Dkt. Kalemani awacharukia wanaotoza bei kubwa za umeme

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1594217134773.png


Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, ametoa onyo kali kwa wazalishaji binafsi wa umeme, wanaowatoza wananchi gharama kubwa tofauti na bei elekezi ya Serikali. Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kahunda, wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Julai 7, 2020, Waziri alisisitiza kuwa gharama stahiki ya umeme kwa wananchi wote wenye matumizi ya kawaida ni shilingi 100 tu kwa uniti moja. Alisema, wananchi wanapaswa kutozwa gharama inayofanana katika maeneo yote nchini kwani wote wana haki sawa.

“Bei hiyo ni kwa maeneo yote nchini vikiwemo visiwa na ni kwa umeme wa aina zote pasipo kujali ni wa TANESCO au kutoka kwa wazalishaji binafsi wanaotumia umeme jua na aina nyinginezo,” alisisitiza Waziri.

Alitoa agizo kwa viongozi wa Serikali, hususan Wakuu wa Wilaya kote nchini, kuwachukulia hatua wazalishaji binafsi wa umeme, watakaobainika kukiuka mwongozo huo wa Serikali. Alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi mbalimbali, hususani wanaoishi visiwani, kwamba wamekuwa wakitozwa gharama kubwa na wawekezaji binafsi wa umeme hali inayosababisha wengi wajisikie kama wakimbizi ndani ya nchi yao. Waziri alisema kamwe Serikali haitavumilia tabia za aina hiyo zinazooneshwa na baadhi ya wawekezaji binafsi wa umeme kwani imewaamini kutenda haki katika kuwafikishia umeme wananchi hao ambao hawajafikiwa na gridi ya Taifa.

Hata hivyo, alibainisha kuwa Serikali inaendelea na zoezi la kupeleka umeme wa gridi ya Taifa katika visiwa vyote nchini kwa kupitisha nyaya chini ya maji yanayozunguka visiwa hivyo. Aliwataka wananchi wa visiwani ambao hawajafikiwa na huduma hiyo kuwa watulivu kwani huduma hiyo itawafikia wote awamu kwa awamu. Akiwa katika Mkutano huo, Waziri aliagiza kukamatwa na kuhojiwa wawakilishi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa jua iitwayo Jumeme, baada ya wananchi wa kisiwa cha Maisome wilayani humo, kuwatuhumu kuwa wamekuwa wakiwauzia umeme kwa gharama ya shilingi 3,500 kwa uniti moja.
 
Kwani huyu naye bado atachaguliwa? Huyu niliyesikia matendo yake? Nadhani ifikie hatua kabla ya kuchaguliwa tujue moral correctness ya mtu.
 
Tatizo ni kuleta Siasa katika kila Jambo , haiwezekani bei ikawa sawa kila mahali , hata mafuta pamoja Na kuwa yapo regulated hayapo sawa kila mahali .

TANESCO shirika lenye wateja wanaokadiliwa 4Million linatoza almost 357 Tshs per unit ( KWh ) pamoja Na Vat Na Tozo zingine .. fact ni kwamba hata tukitoa VAT , Ewura Na REA tozo bado Gharama ya Unit moja ni zaidi ya 250Tshs per unit .hapa tukumbuke kuwa hili shirika bado linapokea Ruzuku toka serikalini , wateja wa vijiji I wanalipa kidogo kwa kuwa wateja wa mjini wanawalipia ..

Malipo ya unit moja ya yanategemea mambo yafuatayo .
1. Gharama za kujenga plant au min grid , Gharama hizi hutofautina Kulingana Na mahali , Mfano kujenga mtambo Dar ni rahisi kuliko Ngorongoro au Bukoba
2. Idadi ya wateja , idadi kubwa ni nafuu kwa Mteja
3. Aina ya Min Grid , Hydro power mingrid ni cheaper than Solar Min grid .

4. Gharama za Uendeshaji.

5. Pay back time , kumbuka kila Mwekezaji anatakiwa kupata pesa take back au kulipa mkopo wake bank .

Nini cha kufanya .

Badala ya kuja Na bei moja kila mahali ni vyema Serikali ikakaa Na wadau na kuchanganua Gharama Na kuja Na bei elekezi kwa kila mahali Na kwa Aina ya umeme .

Kutamka tu kama hivi kutaua Private sector iliyowekeza kwenye eneo hilo .
 
Back
Top Bottom