My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,283
Kwa mara ya tatu tena nakuandikia Mzee wangu Dr Modestus Kipilimba, mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa, TISS.
Natamani sana, Rais Magufuli awe wa kwanza kusoma hii mada kabla yako.
Nimeshindwa kuendelea na kazi niliyokuwa naifanya usiku huu kwenye Computer, moyo wangu umekosa amani kabisa hadi niandike hii mada.
Dr. Kipilimba, unadhani bado unastahili kuongoza Idara nyeti na muhimu Kama hii ya TISS?
Kwanini mikononi mwako serikali ya awamu ya tano inadhalilika sana kimataifa?
Kwanini Idara yako imeruhusu uwepo wa watu Kama Musiba wanaokashifu viongozi wakubwa hadharani?
Sikufundishi kazi, ila nashangaa kwanini hujui kuwa idara kama TISS ndo Roho kamili ya Tanzania.
Kifo cha TISS ni kifo cha Tanzania, kwanini hujifunzi magumashi ya CIA, MI5, Mossad na mashirika mengineyo kama TISS?
Ninaposema magumashi nadhani umeelewa vizuri kabisa, maana nikielezea itahitaji kitabu.
Uimara wa TISS ndo Uimara wa Tanzania, na udhaifu wa TISS ndo udhaifu wa Tanzania.
Tunajua ya kwamba dawa ya Deni ni kulipa, lakini ilikuwaje TISS ikashindwa kubaini kuwa Steyn kafungua shauri mahakamani dhidi ya Tanzania kudai mali yoyote ya nchi ikamatwe?
TISS ingeitaarifu serikali basi, ndege isingeenda SA, na hivyo wangetafuta namna nyingine ya ku-solve tatizo.
Ni aibu kubwa mno nchi kudaiwa na raia mmoja Halafu mali ya nchi kukamatwa kwa Deni nje ya nchi, hii fedheha kubwa.
TISS mngeweza kuepusha hii fedheha. Kama TISS, ilishindwa kubaini njama za kutaifisha mali ya nchi, je itaweza kujua nini kinapangwa Somalia na Alshabab kwa mfano juu ya nchi?
Dr Kipilimba, TISS chini yako ni dhaifu mno, nakushauri u resign tu. TISS chini ya Dr Hansy Kitine na hayati Imran Kombe ilikuwa imara kupindukia.
Nakumbuka Tukio moja (siwezi kulitaja) nilikuja kushtuka mission accomplished muda mrefu kumbe yule jamaa alikuwa TISS na akapotea kama jini.
TISS ya leo imejaa vijana wa UVCCM, wasiojua lolote kuhusu intelligence wala miiko yake. Idara hii imegeuzwa kuwa ya kisiasa ili CCM itimize ndoto zake za alinacha za kutawala milele. Inashangaza sana, yaani Idara haikuweza hata kuzuia maandamano ya kuharibu Diplomasia yetu na SA.
Watumishi wa Idara hii wanatakiwa wawe wafia nchi (wazalendo kweli kweli) siyo wafia CCM au CHADEMA.
CCM itakufa, CHADEMA itakufa, lakiniTanzania ipo tu!