Dkt. John Pombe Magufuli akikubali tu, niko tayari kumpokea kijiti hicho 2025

Dkt John Pombe Magufuli ni mwananchi namba 1, kiongozi namba 1, na mtawala namba 1.

Akiafiki atakuwa na uwezo mkubwa wa kuwaeleza wananchi wenzetu kwa nini mimi na si mwingine

Briefly, huu ni muda wa kuomba kuaminiwa na taasisi ya CCM, kisha wananchi watatupima na kufanya maamuzi kwa wakati mwingine ufuatao
Wewe hata ukiwa rais utakuwa unaendeshwa kwa remote control na huyo Magufuli.

Nitakupa story ya Mzee mmoja namfahamu na kumuheshimu sana.

Huyo Mzee alitambulika kazini kwake kwamba ni gwiji wa kazi, kazi anaijua, ni kichwa.

Sasa, ikatokea kwamba, bosi wake ambaye ni kiongozi wa shirika anastaafu, anatakiwa ateuliwe mtu mwingine kuwa kiongozi wa Shirika.

Sasa watu wakaanza kujinadi na kutafuta network ya kuteuliwa.

Hapo utawala wa Mwinyi. Yule Mzee alikuwa anajuana na John Shibuda. Enzi hizo John Shibuda kada mkubwa sana CCM.

Basi John Shibuda akamfuata yule Mzee. Akamwambia, mzee mwenzangu, ukubwa hauji hivi hivi tu, inabidi upaliliwe na kumwagiliwa, inabidi tuanze kukujengea mazingira ya kuteuliwa.Tupange siku nikupeleke Ikulu kwa Mwinyi nikutambulishe, Mwinyi akuone, nitie neno, uteuliwe.

Basi yule Mzee aliyeambiwa hivyo, kwa kumheshimu Shibuda, akasema tu sawa, nitakutafuta.

Halafu hakumtafuta, akaipotezea kabisaa ile habari. Yeye akaendelea kupiga kazi tu.

Bada ya muda, akateuliwa mtu mwingine kukaimu ile nafasi. Jamaa hakukaa hata miezi sita akapiga hela kubwa, akaondolewa.

Mwinyi akaangalia, akamteua yule Mzee ambaye Shibuda alitaka kumpa intro finally.

Nikamuuliza yule Mzee aliyekataa into, pale mbona kama umecheza mchezo hatari? Kwa nini ulimpotezea Shibuda?

Mzee akasema, anayeteua ni rais, kama angetaka kuniteua angeniteua tu ikiwa nimeenda na Shibuda au sijaenda.

Pia, ningeenda na Shibuda halafu nikateuliwa, uongozi wangu ungekuwa wa ubia na Shibuda, ningekuwa na deni kubwa sana kwake.

Hakutaka hilo.

Wewe unataka urais wako uwe na deni kwa Magufuli, si kuongoza wananchi.

Una focus kwa mtu amabaye hana mandate ya kuchagua rais, badala ya kutafuta ridhaa ya watu wenye mandate ya kuchagua rais.

Kwa taarifa yako tu, Nyerere alitaka Salim awe rais, Mkapa alitaka Dr Omar Ali Juma awe rais, Dr Omar alipofariki Mkapa akataka Abdallah Kigoda awe rais, Kikwete alitaka Membe awe rais.

Wote hawakufanikiwa.
 
Hivyo hivyo nami napenda Rais Magufuli akubali
 
Wewe una asili ya kujipendekeza, si asili ya kuongoza.
Sawa, huo unaweza kubaki kuwa mtizamo wako - bahati nzuri palipo na wengi hupatikana - na sidhani iwapo kujipendekeza kwangu kutariathiri taifa na watu wake
 
Sio mtizamo wangu tu, ni mantiki.

Kama wanaomchagua rais ni Watanzania, na wewe unajikita kwa Magufuli ili ukubalike, unatafuta shortcut kwa kujipendekeza.

Bahati nzuri mpaka sasa unapiga hadithi na kuota njozi tu.

Wanaoutaka urais hawatangazi hivi JF, na wanaotangaza hivi JF hawana nia ya urais.

Wanapiga soga tu.

Ila wewe umezidi. Hata katika soga unaboronga.
 
God and time!
Hatutatumia njia moja kuifikia hadhira - hatutawaza mamoja na wala wote hawatakuwa waoga wa kutoa hisia zao - upo wakati wangu, utakuja wakati wako kisha wakati wa wengine.

