Dkt. Kimei(CRDB): Hali ya uchumi nchini ni tete

Status
Not open for further replies.
Tuogope kusema ukweli kuhusu Dr Kimei kustahili kutumbuliwa kwa kutaka kumchelewesha na kumkwamisha Mungu wa Ikulu ? Usiogope kusema kweli Mkuu msema kweli siku zote ni mpenzi wa Mungu, yule Mungu wa ukweli siyo huyu Mungu wa Ikulu anayependa kudanganywa danganywa na pia ni mpenda sifa sana.
Jamaa ana sifa hadi kero yani mie ananikeraga yule
 
Sidhani kama Dr Kimei kafanya conclusion na hata debate hii is not concluding either, nnachoelewa ni kwamba ame trigger economic trend ya nchi kwa sasa basing on area yake ya specialization, hivyo ni vizuri ku expand horizon kwa kuangalia status kwenye aspects nyingine za uchumi nchini mwetu.

Ku react negatively kwenye finding ya mtu bila kujiahughulisha kuja na alternative findings nadhani it's not healthy.
You are absolutely right....kimei alicho sema ni kwamba ana angalia mwelekeo wa uchumi una elekea wapi. Kama CEO, hawezi kuwekeza kwenye sector au biashara ambayo haina mwelekeo kwa sasa. Kazi yake ni kuwekeza mahali penye faida kwa shareholders. Kama kwenye Gas na hotels kwa sasa hivi ni neutral, hakuna mwelekeo, haoni sababu ya kuwekeza kwenye hizi sectors Mpaka hapo Zitakapo toa muelekeo.
 
Clever people are supposed to foresee future outcome it is the essence policy planning and risk management, Kimei is not a government economic planner. Haya madhara yako kila mahala tells you something kuhusu wataalamu wa serikari.
Kwani Tanzania haina policies?
 
Ndiyo tatizo la watu wanaodhani wao ndio wao
"Sitaki mtu anicheleweshe wale anikwamishe"
Ufahamu wako wa mambo ya uchumi ni SIFURI ndiyo sababu kuna washauri wa kukupa ushauri nini kifanyike ili kukuza uchumi bila kuathiri wananchi sasa leo unakurupuka na mwendo kasi wako na kuwaathiri wananchi na huku uchumi ukiendelea kuwa DORO.

Jamaa ana sifa hadi kero yani mie ananikeraga yule
 
Eeeh.. Kimei amesha maliza na concluded... ** HALI YA UCHUMI NI TETE** unataka conclusion gani tena.. ndio maana tunapinga.. sbb kahitimisha hivyo..!!

Wee unasema haja conclude..!! Ndio kamaliza, kuwa HALI YA UCHUMI ni TETE..!! That is why we are negating and brainstorming here.. i.e he is only correct probably by 25% only.. sio zaidi ya hapo.. banking alone huwezi kuhitimisha kama Kimei alivyofanya.. nimekupa mfano, kama ni paper utafeli..!!
You are rating correctly if you conquer Kimei's conclusion at 25% hence the stepping stone for further country economic analysis!
 
kweli watanzania IQ zero Kisa kimei amesema ukweli eti mnaanza kusema kakaa miaka mingi imefikia wakati aondoke,mara walizoea pesa za dezo za serikali,mara walipata dili la mishahara ya watumishi kupitia serikali huku wakiwa hawana mtandao mpana wa mabenki.kweli hii nchi inahitaji zaidi ya maombi yaani LUMUMBA ukweli wao ni kama kuwachoma kisu cha moyo
 



Dk. Charles Kimei

BENKI ya CRDB imesema imepunguza kasi ya utoaji mikopo kuangalia hali ya uchumi nchini inavyokwenda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, alisema kwa sasa beni hiyo inaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo wa kukopesheka.

“Kipindi hiki ni cha mpito bado watu hawajatulia, tunaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo kwa sababu kama hoteli zinayumbayumba lazima tusubiri hali ikae vizuri.

“Sisi tunasimamia fedha za watu hivyo hatuwezi kucheza nazo, tunazidi kujipanga kufuatana na sera ya Serikali,” alisema Dk. Kimei.

Akitoa mfano, alisema sekta za mafuta na gesi ni kama vile zimesimama hivyo CRDB inasubiri hali ikae vizuri iweze kufanya tathmini.

“Mikopo mingine kama ya watu binafsi tunaendelea kuitoa na kama ni waajiriwa waje watapewa lakini katika sekta nyingine hali imekuwa tete sana,” alisema.

Serikali ilieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya vipaumbele yatakayozingatiwa kama yalivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 ni pamoja na kuendeleza huduma za fedha, biashara na masoko.

Hata hivyo, hatua ya Serikali kutangaza mkakati wa kupunguza na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima imeanza kuathiri sekta nyingi ikiwamo ya fedha.

Licha ya mkakati wa kubana matumizi, pia Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika ada ambazo benki inatoza wateja wake kwenye huduma mbalimbali zinazotolewa ni miongoni mwa vitu vilivyochangia mtikisiko huo.

Wakati akisoma bajeti ya serikali bungeni kwa mwaka 2016/17, Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, alisema serikali inakusudia kutoza VAT katika huduma za benki zinazotozwa na benki zote nchini ili kupanua wigo wa kodi.

Chanzo: Mtanzania




Hii hoja kwa taarifa za kiintelejensia za policcm inaweza kuwa na kiwango kikubwa sana cha uchochezi,hili ni jaribu la dhahiri kabisa kwa "baba mtakatifu wetu" ambaye alishasema kuwa hajaribiwi.
 
Wee Kimei kaongea kivyake...

Nia yake ilikuwa hiyo VAT.. aache kuitisha watu na serikali..!! Unamjua Kimei ww..? Sisi tunamjua sana..

Kutamka hali ya UCHUMI TETE kwa kuangalia banks tu ni kosa kubwa.. hasa benki ya CRBD tu... Uchumi kuwa tete sio swala la single indicator... acha short sightness ya mambo
swala si kumjua kimei bali kitu alichikiongelea,kwa nchi kama Tanzania mabenk ni indicator kubwa sana ya uchumi wa Tanzania
 
we utakuwa un
Mzee Kimei kwanini husemi ukweli.................
Unawatisha wa Tz wakati unajuwa kileCRDB manakifanya kwa miaka yote na serikali ikawa kimya Bot wakawa kimya maisha yakaendelea, binafsi nalijuwa ikija serikali inafuwata taratibu za fedha nakuyabana ma bank na mcheo wao wakufanya mchezo na pesa za serikali yapo mabank yatatangazwa mufilisi hii ni dalili ya mawingu ila mvua bado.....
nilazima ukweli tutaujuwa watanzania........
tujiulize kama hali ya uchumi ni mbaya mbona yapo ma bank yanapika mzigo kama kawaida wala hawalalamiki?
Kama hali ni mbaya mbona NMB plc pamoja nakufanyiwa fitina zote na crdb kunyakang'anywa mishahara ya watumishi na akaunti za serikali badoi shear yao inapaa wakati ya mzee kimei inashika mkia kila kukicha?
I love mothermatics because ye can't fool mathermatics even if ye have good iq
we uatakuwa unaishi rwanda unasema mabenki mengine hali ni nzuri???
 
achan
Hii tafiti ya coverage ya mtandao wa matawi ya CRDB mliifanya lini na mbona hamtupi takwimu sahihi kwamba haijafika wapi?

Benk yenye mpaka mawakala vichochoroni mnasema haina mtandao mkubwa kweli?!

Watu wa banking and finance njoo mtusaidie kitaalamu hapa please!
e nae huyo hajitambui hivi kuna wilaya gani hapa Tz CRDB haipo
 
kwa sisi wanauchumi kipindi hiki cha magu watu wenye uhafadhali watakuwa wafanyakazi ila kwa wafanyabiashara na wajasiliamali waandike maumivu
 
Ukifatilia kwa umakini kuna kitu utangundua wote hawa wanaolia halo ngumu hata Kimei mwenyewe walizoea bwelele,yaani wote waliokuwa wanafanya biashara na serikali tena za ujanjaujanja ndio wanaolia tazama mahoteli yaani siwabunifu kabisa kufanya biashara na watu wengine,hawajuikutafuta masoko hata wasomi kama Kimei eti nae analia.
hizi kauli za kuwa walizoea bwelele zinatakiwa zitumiwe na watu wasiokuwa na uelewa wa mambo si ww ambaye unashinda mitandaani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom