Dkt. Kalemani tunaomba imulike TANESCO jiji la Mbeya rushwa imezidi kuunganishiwa umeme

Habari wanajamvi,

Kiukweli kuunganishiwa umeme kwa jiji la Mbeya, imekuwa kama ni hisani. Nimelipia nguzo ili niunganishiwe umeme laki 567,000 tokea mwezi wa pili lakini hadi leo sijapata huduma ya kuunganishiwa umeme.

Nimefuatilia ofisini kwa mara kwa mara wanasema tutakuja tutakuja lakini hamna kinachofanyika. Kwa maelezo yao kwa mteja wa nguzo baada ya kulipia inabidi akae miezi miwili ili aunganishiwe huduma lakini mpaka sasa ni takribani miezi sita hakuna huduma.

Cha kushangaza zaidi jirani yangu ameomba kuunganishiwa umeme mwezi wa nne lakini ameunganishiwa mapema kabla ya niliyeomba huduma hii mwezi wa pili. Kumuuliza anasema jiongeze ndo utapata umeme lasivyo utasubiri sana.

Sasa najiuliza hivi Tanesco wapo serious kweli na hii biashara? Zaidi ya miezi hii sita ningekua nimenunua umeme wa shilingi ngapi? Kiukweli inauma sana. Leo nimemkuta mzee mmoja analia yeye alilipia tokea mwezi wa kwanza na ndipo nilipochoka zaidi.

SIDHANI KWA MWENDO HUU, KAMA KAULI MBIU YA " TANESCO TUNAANGAZA MAISHA YAKO" Kama ina maana.

Nawasilisha.
Dr kalemani,tunamuomba utusaidie kumsisitiza mkurugenzi mkuu wa tanesco ,muhimize apitishe na kuidhinisha miradi ya umeme iliyopo mezani kwake ya mikoa ya Kanda ya ziwa. Kwa kifupi anafanya makusudi na wananchi wapiga kura wetu wanalia yeye anaendelea kuchekelea.Wananchi wamesisitiza kuwa maeneo yasiyo na nishati ya umeme hawatapiga Kura October 28,hivyo inatuwia kazi ngumu kufanya kampeni za chama tawala kwani wananchi walisha haidiwa kupata umeme na Mh Rais tangu mwaka 2018.
 
Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco na waziri wa nishati ninaomba kukujulisha kuwa mkurugenzi waTanesco Tanzania ana matatizo kwenye utendaji wake especially kupitishwa miradi ya umeme mikoani.unakuta mameneja wa Tanesco mikoani wametuma bajeti za miradi mipya ya kusambaa umeme mikoani kwa wateja, mkurugenzi mkuu wa tanesco anakalia miradi hiyo kwa zaidi ya mwaka mzima bila utekelezaji kuipitisha ifanyike au kutuma fedha ili miradi ufanyike.

Hili tatizo limeendelea kuwa kubwa sana haswa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa ambsjo maeneo mengi hayajawahi kupata nishati ya umeme tangu nchi ipate uhuru.ombi tunamuomba mkurugenzi mkuu wa tanesco apitishe miradi iliyotumwa kwake na meneja wa Tanesco mikoa na ipo mezani kwake ili utekelezaji wa miradi hiyo uweze kufanyika kwa wakati.

Tunatarajia atasikia kilio hiki ili siku ya kupiga Kura October 28,wananchi wasipigie kura gizani kwani Mh Rais Alisha toa ahadi ya kila mtanzania kupata nishati ya umeme.
Ndugu mpendwa mteja wetu taarifa yako inapaswa kuonyesha kijiji gani unalalamikia namba yako ya simu tafadhali
 
Habari wanajamvi,

Kiukweli kuunganishiwa umeme kwa jiji la Mbeya, imekuwa kama ni hisani. Nimelipia nguzo ili niunganishiwe umeme laki 567,000 tokea mwezi wa pili lakini hadi leo sijapata huduma ya kuunganishiwa umeme.

