SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt. Charles Stephen Kimei akizungumza na Azam TV ameeleza umuhimu wa serikali kuanzisha mfuko maalum wa kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wa kati kwa mikopo ya masharti nafuu, riba ndogo na ujuzi katika kuendesha na kusimamia biashara zao au kuziongezea thamani.
Anasema biashara ndogondogo na zile za kati zimeajiri idadi kubwa ya watu wanaojipatia kipato, wanachangia mapambano ya kuondoa umaskini na hata maendeleo ya nchi.
Amesema duniani leo asilimia karibu 80 ya ajira katika mataifa mbalimbali zinatokana na biashara hizi.
Amesisitiza kwa kasi hii ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua kama mchumi kwa kutaka ustawi kwenye uwekezaji na biashara mfuko huu utamuandikia historia ya kipekee.
Kazi Iendelee.