Dkt Kigwangalla: Nchi haiwezi kuwa ya watu wanaodhani watatajirika kwa bahati nasibu

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
Habari,,,,,

Ni ndugu EVARIST CHAHALI,swali kwa Dr kigwangalla kwenye twitter.

Majuzi nilitoa angalizo kwa Dkt @HKigwangalla kuwa wakimaliza kukamata mashoga, wageukie janga la kubeti.
C5A1fexWEAAtNyq.jpg

Jibu kwa Dr kigwangalla

Tutafuatilia ili tuwashauri wanaohusika na 'alosto' hii washughulikie! Nchi haiwezi kuwa ya watu wanaodhani watatajirika kwa bahati nasibu.

NOTE:Ukiona umekosea njia usiongeze mwendo
 
Unamkamata vipi mtu anaebet wakati betting ipo kisheria? Au hizo betting shops ni illegal?

Muuliza swali na aliejibu hawajui wanachoongea.
Hawawezi kufuta ila wanaweza kuweka control ili kupunguza urahisi wa watu ku bet, maana inakua janga hadi kwa watoto, mfano pombe ya konyagi ni legal lakini walipoona inakuwa too much kwa vijana, wakaamua kuondoa za ujazo mdogo ili kupunguza urahisi wa kupata hizo
 
kweli ni tatizo nimeliona muda mrefu hadi nilianzisha uzi kuzungumzia hilo, suprisingly watanzania wengi vijana wanaamini mchezo wa kamari utawatoa kimaisha.

Ku bet sio tatizo ila inaanza kuwa tatizo pale vijana wanapoamini kuwa ni kazi itakayowatoa kimaisha

Namna mchezo wa ku-Bet unavyofanana na Matumizi ya Madawa ya Kulevya
Betting ipo kwa mujibu wa sheria,as long as muhusika ni 18yrs anategemewa kujua anachofanya.

Though nilikuwa sehemu nikaona vijana walivyokuwa busy, wanaombani buku,buku,jero jero ili mradi wabet. Mimi nimekaa hapo mfukoni nina over 200k lakini sithubutu kubet.

Baada ya like two hours alikuja mchina na toyota harrier na mbongo wakafungua ile mashine wakachukua hela za wajinga wakasepa,nilibaki kusikitikia wale vijana huku nikijisemea 'inawezekana kuwa masikini sio bahati mbaya'
 
Hawawezi kufuta ila wanaweza kuweka control ili kupunguza urahisi wa watu ku bet, maana inakua janga hadi kwa watoto, mfano pombe ya konyagi ni legal lakini walipoona inakuwa too much kwa vijana, wakaamua kuondoa za ujazo mdogo ili kupunguza urahisi wa kupata hizo
Yes CONTROL. Hilo ndio wahusika linawashinda. Na bahati mbaya wanaweza kukurupuka na control measures zitakazoua hio biashara badala ya ku improve.
 
Na control inawashinda kwenye vitu vingi sababu hawawashirikishi ipasavyo wahusika wao wapo kimbelembele kutamkatamka.
 
Kwa mfano mm ninajua mtu anafanya kazi kwenye hizo gambling company analipwa mshahara na anakatwa paye yakutosha kulingana na anacholipwa, isitoshe kampuni yenyewe inakatwa kodi ya maana, na isitoshe imetoa ajira kwa makapuni mengi ikiwemo media, mitandao ya simu, shirika la umeme nk. Hivi leo hizo kodi utazipata wapi kama ukiamua kufunga hizi kampuni bila kufikiria, mimi nachoona elimu itolewe na watu wanaopenda kucheza hii michezo wacheze kwa uanaglifu "RESPONSIBLE". Nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea hyo ni official job
 
Hawawezi kufuta ila wanaweza kuweka control ili kupunguza urahisi wa watu ku bet, maana inakua janga hadi kwa watoto, mfano pombe ya konyagi ni legal lakini walipoona inakuwa too much kwa vijana, wakaamua kuondoa za ujazo mdogo ili kupunguza urahisi wa kupata hizo
Mkuu wanatakiwa waweke mkazo kwa vitoto ambavyo vinajazana kwenye betting centres ila kwa kuwa ni mchezo unaojihusisha na 18+ waache waliwe. Binafsi huwa siendi kwenye betting shops. Binafsi na kwa wajanja wengi wanatumia simu na laptop.
 
Hawawezi kufuta ila wanaweza kuweka control ili kupunguza urahisi wa watu ku bet, maana inakua janga hadi kwa watoto, mfano pombe ya konyagi ni legal lakini walipoona inakuwa too much kwa vijana, wakaamua kuondoa za ujazo mdogo ili kupunguza urahisi wa kupata hizo
we inakuuma nini vijana kubet acha ujinga kubet iko dunia yote lakini kwa Tanzania inaonekana kosa mfano ligi ya uingereza makampuni ya kubeti ndio wadhamini wake wakuu achene wivu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom