Dkt Kigwangalla, Margaret Sitta, Emmanuel Adamson Mwakasaka na Mussa Rashid Ntimizi mmelala sana kwenye maendeleo ya jimboni kwenu

CHEF

JF-Expert Member
Nov 4, 2013
222
122
Hapo chini nimewaorodhesha wabunge na mkoa wa Tabora, wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wa viti maalum, awali wabunge tegemezi wa mkoa wa Tabora walikuwa ni Dkt Hamis Andrea Kigwangala na Hussein Mohammed Bashe, Uhodari wao wa kusemea wananchi na kujitolea kidogo wanachokipata kugawana na wananchi kuliwafanya kuonekana viongozi imara na shupavu kwa maendeleo ya Tabora na Tanzania kwa ujumla, lakini kwa sasa amebaki Hussein Bashe tu ambaye anaonekana kuwa kiongozi mwenye maono na Maendeleo ya Tabora, Kingwangala naweza kusema amelisahau jimbo kwa sasa.

Dkt Kigwangala nakuita amka kaka, anza mchaka mchaka, oga maji ya baridi halafu uanze nguvu mpya kuiinua Tabora kulingana na dunia inavyotaka, Wabunge wafuatao wanahitaji kuamshwa na kupewa amsha amsha ili wafanye kazi kwa ajili ya wananchi kwani wamelala sana na hakuna wakuwapa changamoto, hawana mawazo mbadala ya kuleta maendeleo tofauti na mipango ya serikali kuu,

1. Mh. Margaret Simwanza Sitta mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki

2. Mhe. Emmanuel Adamson Mwakasaka Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini

3. Mhe. Munde Abdallah Tambwe mbunge wa viti maalum mkoa wa Tabora

4. Mhe. Joseph George Kakunda Mbunge wa Jimbo la Sikonge

5.Mhe. Selemani Jumanne Zeddy mbunge wa jimbo la Bukene

6. Mhe. Mussa Rashid Ntimizi mbunge wa jimbo la Igalula

7. John Peter Kadutu mbunge wa jimbo la Ulyankulu

8. Mhe. Seif Khamis Said Gulamali mbunge wa jimbo la Manonga

9. Mhe. Almas Athuman Maige Jimbo la Tabora Kaskazini

10 Mhe. Dkt Dalali Peter Kafumu Mbunge wa jimbo la Igunga

11. Mwanne Ismail Mchemba Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora

12. Mhe. Magdalena Hamis Sakaya mbunge wa jimbo la Kaliua

Ndugu wabunge niwakumbushe tu sisi warugaruga tunataka kwenda na kasi ya maendeleo ya Dkt John Pombe Magufuli, sisi warugaruga tunataka kwenda na maendeleo kutokana na dunia inavyotaka, hatujawachagua ili mpumzike, tumewachagua ili muwe chachu ya maendeleo, mpambane kutuonesha njia ya kuitambaua dunia inataka nini na tufanye nini, tunataka Tabora ya leo inayoendana na sayansi na teknolojia. Tusome kwa teknolojia, tulime kwa teknolojia, tufanye biashara kwa teknolojia, tutibiwe kwa teknolojia na tule kwa teknolojia.

Ujumbe uwafikie ndugu wabunge na viongozi wote kwa ujumla
 
wafanye kazi kwa bidii kwani kuna ushindani wa kivyama hapa Tanzania???

si nyie mnaoshanglia kuwa upinzani umekufa??
Kama waliamua kuwatumikia wananchi, wafanye kazi kwa bidii wasilale, waumize vichwa jinsi ya kuifikisha tabora kwenye karne hii ya sayansi ya teknolojia, sisi tunataka uwajibikaji, upinzani utapanda kwa kasi sana kama hakuna uwajibikaji na wananchi wakiona hakuna maendeleo wanayoyapata
 
hakuna maendeleo na uwajibikaji bila kuwa na ushindani.

CCM wanajitapa kuua vyama vya upinzani na matokeo ya hilo ni wabunge wa CCM kubweteka kwasababu hakuna wa kuwashindanisha nao.
 
hakuna maendeleo na uwajibikaji bila kuwa na ushindani.

CCM wanajitapa kuua vyama vya upinzani na matokeo ya hilo ni wabunge wa CCM kubweteka kwasababu hakuna wa kuwashindanisha nao.
Mkuu, wananchi ndio waamuzi wakitaka maendeleo wanaweza kufanya chochote kile, mifano ni mingi sana, Pia Tanzania upinzani upo sana sema upinzani wao wa mashaka , matumbo yao yakiguswa tu wote wanainua mikono juu
 
Wange jiunga na kifurushi cha CHATO ni mitandao yote miaka 10.
Mkuu wananchi tunataka maendeleo, hata Mh: anataka kuona kasi ya maendeleo ni kubwa sio kuunga kifurushi mkuu
 
Na huyo mama Sitta anataka kumuachia hilo jimbo mtoto wake ambae ni meya huko dar.
 
Kigwangala yuko bussy twitter akibishana na mtu asiyemjua anayejiita Kigogo2014
Halafu anasahau kilichomuweka hapo, sisi tunamkumbusha akijisahau asirudi jimboni abaki Dar es Salaam, tunataka maendeleo
 
Na huyo mama Sitta anataka kumuachia hilo jimbo mtoto wake ambae ni meya huko dar.
Hiyo ndio shida sasa, wananchi tukilala tutakuwa tupiga mark time tu huku Dunia inatuacha mwisho wa siku tunakujakuwa watumwa wa maeneo yetu, wenyewe haya hawanyaoni ili mradi familia zao zimeelimika na kupata ahueni ya maisha basi wanasahau hata cha kufanya,au nini wawafanyie wananchi ili tuondoke hapa tulipo
 
Kiongozi asiye na maono ni huyo jamaa per se.
viongozi wasiokuwa na maono sisi waruga ruga tuseme hatuwataki kwa sauti za kupaza ,kwa kizazi hiki watatupeleka gizani halafu vizazi vyetu vitakuwa watumwa kwa hii Dunia inapoelekea
 
Mkoa wa Tabora bado kupata wabunge imara, 2020 tunataka nguvu mpya, tena vijana
Tukiseme kwa pamoja tunataka viongozi wenye maono na wachapakazi, ama kweli tutafika mbali sana na kwa muda mfupi kwa sababu wanatabora ni wachapakazi wazuri sana lakini hawana muongoza njia, miundombinu pia
 
Hiyo ndio shida sasa, wananchi tukilala tutakuwa tupiga mark time tu huku Dunia inatuacha mwisho wa siku tunakujakuwa watumwa wa maeneo yetu, wenyewe haya hawanyaoni ili mradi familia zao zimeelimika na kupata ahueni ya maisha basi wanasahau hata cha kufanya,au nini wawafanyie wananchi ili tuondoke hapa tulipo
Elite families hizo wala hazina habari na majimbo yao huko mikoani,tuko nao huku dar wamejenga maghorofa ya kufa mtu huko masaki.
 
Back
Top Bottom