Nimefuatilia ofisini kwa mara kwa mara wanasema tutakuja tutakuja lakini hamna kinachofanyika. Kwa maelezo yao kwa mteja wa nguzo baada ya kulipia inabidi akae miezi miwili ili aunganishiwe huduma lakini mpaka sasa ni takribani miezi sita hakuna huduma.

Cha kushangaza zaidi jirani yangu ameomba kuunganishiwa umeme mwezi wa nne lakini ameunganishiwa mapema kabla ya niliyeomba huduma hii mwezi wa pili. Kumuuliza anasema jiongeze ndo utapata umeme lasivyo utasubiri sana.

Sasa najiuliza hivi Tanesco wapo serious kweli na hii biashara? Zaidi ya miezi hii sita ningekua nimenunua umeme wa shilingi ngapi? Kiukweli inauma sana. Leo nimemkuta mzee mmoja analia yeye alilipia tokea mwezi wa kwanza na ndipo nilipochoka zaidi.

SIDHANI KWA MWENDO HUU, KAMA KAULI MBIU YA " TANESCO TUNAANGAZA MAISHA YAKO" Kama ina maana.

Nawasilisha.
Mambo ni hivyohivyo hata Wilaya ya Kibamba, Dar es Salaam. Sema Mhe. Kalemani nae hapokei simu yake kwa namba aliyoweka kwenye tovuti ya Bunge, ukipiga inaita weee na kukata yenyewe. Ila TANESCO wanahimiza sana rushwa, maana utakaza wee ila mwisho wa siku utatoa tu hela uletewe umeme
 
TANESCO rushwa imekuwa kama kawaida.
Nimejaza fomu naambiwa nimlipe surveyer aje chap. Nikatoa RUSHWA (JAPO NAJUA NI KOSA)
siku hiyo hiyo akaja.
Baada ya siku 10hv nimeitwa kulipia gharama za kuunganishiwa. Nako wameomba RUSHWA kwa kuwa fomu imepitia shot cut.

Hapa nasubiri kuletewa mita nione wataomba tena ngapi.

Na wote waliounganishwa WAMETOA RUSHWA LAA SIVYO UNAKAA MPAKA BASI
Pole sana mpendwa mteja wetu tafadhali tusaidie mwa siri kuwa na nani alipokea rushwa namba yako ya simu kwa hatua zaidi
 
Mambo ni hivyohivyo hata Wilaya ya Kibamba, Dar es Salaam. Sema Mhe. Kalemani nae hapokei simu yake kwa namba aliyoweka kwenye tovuti ya Bunge, ukipiga inaita weee na kukata yenyewe. Ila TANESCO wanahimiza sana rushwa, maana utakaza wee ila mwisho wa siku utatoa tu hela uletewe umeme
Tatizo gani mkuu onyesha namba yako ya simu kwa hatua zaidi
 
Pole sana mpendwa mteja wetu tafadhali tusaidie mwa siri kuwa na nani alipokea rushwa namba yako ya simu kwa hatua zaidi
Unataka namba yake ya simu ya nini? Bila namba yake ya simu hamuwezi kumsaidia?

Au mnataka kumteka?
 
Pole sana mpendwa mteja wetu tafadhali tusaidie mwa siri kuwa na nani alipokea rushwa namba yako ya simu kwa hatua zaidi

Ifike sehemu mtambue ya kwamba hii ni biashara kama biashara zingine mtu anapolipia anatakiwa afanyiwe huduma fasta lakini mnapoleta maswala sijui ya siku 90 mara siku 60 wakati mtu kashalipia inakuwa haipendezi.

Ifahamike kuwa huduma yenu ni mbovu sana kwa wananchi na tena kwa hao wafanyakazi wenu wanaweka rushwa mbele sana kuliko kufanya huduma uliyowapeleka hapo ofisini, haiwezekani mtu kalipia tokea mwezi wa kwanza lakini hadi leo unazungushwa tu.