Urais ni taasisi sawa na taasisi zingine ingawa kwa sababu ya structure ya kiuongozi imepewa authorative power kubwa, hatutapata kiongozi toka mbinguni au sayari nyingine - kiongozi atatoka miongoni mwetu (tuliyecheza nae utotoni, tuliyesoma nae darasani, tunayeshiriki nae masuala ya kijamii, na pengine tuliyefanya nae kazi "iwe ofisini, kugonga kokoto, kusukuma mkokoteni, kuimba mziki, kulima shambani nk nk)

Hata nisipopata mimi nafasi hiyo bado atapata mwingine ambaye nae si Mungu, si malaika bado taifa litaongozwa.
 
Hicho kichwa kilivyobonyea hapo kwenye utosi ndio uwe raisi wa nchi ?

Labda uwe raisi wa FM ACADEMIA
Sikujiumba, niliumbwa - hututatafuta big brother wala mlembwende. Hatujawahi kuwa na mashindano ya sura za presidents duniani wanaopimwa kwa uzuri wa sura wala maumbile.

Iwapo zipo sababu za kunidisqualify basi ziwe kwanza za kiuwezo (administrative), kiuono (planning & economic aspects).
 
God and time!
Hatutatumia njia moja kuifikia hadhira - hatutawaza mamoja na wala wote hawatakuwa waoga wa kutoa hisia zao - upo wakati wangu, utakuja wakati wako kisha wakati wa wengine.

Urais ni taasisi sawa na taasisi zingine ingawa kwa sababu ya structure ya kiuongozi imepewa authorative power kubwa, hatutapata kiongozi toka mbinguni au sayari nyingine - kiongozi atatoka miongoni mwetu (tuliyecheza nae utotoni, tuliyesoma nae darasani, tunayeshiriki nae masuala ya kijamii, na pengine tuliyefanya nae kazi "iwe ofisini, kugonga kokoto, kusukuma mkokoteni, kuimba mziki, kulima shambani nk nk)

Hata nisipopata mimi nafasi hiyo bado atapata mwingine ambaye nae si Mungu, si malaika bado taifa litaongozwa.
Moja ya matatizo makubwa yanayosababisha umasikini wa hali na mali ni fikra za kuangalia viongozi zaidi badala ya kuangalia wananchi.

Na wewe hujaweza kuvuka mtego huu, hivyo, ukiendelea kuwa hivyo, hata ukipata uongozi, huwezi kuwa kiongozi mzuri.

Utaingia kwenye uongozi na kukuta interests za viongozi ni tofauti na za wananchi. Viongozi interests zao karibu mara zote ni kuendelea kuwa madarakani, hata kwa kuiba fedha za uma na kuharibu uchumi wa nchi. Ukisoma kitabu cha Mkapa utaona alivyokubali kwa aibu kwamba alihusika na ubadhirifu wa hela za EPA, amejifaragua kusema kwamba ameingizwa choo cha kike bila kujua. Mr. Clean, long time diplomat, Editor-In-Chief unamuingizaje choo cha kike kirahisi hivyo kama mtu mshamba? Alikula deal.

Sasa huyo ndiyo Godfather wa unayetaka awe Godfather wako.

Magufuli akikwambia nitakusaidia upate urais, lakini huwa tunapiga hela za uchaguzi kutoka pesa za umma, tupige hapa na pale, utaweza kumkatalia?
 
"Future is elusive" - mchakato wa kupata kiongozi una hatua nyingi baadhi tu ni:-
(i). Taasisi ya chama cha siasa kukuamini, kukusimamia na kukukubali (hapa mwenye chama ni Dkt John Pombe Magufuli kama mwenyekiti) no way unaweza kufikiria kuvuka iwapo hamuaminiani;

(iii). Ushindanishwaji na wagombea wa vyama vingine vya siasa (hapa ndipo wananchi wanapopima wagombea generally na kuamua nani wampitishe kuwaongoza). Sasa ninaposema Dkt John Pombe Magufuli akikubali namaanisha michakato ya awali kisha inayofuata ndiyo itakayoamuliwa na wananchi.

Kuhusu rushwa, hilo siwezi kulizungumzia sababu hata wewe unayelileta huna ushahidi nalo - sasa hatuwezi kuongozwa na hisia pale tunapohukumu wenzetu.

Dhamira kuu ni kuacha legacy isiyofutika "katiba mpya, miundombinu, ajira kwa vijana, ubora na uimara wa sekta binafsi, elimu ya juu nk nk" ni baadhi ya vitu nionavyo muhimu kuanza navyo.
 
Hii nchi ilibidi iongozwe na watu ambao wamefsnya mambo ya pekee kwa jamii, mtu Kama Bakheresa,Charles Kimei, Tundu Lisu, January Makamba, kuliko kuwapa watu wanaotaka kutajirika kupitia migongo ya Watz.
Ktk jamii Tundu Lissu kafanya kipi? Au unasema Tundu Lissu mwingine si huyu wa Ikungi?

Nitawafaa sana
 
Back
Top Bottom