singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Mwenyekiti wa CCM taifa, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ametangaza rasmi kwamba sherehe za maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 39 toka kianzishwe zinazofanyika kitaifa leo Singida zitakuwa za mwisho kwake kuwa mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini.
Bila kutoa ufafanuzi zaidi,Dkt. Kikwete ambaye alikuwa ameongozana na mke wake mama Salma, alisema anafuraha mno kuwa alianza kazi ya kuitumikia CCM kwa mara ya kwanza hapa mjini Singida Aprili 1975,na anamalizia Singida mjini Februari sita mwaka huu.
Dkt. Kikwete ambaye ni rais mstaafu wa awamu ya nne,aliyasema hayo jana jioni wakati akizungumza na baraza la wazee la Manispaa ya Singida kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini hapa.
Aidha,mwenyekiti huyo alilishukuru baraza la wazee Manisaa ya Singida kwa juhudi zao kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu uliopita.
“Mkutano mkuu uliopita, ulijaa changamoto nyingi na kwa kifupi,ulikuwa mgumu mno.Bila busara zenu ninyi wazee,kwa sasa pengine tugekuwa tunazungumza hadithi nyingine, mmefanya kazi kubwa,msichoke endeleeni kukitetea chama chenu ili amani na utulivu uendelee kudumishwa,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa miaka yote mkoa wa Singida umeendelea kuwa ngome imara ya CCM, kwa hali hiyo,amelitaka baraza la wazee wasiache sifa hiyo ikapotea.
Kwa upande wa serikali ya Dkt.Magufuli, alisema yeye anaiunga mkono na kuitakia kila la kheri katika kuwatumikia wananchi.
“Niwaombe na ninyi wazee na wakazi wote wa mkoa wa Singida, muiunge mkono serikali hii ya awamu ya tano imeonyesha dalili nzuri katika kutekeleza majukumu yake mkiacha kuiunga mkono, mtaikatisha tamaa kwa hali hiyo, itashindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo,” alisema Dk.Kikwete.
Wakati huo huo, serikali ya rais Dk.Magufuli inatajiwa kuhamia Singida mjini kwa siku nzima ya leo kushiiki sheehe za maadhimisho ya kitaifa CCM kutimiza miaka 39 toka kianzishwe.
Kwenye sheehe hizo ,akamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Wazii Mkuu Mhe. Majaliwa Kasimu Majaliwa, mawaziri, manaibu waziri na wabunge wa CCM wanatarajiwa kuwepo.