Basi kama ni hivyo mnatakiwa muwaweke wazi wananchi kwamba kuleta survey ni bei kadhaaa, kuja kufungiwa umeme ni bei kadhaa ili muweze kuondoa hii sitofahamu kati ya wananchi na wafanyakazi wenu.

Hizi tabia za mtu ameshalipia harafu anasubiri miezi miwili mara mitano inakera sana.
 
Tafadhali onyesha ushirikiano wa nani umempa rushwa? Au peleka TAKUKURU unapotoa malalamiko bila taarifa kamili maana yake haupo tayari kumaliza tatizo hilo ulilodai kuwepo
 
yaani TANESCO mnajifaraguza hapa eboo

Fanyieni kazi hayo matatizo sio kusema eti tupe namba yako ki siri siri
Tunawasihi wateja wetu kujenga utaratibu wa kutoa taarifa kamili unapolalamika kwa taarifa isiyokamili unakuwa haujatusaidia kukuhudumia vema.unaweza kutupatia hapa au kupeleka TAKUKURU vinginevyo inakuwa ngumu sisi kuchukua hatua
 
Tafadhali onyesha ushirikiano wa nani umempa rushwa? Au peleka TAKUKURU unapotoa malalamiko bila taarifa kamili maana yake haupo tayari kumaliza tatizo hilo ulilodai kuwepo

Sasa kama umetoa rushwa na umepata huduma haraka kuna haja gani ya kwenda TAKUKURU?

Kwa mtu ambae ana hali ya chini hawezi kupata huduma kwa haraka maana uwezo wa kutoa rushwa hana ndiyo maana tunasisitiza huduma itolewe kwa haraka bila kujali tajiri au masikini kikubwa mtu amelipia ili aweze kupata huduma.

Hao wafanyakazi wenu baadhi ya ofisi wanapoleta maswala ya kusema una shilingi ngapi hapo tukufanyie huduma kwa haraka inaleta picha mbovu sana kwa shirika lenu.
 
Ndugu mpendwa mteja wetu taarifa yako inapaswa kuonyesha kijiji gani unalalamikia namba yako ya simu tafadhali
Dr kalemani,tunamuomba utusaidie kumsisitiza mkurugenzi mkuu wa tanesco ,muhimize apitishe na kuidhinisha miradi ya umeme iliyopo mezani kwake ya mikoa ya Kanda ya ziwa. Kwa kifupi anafanya makusudi na wananchi wapiga kura wetu wanalia yeye anaendelea kuchekelea.Wananchi wamesisitiza kuwa maeneo yasiyo na nishati ya umeme hawatapiga Kura October 28,hivyo inatuwia kazi ngumu kufanya kampeni za chama tawala kwani wananchi walisha haidiwa kupata umeme na Mh Rais tangu mwaka 2018.
 
Ndugu mpendwa mteja wetu taarifa yako inapaswa kuonyesha kijiji gani unalalamikia namba yako ya simu tafadhali
Mikoa ya Kanda ya ziwa huijui? Mkurugenzi mkuu wa tanesco analijua miradi ambayoinatakiwa ipitishwe na hajaipitisha .una Tabia ya kudai namba za simu kila unapokutana na malalamiko yanayohusu Tanesco. Namba yangu hii hapa 0754-562366
 
Tanesco sikuhizi yaani umeme mnakata tuu kila siku wiki hii karibu yote, twambieni kama kuna mgao ili tujue maana vitu vinaharibika tu.
Goba hii
 
Mikoa ya Kanda ya ziwa huijui? Mkurugenzi mkuu wa tanesco analijua miradi ambayoinatakiwa ipitishwe na hajaipitisha .una Tabia ya kudai namba za simu kila unapokutana na malalamiko yanayohusu Tanesco. Namba yangu hii hapa 0754-562366
Ahsante sana tutawasiliana na wewe kujua ni mradi gani unaodai
 
Back
Top Bottom