje na sidhani kama nitakwenda (Simiyu) kwani kama wazazi wamekufa hata nikienda haitasaidia. Sasa ninachokiangalia ni kumaliza kwanza hili la kuzipata nyumba zangu.”

“Siku nikipeleka fedha nataka Yono (Kampuni ya Udalali iliyoendesha mnada huo) na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) waite waandishi wa habari waone na wautangazie umma,” alisema kwa kujiamini.

Polisi wamwachia kwa dhamana

Awali, kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alilieleza Mwananchi kuwa wamemwachia Dk Shika kwa kujidhamini mwenyewe baada ya kukosa mtu wa kumdhamini ila atakuwa akiripoti kila siku saa tatu asubuhi.

“Uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea, lakini mpaka sasa hakuna mtu aliyefika kutaka kumuwekea dhamana, anaishi kama mtu wa nyikani. Nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana ajidhamini yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti kila siku,” alisema.

Njiani wakati akielekea kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja baada ya kuachiwa na polisi, Dk Shika alikuwa kivutio kwa watu aliokuwa akipishana nao.

Hata allipopanda daladala la kwenda Tabata Mawenzi, kondakta alimkaribisha kwa kumweleza, “karibu mzee Shika”, huku ndani ya gari hilo watu wakipiga naye picha na alipowasili nyumbani kwake aligonga geti na kujitambulisha “choka mbaya bin mlalahoi” jambo lililowafurahisha waliojitokeza kumpokea.

Chanzo: Mwananchi
 
Kinachonifanya nizidi kumkubali huyu mzee. AMESIMAMIA MSIMAMO WAKE ULE ULE. anataka anunue nyumba za lugumi.
Mzee peace Sana. Na ushirikiano anatoa kwa waandishi.
Nimecheka pale getini alipokuwa anahojia alipomaliza akasema. Haya Asanteni.
 
Kuna mtu mmoja wa internet Cafe alisema Dr Luis alikuwa anakwenda sana kiufupi maelezo ya pesa aliyoyatoa yanaonyesha amekutana na matapeli wa mtandao ambao wanaweza kukwambia umeshida pesa kibao namna hile ya usafirishaji aliosema wa kulipia bima pesa niya kutapela badala ya money transfer cost ambayo wanaweza kukata kwenye pesa yako bila kutuma chochote, hivyo kwa hatua hii inahitaji mjadala mpana wa kusaidia watu wasiojua kadhia hiyo
 
watanzania wengi wanaoenda urusi huishia kuvurugikiwa akili.

Nawafahamu zaidi yA watatu. Sijui kuna jambo gani (japo kuna exception ya wazanzibar)
He he hee,
Kuna mwalim wangu toka Tanganyika alienda intake moja na Shein,mwl alikuwa mtaalam wa namba na shein masuala ya sayansi,wote walikuwa vizur sana upstairs,ajabu yule mwl wangu alikuwa ni mlevi MBWA its like mwehu,ila shein yupo POWA.
 
Back
Top Bottom