Dkt. Joseph Kasheku Msukuma: Sasa nina hadhi kubwa duniani kisiasa. Naweza kuitwa nchi yoyote kuwa msuluhishi wa kisiasa

"PhD ya Siasa na Uongozi ni Shahada kubwa sana kimataifa, kwa kuwa Taifa lolote linaongozwa na siasa pamoja na uongozi. Mimi kwa sasa naweza kuitwa Marekani, Liberia, India kama kuna mgogoro na kwenda kusuluhisha, hizi PhD ni chache sana duniani" Dkt.Joseph Msukuma
https://t.co/qxUmXsmHfu
View attachment 2034836
Si huyu huyu alikuwa anazidharau hizo PhD... Sasa inakuwaje leo anazipapatikia, tena za kununua.
 
"PhD ya Siasa na Uongozi ni Shahada kubwa sana kimataifa, kwa kuwa Taifa lolote linaongozwa na siasa pamoja na uongozi. Mimi kwa sasa naweza kuitwa Marekani, Liberia, India kama kuna mgogoro na kwenda kusuluhisha, hizi PhD ni chache sana duniani" Dkt.Joseph Msukuma
https://t.co/qxUmXsmHfu
View attachment 2034836
Hata kufanya mihadhara ya vyuo vikuu vikubwa duniani unaweza,, PI Hechi Dii si mchezo sheikh, ila kwa kuanza anzia pale Mlimani ya U-Dom kuna wanafunzi wa Science ya siasa anza kuwafua fua.
 
Phd holder Dr.Joseph Msukuma.
Dunia inaenda kasi sana wakuu.
Hadhi ya tuzo yoyote ile inayotolewa kwa mtu, kampuni ama taasisi yoyote ile inategemea pia hadhi ya mtoa tuzo. Ili tuzo ikapate kuaminika na kukubalika mbele ya jamii, basi ni lazima mchango wa muhusika kwenye nyanja fulani ya maisha uwe wenye kutambulika wa wabobezi wa mambo, wataalamu ikiwamo na wanataaluma pia.

Hii ndiyo maana hadhi ya tuzo lazima iwe "accredited" kuwa na "accreditation" kwa kuwa utoaji wa tuzo huendana na ubora wa kitaifa, kikanda na kimataifa. Kwa hiyo ni rahisi sana kwa Mh. Msukuma kusema kuwa sasa anatambulika kimataifa huku akisahau kuhusu hadhi ya tuzo aliyopewa na hadhi ya mtoa tuzo hiyo.

Kwa ulimwengu wa sasa hakuna siri kwa kuwa technolojia ya habari na mawasailiano inaweza kubainisha hilo. Kwa hivyo ni vyema akatulia ili hadhi yake mwenyewe imtetee yenyewe kuliko hicho anachoamini amekipata.
 
Ha ha ha ha ha cheki alivyosimama kama mgambo swahiba wake angelikuwepo kwa kutaka sifa angelimpa unaibu waziri kweli awamu ya tano tuliyakanyaga kuwapa washamba nchi
 
shes-gotta-have-it-laughing.gif
 
Huyu jamaa bado anarandaranda mtaani tu ? Ati tangu 2017 anafanyiwa dissection ya kupata PHD. Hana taarifa kuna wasomi hapo wenye PHD wanahaha kupata visa kwenda nchi za watu .ama yake ni mpya .nashauri akamatwe achapwe viboko 12 then awekwe Ndani 12 akitoka akawaonyeshe wapiga Kura wake. Huyu chalii asituchezee akili.
 
Kwakweli dunia hii ina maajabu yakee Leo msukuma ana PhD hata Course work hajuii maana akeee jamani jamani hii dunia kuwa na hela Tu kila kit kitakuwa Rahisi kwako, na Hilo suala mm sishangai coz yupo TENA mwingine aliyechukua degree yake ndani ya mwaka mmoja tuu
 
"PhD ya Siasa na Uongozi ni Shahada kubwa sana kimataifa, kwa kuwa Taifa lolote linaongozwa na siasa pamoja na uongozi. Mimi kwa sasa naweza kuitwa Marekani, Liberia, India kama kuna mgogoro na kwenda kusuluhisha, hizi PhD ni chache sana duniani" Dkt.Joseph Msukuma

View attachment 2034836
Yaani huyu mdau kajimaliza kisiasa. Na waliomuandalia hili tukio wana akili sana. Yaani 2025 hawezi kupita tena. Vyombo vya habari vitalipwa ili wamuandike ana elimu fake. Ikija NEC watamkata kwa sababu ya kukosa weledi wa kuwa na elimu fake. In short poor mind yake imepelekea kujikaanga. He will never rise again kumuongelea Dkt Magufuli kwa sababu hakuna atakaye mchukulia serious kwa sababu ana elimu fake. Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom