Profesa Kitila Mkumbo, wewe ni Waziri jadili hoja za Wizara uliyokabidhiwa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nimefuatilia mahojiano ITV Kati ya mtangazaji na Dr. Kitilla Mkumbo kuhusu hoja mbalimbali.

Kwa ngazi yake ya elimu na hoja alizotoa unaona namna elimu ya Phd isivyo na umuhimu hasa kwa mwanasiasa.

Leo Kitila Mkumbo aliyekosa ushawishi kwa Wana ubungo anatuaminisha upinzani imepoteza imani kwa wananchi?

Kwamba yeye huko aliko anaona anapendwa na wanapendwa?

Naomba nimkumbushe kwamba siku zote mate utemwa chini na hata yakitemwa kuelekea juu yatarudi chini tu.

Upinzani siyo chama Tena Bali ni imani ya watu hivyo hata ufanye mazuri mengi kiasi gani bado unahitaji dola kusalia madarakani na si wananchi. Hakuna mwananchi mwenye imani na chama Tawala Duniani, watu wanatamani kuona mifumo mipya kila wakati.

Watu wanataka haki ya kuishtakiwa iwe kwa wote kwa dhana kwamba hakuna binadamu aliye juu ya sheria. Nani atakuwa na amani na mtu mwenye mamlaka yakushtaki lakini yeye ashtskiwi?

Mgabe alipoondoka ikulu ndipo alipojua kwamba hakuna mzimbabwe aliyekuwa na kiu yakumwona akiwa anatawala ila awali akiwa madarakani kila mtu alionekana kuwa mfuasi wake. Alipopinduliwa hata Mawaziri na wasaidizi wake awakumsapoti walikaa pembeni.

Kwa mfano huu nataka kumsaidia Dr. Mkumbo kwamba ulimwengu huu wa sasa hakuna uwekezaji unaofanywa kwa kupenda mtu au chama cha siasa Bali uwekezaji upo kwenye mabadiliko.

Na tafsiri ya mabadiliko haiwezi kuletwa na chama Bali mabadiliko ni itajio la kila siku likihusishwa na dhana ya endles needs.

Ajikite kwenye nafasi ya Waziri na majukumu yake, habari za siasa za vyama awaachie kina polepole. Unapopewa muda wakuzungumza Kama Waziri jikite kwenye hoja zakiwizara maana muda ni mchache na matatizo ni mengi.
 
Kitila nimempuuza sana! Yaani anapewa muda wa kuongelea mikakati ya wizara anaanza kuongelea CHADEMA? Yaani alipofika hapo tu nikahama channel! Ukweli wenyewe anajua kwamba CHADEMA iko ndani ya mioyo ya Watanzania, hata ubunge alionao hakushinda!
Yupo humu Kitila Mkumbo
Kiufupi alishafeli kabla ya yote.
Waziri wa uwekezaji unaenda kuwa kuwachamba chadema kwenye Tv?

Yaani unatuonaje watz?

Kila mtu aliona mlivyokwapua kura.

Bora ajikite kwenye uwekezaji ambao haupo na hakuna mwekezaji atakayekuja manji mwenyewe kakimbia
 

Attachments

  • IMG-20210302-WA0000.jpg
    IMG-20210302-WA0000.jpg
    78.4 KB · Views: 1
Yupo humu Kitila Mkumbo
Kiufupi alishafeli kabla ya yote.
Waziri wa uwekezaji unaenda kuwa kuwachamba chadema kwenye Tv?

Yaani unatuonaje watz?

Kila mtu aliona mlivyokwapua kura.

Bora ajikite kwenye uwekezaji ambao haupo na hakuna mwekezaji atakayekuja manji mwenyewe kakimbia
Yaani hata mie nilikaa mkao wa kusikiliza, mikakati aliyonayo, kama msomi kuleta uwekezaji ili kuharakisha maendeleo, but nikaona analeta tena mambo ya siasa..... nikaishia kusema kimoyomoyo..hiiiiiii kazi kwelikweli!!
 
Mbona hata hayo yanayoihusu hiyo Wizara yake na Changamoto zake aliyasema? au Kuisema CHADEMA na Changamoto zao Kwako ni Kosa sana?
 
Kitila nimempuuza sana! Yaani anapewa muda wa kuongelea mikakati ya wizara anaanza kuongelea CHADEMA? Yaani alipofika hapo tu nikahama channel! Ukweli wenyewe anajua kwamba CHADEMA iko ndani ya mioyo ya Watanzania, hata ubunge alionao hakushinda!
Swali la kujiuliza upinzani ni CHADEMA pekee? yaani tuna watawala wa hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom