amshapopo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 723
- 1,233
Habari wanajamvi,
Kiukweli kuunganishiwa umeme kwa jiji la Mbeya, imekuwa kama ni hisani. Nimelipia nguzo ili niunganishiwe umeme laki 567,000 tokea mwezi wa pili lakini hadi leo sijapata huduma ya kuunganishiwa umeme.
Nimefuatilia ofisini kwa mara kwa mara wanasema tutakuja tutakuja lakini hamna kinachofanyika. Kwa maelezo yao kwa mteja wa nguzo baada ya kulipia inabidi akae miezi miwili ili aunganishiwe huduma lakini mpaka sasa ni takribani miezi sita hakuna huduma.
Cha kushangaza zaidi jirani yangu ameomba kuunganishiwa umeme mwezi wa nne lakini ameunganishiwa mapema kabla ya niliyeomba huduma hii mwezi wa pili. Kumuuliza anasema jiongeze ndo utapata umeme lasivyo utasubiri sana.
Sasa najiuliza hivi Tanesco wapo serious kweli na hii biashara? Zaidi ya miezi hii sita ningekua nimenunua umeme wa shilingi ngapi? Kiukweli inauma sana. Leo nimemkuta mzee mmoja analia yeye alilipia tokea mwezi wa kwanza na ndipo nilipochoka zaidi.
SIDHANI KWA MWENDO HUU, KAMA KAULI MBIU YA " TANESCO TUNAANGAZA MAISHA YAKO" Kama ina maana.
Nawasilisha.