Dkt. Kalemani tunaomba imulike TANESCO jiji la Mbeya rushwa imezidi kuunganishiwa umeme

amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
374
500
Habari wanajamvi,

Kiukweli kuunganishiwa umeme kwa jiji la Mbeya, imekuwa kama ni hisani. Nimelipia nguzo ili niunganishiwe umeme laki 567,000 tokea mwezi wa pili lakini hadi leo sijapata huduma ya kuunganishiwa umeme.

Nimefuatilia ofisini kwa mara kwa mara wanasema tutakuja tutakuja lakini hamna kinachofanyika. Kwa maelezo yao kwa mteja wa nguzo baada ya kulipia inabidi akae miezi miwili ili aunganishiwe huduma lakini mpaka sasa ni takribani miezi sita hakuna huduma.

Cha kushangaza zaidi jirani yangu ameomba kuunganishiwa umeme mwezi wa nne lakini ameunganishiwa mapema kabla ya niliyeomba huduma hii mwezi wa pili. Kumuuliza anasema jiongeze ndo utapata umeme lasivyo utasubiri sana.

Sasa najiuliza hivi Tanesco wapo serious kweli na hii biashara? Zaidi ya miezi hii sita ningekua nimenunua umeme wa shilingi ngapi? Kiukweli inauma sana. Leo nimemkuta mzee mmoja analia yeye alilipia tokea mwezi wa kwanza na ndipo nilipochoka zaidi.

SIDHANI KWA MWENDO HUU, KAMA KAULI MBIU YA " TANESCO TUNAANGAZA MAISHA YAKO" Kama ina maana.

Nawasilisha.
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
1,320
2,000
Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco na waziri wa nishati ninaomba kukujulisha kuwa mkurugenzi waTanesco Tanzania ana matatizo kwenye utendaji wake especially kupitishwa miradi ya umeme mikoani.unakuta mameneja wa Tanesco mikoani wametuma bajeti za miradi mipya ya kusambaa umeme mikoani kwa wateja, mkurugenzi mkuu wa tanesco anakalia miradi hiyo kwa zaidi ya mwaka mzima bila utekelezaji kuipitisha ifanyike au kutuma fedha ili miradi ufanyike.

Hili tatizo limeendelea kuwa kubwa sana haswa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa ambsjo maeneo mengi hayajawahi kupata nishati ya umeme tangu nchi ipate uhuru.ombi tunamuomba mkurugenzi mkuu wa tanesco apitishe miradi iliyotumwa kwake na meneja wa Tanesco mikoa na ipo mezani kwake ili utekelezaji wa miradi hiyo uweze kufanyika kwa wakati.

Tunatarajia atasikia kilio hiki ili siku ya kupiga Kura October 28,wananchi wasipigie kura gizani kwani Mh Rais Alisha toa ahadi ya kila mtanzania kupata nishati ya umeme.
 
dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,550
2,000
Huu ni mda wa kampeni; Subiri wamalize kampeni mengine yatafuata!
 
MC44

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
1,240
2,000
TANESCO rushwa imekuwa kama kawaida.
Nimejaza fomu naambiwa nimlipe surveyer aje chap. Nikatoa RUSHWA (JAPO NAJUA NI KOSA)
siku hiyo hiyo akaja.
Baada ya siku 10hv nimeitwa kulipia gharama za kuunganishiwa. Nako wameomba RUSHWA kwa kuwa fomu imepitia shot cut.

Hapa nasubiri kuletewa mita nione wataomba tena ngapi.

Na wote waliounganishwa WAMETOA RUSHWA LAA SIVYO UNAKAA MPAKA BASI
 
Yaani mkuu najiuliza hili shirika linafanya biashara gani. Yaani mteja anakuletea hela unamuomba rushwa tena. Mbona idara ya maji hamna ujinga kama huu?
 
JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,758
2,000
TANESCO rushwa imekuwa kama kawaida.
Nimejaza fomu naambiwa nimlipe surveyer aje chap. Nikatoa RUSHWA (JAPO NAJUA NI KOSA)
siku hiyo hiyo akaja.
Baada ya siku 10hv nimeitwa kulipia gharama za kuunganishiwa. Nako wameomba RUSHWA kwa kuwa fomu imepitia shot cut.

Hapa nasubiri kuletewa mita nione wataomba tena ngapi.

Na wote waliounganishwa WAMETOA RUSHWA LAA SIVYO UNAKAA MPAKA BASI
Takukuru njooni mmchukue huyu mteja wenu
 
tibe_j

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
428
1,000
Mbeya wamezidi mimi nilikaa miez 5 tulisumbuana sana wanajibu shortcut tu as if mtu umeenda kuomba msaada kumbe unadai haki yako ...niliwatolea uvivu hao wadada wa reception hadi nikafika kwa meneja akanitatulia ndani ya week moja.
 
Kumbe dawa ni kuwa na sura ya mbuzi
 
MoneyHeist4

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
769
1,000
TANESCO rushwa imekuwa kama kawaida.
Nimejaza fomu naambiwa nimlipe surveyer aje chap. Nikatoa RUSHWA (JAPO NAJUA NI KOSA)
siku hiyo hiyo akaja.
Baada ya siku 10hv nimeitwa kulipia gharama za kuunganishiwa. Nako wameomba RUSHWA kwa kuwa fomu imepitia shot cut.

Hapa nasubiri kuletewa mita nione wataomba tena ngapi.

Na wote waliounganishwa WAMETOA RUSHWA LAA SIVYO UNAKAA MPAKA BASI
Umeongea ukweli mtupu sema tunajificha lakini wengi huduma tunaipata kwa njia hiyo hiyo.

Huenda wafanyakazi wao huwa hawalipwi hela nzuri juu ya kazi yao ya kuhatarisha maisha ndo maana wanajikuta wanapokea rushwa.
 
KARIA

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
717
500
Hili ni tatizo kubwa mno kwa Tanesco, nimeomba savior handeni tangu mwezi wa tatu mpaka leo hajaja.
 
amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
374
500
Yaani si kwao wanaona ni kawaida tu. Yaani ni bora kungekua na mbadala wa Tanesco huenda wangenyooka
 
FUTURE HUNTER

JF-Expert Member
Apr 30, 2018
1,637
2,000
Yaani haya mashirika ya serikali ni hovyo kabisa.Hayapo kibiashara zaidi ya rushwa na ukiritimba ili upate huduma.
Namuonea huruma ngosha anayerudisha biashara ifanywe na taasisi za serikali.
 
amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
374
500
Yaani haya mashirika ya serikali ni hovyo kabisa.Hayapo kibiashara zaidi ya rushwa na ukiritimba ili upate huduma.
Namuonea huruma ngosha anayerudisha biashara ifanywe na taasisi za serikali.
Yaani mkuu unaweza hata kuwachapa ngumi kwa hasira. Hawapo kibiashara kabisa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom