Dkt. Kigwangalla: Uchumi wa dunia utakua kwa kasi baada ya COVID-19 kudhibitiwa, tuchangamkie CHANJO sasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
44,329
2,000
Mbunge wa Nzega vijijini Khamis Kigwangalla amesema utafiti unaonyesha uchumi wa dunia utagrow kwa kasi mara tu baada ya COVID-19 kudhibitiwa.

Tanzania siyo kisiwa hivyo tuungane na dunia katika mapambano na tuanze utaratibu wa kufuatilia Chanjo sasa ili tusiachwe nyuma, amesema Dr Kigwangalla ambaye kitaaluma ni daktari wa binadamu

Kazi Iendelee!
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
22,767
2,000
Kigwangala akiwa waziri wa maliasili na utalii kupitia Twitter alitweet kwamba Kujifukiza ni tiba na kinga ya covid 19 na atashawishi hoteli zote za kitalii kutenga eneo la kujifukiza

Akaenda mbali zaidi na kusema inatakiwa tuuze huo ugunduzi wetu.

Ndani ya mwezi baada ya Magufuli kufariki akasema Mashine ya Kujifukiza Mhimbili ivunjwe. Tukiwa tunataka kumaliza mwezi wa pili anasema tuchangamkie chanjo.

Somo ninalolipata ni kwamba ukipata chansi ya kua mnafiki na unatengeneza zaidi ya 11M kwa mwezi we kua mnafiki tu
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,037
2,000
Akawaombe radhi kwanza wale askari wanyama pori aliokuwa anawaambia 'mzaha au sio mzaha' huku anawakung'uta push ups
 

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,231
2,000
Hatuhitaji chanjo!! Waliochanjwa haikuwasaidia!! Sisi Mungu ametukinga mwenyewe!! Bila kinga ya Mungu hali ingekuwa mbaya sana! Utukufu ubaki kwa Mungu na siyo kuupunguza na kuigawia chanjo kiasi.

Hivi mnaona Tanzania hatujapata shida kubwa kwenye wimbi la pili si bure, ni Mungu ametukinga. Kama Taifa tumepona, kama mtu binafsi inategemea kama unaamini uponyaji wa Mungu kwa nchi yetu! Ukiamini unabaki salama na mzima, kama hauamini corona inakuhusu!! maana umeikuza juu ya Mungu aliye hai.
 

tzkwanza

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,577
2,000
Kigwangala akiwa waziri wa maliasili na utalii kupitia Twitter alitweet kwamba Kujifukiza ni tiba na kinga ya covid 19 na atashawishi hoteli zote za kitalii kutenga eneo la kujifukiza

Akaenda mbali zaidi na kusema inatakiwa tuuze huo ugunduzi wetu.

Ndani ya mwezi baada ya Magufuli kufariki akasema Mashine ya Kujifukiza Mhimbili ivunjwe. Tukiwa tunataka kumaliza mwezi wa pili anasema tuchangamkie chanjo.

Somo ninalolipata ni kwamba ukipata chansi ya kua mnafikia na unatengeneza zaidi ya 11M kwa mwezi we kua mnafiki tu
Mshahara wa ubunge milioni 11+uwaziri milioni 9+posho na safari za uwaziri milioni 10=30 milioni ndani ya mwezi mmoja.

Hapo hata Mwendazake angesema bong'oka apige kimoko watu wangebong'oka tu.
 

tathmini

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
277
250
Hatuhitaji chanjo!! Waliochanjwa haikuwasaidia!! Sisi Mungu ametukinga mwenyewe!! Bila kinga ya Mungu hali ingekuwa mbaya sana! Utukufu ubaki kwa Mungu na siyo kuupunguza na kuigawia chanjo kiasi. Hivi mnaona Tanzania hatujapata shida kubwa kwenye wimbi la pili si bure, ni Mungu ametukinga. Kama Taifa tumepona, kama mtu binafsi inategemea kama unaamini uponyaji wa Mungu kwa nchi yetu! Ukiamini unabaki salama na mzima, kama hauamini corona inakuhusu!! maana umeikuza juu ya Mungu aliye hai.
Naheshimu kauli yako. Kwa heshima na taadhima nakuombea urudi mwaka 1940, au hata wakati wa Musa akiwaongoza Wayahudi jangwani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom