Dkt. Kigwangalla: Rais Samia anaendelea mpaka mwaka 2030, watakaompinga kukiona

Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,347
2,000
Wameanza Tena?

Hawajifunzi tu hawa watu dah mwanasiasa sio mtu wa kumuamin akifa ghafla wataanza kumzodoa mama akina gambo Sasa wanatapika tu madudu ya mwendazake

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Poti hiyo mwendazake jana nimesoma mahali huenda likaja kuwa kosa kutamka. Utahama Peramiho hadi kule maporini alikojenga mwamba mmoja akiitwa aidan - Litigation ndani huko(mkulima maarufu aliyependa kesi)
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,859
2,000
Mbunge wa Nzega vijijini Dkt Hamis Kigwangalla leo wakati anachangia hotuba ya bajeti kuu ya serikali amesema rais Samia anatakiwa kupita bila kupingwa mwaka 2025 ili aendelee mpaka 2030.

Kigwangalla amesema atakayejaribu kumpinga ndani ya ccm na hata nje atakiona cha mtema kuni hasa ikizingatiwa kuwa Chadema walishatangaza kuwa hawatashiriki uchaguzi mkuu wa 2025 hivyo Lisu kuendelea kulelewa Ubelgiji.

View attachment 1818634
huyu anaanza kumletea uchuro rais samia kama wengine walivyomletea uchuro Magufuli kuwa aoingezewa zaidi ya kipindi cha kikatiba.

Najua anatafuta attention tu lakini anasahahu kuwa alikuwa waziri wa Magufuli, ambao ndio sasa hivi mama anawapangua mmoja mmoja kuweka wake. Serikali yetu siyo taasisi inayojiegemea bali ni mali ya rais!
 

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
4,125
2,000
huyu anaanza kumletea uchuro rais samia kama wengine walivyomletea uchuro Magufuli kuwa aoingezewa zaidi ya kipindi cha kikatiba.

Najua anatafuta attention tu lakini anasahahu kuwa alikuwa waziri wa Magufuli, ambao ndio sasa hivi mama anawapangua mmoja mmoja kuweka wake. Serikali yetu siyo taasisi inayojiegemea bali ni mali ya rais!
Amempangua nani?
 

Nsimbinso

JF-Expert Member
Dec 15, 2020
402
500
Kuna story moja ya mama na baba 'ku-du' mbele ya watoto mpaka wakamuangusha mtoto aliyekuwa kalala nao chini... Wakastop mtoto akarudi kulala kitandani... Baadaye wakaanza tena... Kaka mtu ambaye naye ni mdogo akamwambia dogo lake... "Wameanza Tena"

Nimelazimika kutumia mfano huu wa aibu kuonyesha ni kwa namna gani hawa wapuuzi wanatia aibu na kinyaa... Wanajipendekeza kinafiki mpka inatia ukakasi kuwasikiliza...

Hawa ndo waliotaka Magufuli atawale milele... Hawa ndo walilamba si tu nyayo za JPM ila pia footprints alizoacha dakika kadhaa zilizopita... Hawa ndo waliimba na kucheza mapambio yote kumtukuza JPM... Wapo waliothubutu kukatika viuno hadharani wakiimba Magufuli jembe si jembe... Wapo waliosifu na ku-push kila kilichosemwa na JPM... Ghafla Mwenyezi Mungu mwenye mamlaka kamili kafanya yake wakageuza masifu waliyompa JPM kuwa matope... Mifano ni mingi...

Bila aibu, tayari wanaanza kudemka na kuanza kutafuta wapi waanzie kujikomba kwa bi mkubwa.

Hakika huu ni udhalilishaji mkubwa sana wa muhimili wa bunge... Bunge limekuwa kama kikundi cha wapiga ramli tu kwa mambo wanayoshadadia... Bila shaka hii ni moja ya sababu ya Bi Mkubwa kuwapa za uso kuwa waache kudemka... Akaenda mbali zaidi kuwa mengi ya yanayojadiliwa humo si kwa manufaa ya taifa, bali ni kwa ajili ya kuganga maslahi binafsi...

CAG aliyepita aliwahi pia kufananisha tabia hii na 'udhaifu'... nao wakaonyesha udhaifu kwa kupambana na mtoa kauli badala ya kupambana na kauli husika...

Huu pia ni udhalilishwaji mkubwa wa wasomi wenye hadhi ya Dr. Kama wasomi wetu ndo hawa, Msukuma yupo sahihi kabisa kuwashambulia Kama anavoonekana kufanya mara kwa mara...

Pole Tanzania, pole watanzania... Tuombee sana nchi yetu Mungu atunusuru na hili janga la aibu za kufa mtu tunazozishuhudia miongoni mwa hawa wanasiasa wa hovyo kabisa.
 

Theodora

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
761
500
Yaani Madame President ameingia historia ya TZ kama Makamu wa Rais wa 1 na Rais wa kwanza mwanamke.

Sasa - Kigwa anataka amuongeze kwenye historia kama Rais mwanamke wa 1 wa TZ aliyekuwa kwenye utawala na Umri mkubwa maana hadi 2030 atakuwa 70. Akimbizane na Alhaj Mwinyi... SAFI SANA.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,680
2,000
Hiyo mimba ya mwendazake unajifungua lini?
ha ha ha, kijana naona unaumia sana tukisema Mwendazake eee!!! sasa washauri CCM waache tabia za kupamba viongozi ili wapate teuzi - muda huu si wa kujipamba pamba muda huu ni wa kuwapa watanzania matumaini mapya baada ya kuwa katika hali ngumu ya maisha kwa kipindi kirefu - Sidhani hata Mama Samia anapenda hiyo tabia ya kumpamba pamba...

Muonyeni huyo kijana wenu atulie - kama kazi alipewa lakini yeye akawa anashinda mitandaoni kupiga majungu sasa leo anataka nini tena.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom